Ukraine bado inaomba silaha ili kuendelea na mapigano
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Tutapigana kwa muda mrefu ikiwa kutakuwa na silaha nzito na silaha za kisasa: kila kitu ambacho tumeomba na tunaendelea kuomba washirika wetu. Hayo yamesema na Rais wa Ukraine Bwana Zelenski katika ujumbe wake wa kawaida kwa njia ya video wa tarehe 10 Juni ikiwa ni siku ya 107 ya vita, ambayo yeye pia anazungumza juu ya mapigano makali huko Donbass na anashutumu Moscow kwa kutaka kuharibu kila jiji. Maneno ambayo yanaambatana na tahadhari iliyozinduliwa saa chache kabla na naibu mkuu wa ujasusi wa Kiev, kulingana na ambayo Ukraine inapoteza katika suala la mizinga na inategemea vifaa vya Magharibi.
Vituo vya afya 295 vilivyoathirika
Wakati huo huo, chini, ya aardhi ya Waukraine wanaashiria kurudi nyuma kwa Warusi kutoka katikati mwa Zaporizhzhia na kudai kwamba hata Melitopol itaachiliwa huru hivi karibuni. Wakati mji wa Severodonetsk sasa uko mikononi mwa Urussi, ambapo takriban raia 1000 wamejificha pamoja na wanajeshi wa Ukraine katika kiwanda cha kemikali cha Azot. Wanajeshi wa Moscow pia wanasonga mbele hadi Donbass ambapo mamlaka inayounga mkono Urussi imewahukumu wapiganaji wawili wa Uingereza wanaoiunga mkono Ukraine. Meya wa Mariupol amezungumza juu ya majengo yaliyobomolewa na Warussi na maiti bado zimo ndani, ambazo huishia kwenye taka na vifusi. Na vita haviachi miundo ya kiraia, wakati huo huo Shirika la Afya Duniani (WHO) limeshutumu mashambulizi 295 dhidi ya vituo vya huduma za afya tangu kuanza kwa vita!