Shambulizi,Nigeria:uchungu unapodharauliwa
Na Sergio Centofanti
Inashangaza kuvinjari katika wavuti kati ya magazeti makuu ulimwenguni na kutoona kati ya habari za kwanza, mbali na isipokuwa chache, mkasa wa mauaji yaliyotekelezwa katika Kanisa Katoliki nchini Nigeria wakati wa Misa ya Pentekoste. Kwa miongo kadhaa tumekuwa tukisoma katika vyombo vya habari vya Kiafrika malalamiko kwamba bara haliko katika umakini wa kimataifa, sio tu katika majanga yake lakini labda pia na zaidi ya yote kwa kile ambacho ni kizuri na chanya katika ardhi hiyo. Si malalamiko ya mwathirika, lakini uchunguzi rahisi wa ukweli: ukosefu wa maslahi ya wengi kwa ubinadamu wa Afrika katika uso wa maslahi mengi, yaliyofichwa na dhahiri, kwa rasilimali zake.
Picha za mauaji hayo ni mbaya sana. Ni fumbo la uovu unaowakumba kwa ukali watu wasio na ulinzi wanaosali siku ya sikukuu na wanaua maisha ya watu wengi, hata wale wanaoendelea kuishi: watoto wengi ni miongoni mwa waathirika. Inashangaza kuona maumivu mengi yaliyopuuzwa. Inashangaza kutojali, ukosefu wa huruma, bila kusimama mbele ya wale wanaoteseka. Wito wa kwanza wa Papa Francisko ulikuwa wa Afrika ya Kati, ambapo awali alifungua Mlango Mtakatifu wa Jubilei ya Huruma. Tunahitaji moyo unaojifungua kwa maskini zaidi, waliotengwa, na waliosahaulika. Safari yake ya kwanza ilikuwa ni kwenda Lampedusa, ili kutoa heshima kwa wahamiaji wengi ambao walikuwa na ndoto ya maisha bora na kufa kwa sababu hawakupata mkono ulionyooshwa wa kuwaokoa.
Kuna vita vingi na migogoro iliyosahaulika, sio barani Afrika tu. Hebu fikiria Siria, Yemen, Afghanistan, Myanmar, Haiti, kwa kutaja nchi chache tu. Kwa kufikiria juu ya mateso haya yaliyosahaulika, tukifikirie juu ya mji huu mdogo wa Owo nchini Nigeria, tukio la mauaji makubwa, unabii wa Isaya unakuja akilini anapothibitisha kwamba siku moja watu wataona haki ya Mungu na kila mji uliopuuzwa, kila mtu aliyesahauliwa na kusahau, ataona waziwazi upendo wa Mwokozi wake.
Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha Bwana. Nawe utakuwa taji ya uzuri katika mkono wa Bwana, na kilemba cha kifalme mkononi mwa Mungu wako. Hutaitwa tena Aliyeachwa, wala nchi yako haitaitwa tena, Ukiwa. Maana kama vile kijana amwoavyo mwanamwali, ndivyo wana wako watakavyokuoa wewe; na kama vile bwana arusi amfurahiavyo bibi arusi, ndivyo Mungu wako atakavyokufurahia wewe. Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana, msiwe na kimya; wala msimwache akae kimya, mpaka atakapoufanya imara Yerusalemu, na kuufanya kuwa sifa duniani. Bwana ameapa kwa mkono wake wa kuume, na kwa mkono wa nguvu zake, Hakika sitawapa adui zako nafaka yako tena kuwa chakula chao; wala wageni hawatakunywa divai yako, uliyoifanyia kazi. Lakini walioivuna, ndio watakaoila, na kumhimidi Bwana; na walioichuma, ndio watakaoinywa, ndani ya nyua za patakatifu pangu. Piteni, piteni, katika malango; Itengenezeni njia ya watu; Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake; Twekeni bendera kwa ajili ya kabila za watu. Tazama, Bwana ametangaza habari mpaka mwisho wa dunia, Mwambieni binti Sayuni, Tazama, wokovu wako unakuja; Tazama, thawabu yake i pamoja naye, Na malipo yake yako mbele zake. Nao watawaita, Watu watakatifu, Waliokombolewa na Bwana; Nawe utaitwa, Aliyetafutwa, Mji usioachwa.(Is 62).