Tafuta

Serikali imesimamia kwa umakini mkubwa zoezi la uwekaji vigingi kwenye hilo ambalo ni muhimu kwa ikolojia ya Hifadhi ya Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Serikali imesimamia kwa umakini mkubwa zoezi la uwekaji vigingi kwenye hilo ambalo ni muhimu kwa ikolojia ya Hifadhi ya Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.  (ANSA)

Muhimu: Vigingi Loliondo, Elimusingi na Senza ya Watu na Makazi Agosti 2022

Zoezi la uwekaji wa vigingi katika eneo la kilometa za mraba 1,500 la Pori Tengefu la Poloreti-Loliondo ambalo limekamilika kwa asilimia 100 halitoathiri maendeleo ya wakazi waishio kwenye eneo la vijiji 14 vinavyopakana na eneo hilo. Hakutakuwepo na kijiji chochote kitakachofutwa na hakuna miundombinu itakayoondolewa kwa kuwa ndani ya eneo la kilometa za mraba 1,500.

Na Ofisi ya Waziri Mkuu Dodoma, - Dodoma.

Waziri mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amesema zoezi la uwekaji wa vigingi katika eneo la kilometa za mraba 1,500 la Pori Tengefu la Poloreti-Loliondo ambalo limekamilika kwa asilimia 100 halitoathiri maendeleo ya wakazi waishio kwenye eneo la vijiji 14 vinavyopakana na eneo hilo. Hata hivyo, Mheshimiwa Majaliwa amesisitiza kwamba hakutakuwepo na kijiji chochote kitakachofutwa na hakuna miundombinu itakayoondolewa kwa kuwa ndani ya eneo la kilometa za mraba 1,500 hakuna miundombinu yoyote. Ameyasema hayo hivi karibuni wakati akitoa Hoja ya Kuahirisha Mkutano wa Saba wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bungeni jijini Dodoma. Amesema    Serikali imesimamia kwa umakini mkubwa zoezi la uwekaji vigingi kwenye hilo ambalo ni muhimu kwa ikolojia ya Hifadhi ya Serengeti na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Mheshimiwa amesema Serikali imeendelea kushirikiana na wananchi wa Loliondo katika kuboresha malisho ya mifugo, uchimbaji wa visima vya maji, ujenzi wa majosho pamoja na miundombinu ya kunyweshea mifugo kwenye eneo la kilometa za mraba 2,500. “Pianinaielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kushirikiana na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi pamoja na wadau wengine kuhakikisha kuwa Sheria ya Ardhi ya vijiji namba 5 ya mwaka 1999 inatumika ipasavyo kutenga na kuweka mipaka ya vijiji.”

Mkazo ni elimumsingi bute kwa watoto wote Tanzania
Mkazo ni elimumsingi bute kwa watoto wote Tanzania

Amesema Serikali kwa kuzingatia matakwa ya wananchi hasa maeneo ya malisho kwenye vijiji 14 vilivyopo karibu na Pori Tengefu la Poloreti itaweka utaratibu utakaopangwa kwa pamoja baada ya kukamilisha zoezi la utambuzi wa mifugo kwenye vijiji husika. Mheshimiwa Majaliwa amesema katika kuhakikisha uwepo wa matumizi endelevu ya Pori Tengefu la Poloreti, Serikali ilielekeza eneo la kilometa za mraba 1,500 lihifadhiwe na eneo lililobaki la kilometa za mrada 2,500 wananchi waendelee kulitumia kwa shughuli nyingine. Akizungumzia kuhusu zoezi la wakazi wa Ngorongoro kuhama kwa hiari katika eneo kwa ajili ya kupisha uhifadhi endelevu, Waziri Mkuu amesema kumekuwa na mafanikio makubwa katika kusimamia utekelezaji wa zoezi hilo hadi kufikia tarehe 09 Juni 2022, jumla ya kaya 293 zenye watu 1,497 zimejiandikisha. “Serikali imeendelea kuhamasisha na kuandikisha zile kaya ambazo zipo tayari kuhama kwa hiari.” “Upendo huo uliooneshwa na Mheshimiwa Samia, Rais wetu hauna budi kupongezwa na kila mwenye kuitakia mema nchi hii. Hata hivyo, utaratibu huu ni maalum kwa Ngorongoro pekee. Tarehe 30 Juni, 2022 kaya nyingine 25 zenye jumla ya watu 115 zilisafirishwa kwa hiari kuelekea Msomera na kuendelea na maisha yao kama kawaida.”

Wakati huo huo, Waziri Mkuu ameiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii isianze zoezi la upandishwaji hadhi wa maeneo ya mapori tengefu kuwa mapori ya akiba hilo hadi wananchi watoe maoni yao kwa maslahi ya pande zote. “Niwahakikishie wananchi wa maeneo husika kwamba utaratibu wa kupandisha hadhi maeneo ya mapori hayo kuwa mapori ya akiba utasubiri mapitio ya pamoja kati ya Serikali na wananchi. Tathmini hiyo na ushirikishwaji wa wananchi husaidia Serikali kufanya maamuzi ya iwapo kuendelea na utaratibu wa kupandisha hadhi au la Hivyo, Wizara isianze zoezi hilo hadi wananchi watoe maoni yao kwa maslahi ya pande zote.” Amesema rasilimali za wanyamapori ni muhimu kwa maendeleo ya nchi, hususan katika kukuza utalii na hivyo kuongeza pato la Taifa. “Kwa msingi huo, mpango wa Serikali kupandisha hadhi baadhi ya mapori tengefu kuwa mapori ya akiba ni katika kuimarisha ulinzi wa rasilimali zilizopo katika mapori hayo kwa uhifadhi endelevu. Hata hivyo,  Waziri Mkuu amesema utaratibu wa kutangazwa kwa eneo  lolote kuwa Pori la Akiba hufanywa na Mheshimiwa Rais kwa kufuata taratibu zilizowekwa kisheria ikiwemo kufanya tathmini ya kina ya umuhimu wa eneo husika katika uhifadhi na ushirikishwaji wa wananchi kupitia Mamlaka za Serikali za Mitaa za maeneo husika.

Hatua hii ni muhiimu katija kukuza sekta ya utalii nchini Tanzania
Hatua hii ni muhiimu katija kukuza sekta ya utalii nchini Tanzania

Wakati huo huo, Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza Ofisi ya Rais-TAMISEMI ishirikiane na Sekretarieti  za  Mikoa na  Halmashauri zote kufuatilia matumizi na upatikanaji wa taarifa za fedha za Elimumsingi bila ada na zihakikishe wanafunzi hawatozwi  michango kiholela. Vilevile, Mheshimiwa Majaliwa amezitaka taasisi hizo zihakikishe kuanzia sasa maelezo ya kujiunga na shule za umma (Joining Instructions) yanahakikiwa na kupewa idhini na Katibu Tawala wa Mkoa husika kwa kushirikiana na Maafisa Elimu wa maeneo husika. Ameyasema hayo wakati akitoa Hoja ya Kuahirisha Mkutano wa Saba wa Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bungeni jijini Dodoma. Amesema asilimia 10 ya fedha hiyo pia hutumika kugharamia huduma za umeme, maji na ulinzi. “Pamoja na utekelezaji wa mpango huu, waheshimiwa wabunge wamelalamikia kuwepo utitiri wa michango shuleni.

Aidha, Serikali kupitia waraka wa elimu namba tano wa mwaka 2015 na waraka wa elimu namba sita wa mwaka 2015 imetoa maelekezo bayana kuhusu utekelezaji wa Elimumsingi Bila Ada.” Amesema maekezo hayo ni pamoja na matumizi ya fedha za utawala ambazo hutolewa HAZINA na kupelekwa moja kwa moja katika akaunti za shule za msingi na sekondari nchini kwa ajili ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia, ukarabati, uendeshaji wa mitihani  ya   ndani  na utawala. Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kumpongeza Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa maono na dhamira yake kutekeleza kwa vitendo maelekezo ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 kuhusu Serikali kutoa Elimumsingi Bila Ada kwa ngazi ya shule za msingi na sekondari kwa lengo la kuimarisha mazingira ya utoaji wa elimu, mahudhurio na ufaulu.

Uwekaji vigingi ni kwa ajili ya kuimarisha utalii wa Kimataifa.
Uwekaji vigingi ni kwa ajili ya kuimarisha utalii wa Kimataifa.

Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 yanaendelea vizuri na yamefikia asilimia 87, hivyo amewaomba wabunge hususan wanaporejea kwenye maeneo yao ya uwakilishi weendelee kuhamasisha wananchi kushiriki kwenye zoezi hilo muhimu. Vilevile, nitoe wito kwa Watanzania wote kujiandaa kuhesabiwa ikiwa ni pamoja na kutoa ushirikiano wa kutosha kwa makarani wa sensa na viongozi kwenye maeneo wanamoishi. Zoezi hilo limepangwa kufanyika nchini kote Agosti 23, 2022. Waziri Mkuu amesema zoezi hilo lilitanguliwa na Operesheni ya Anwani za Makazi ambayo utekelezaji wake umefikia asilimia 95 na Serikali imefanikiwa kukusanya taarifa na kutoa anwani za makazi zaidi ya milioni 12. Sanjari na mafanikio hayo, Waziri Mkuu amezielekeza taasisi zote zenye dhamana ya masuala ya ardhi na makazi zihakikishe zinakuja na mikakati thabiti ya kutatua migogoro ya matumizi ya ardhi iliyoainishwa wakati wa utekelezaji wa Operesheni Anwani za Makazi. Waziri Mkuu amesema mbali na kuwa na mikakati ya kutatua migogoro ya ardhi, pia taasisi hizo pia zitoe miongozo ya namna bora ya kushughulikia changamoto za Watanzania kuishi katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria ili kuhakikisha wananchi wote wananufaika na fursa zitokanazo na zoezi hilo.

05 July 2022, 15:13