Tafuta

Rais Samia Suluhu Hassani wa Tanzania akishiriki Mktano wa Mwaka huko Accra  Ghana  25 Mei 2022 Rais Samia Suluhu Hassani wa Tanzania akishiriki Mktano wa Mwaka huko Accra Ghana 25 Mei 2022 

Siku ya Afrika 2022:haja ya kusherehekea na kuimarisha mifumo ya kilimo!

Katika Siku ya Afrika 2022,Umoja wa Afrika umechagua kauli mbiu:“Haja ya kusherehekea na kuimarisha mifumo ya kilimo cha chakula,afya na ulinzi wa kijamii”:Umoja wa Mataifa umewataja vijana wa Afrika na wanadiaspora kuwa wahusika wakuu wa maadhimisho hayo,kwamba mustakabali wa Afrika upo mikononi mwao,ili mradi tu wahakikishiwe fursa muhimu za kuwa na mustakabali.

Angella Rwezaula – Vatican.

Ni siku ya  kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika, ulioanzishwa  mnamo tarehe 25 Mei 1963 mjini Addis Ababa  Ethiopia na kuwa Umoja wa Afrika (UA)tangu mwaka 2002 ambayo inakumbushwa viongozi wakuu 30 kati ya 32 wa nchi  zilizokuwa tayari huru zilitia saini ya mkataba huo. Siku ya Afrika ilipoanzishwa, lengo kuu zaidi ilikuwa ni kuweza kuashiria maendeleo ya harakati za ukombozi na kuashiria dhamira ya watu wa Afrika kujikomboa kutoka katika utawala na unyonyaji wa kigeni, kuzuia bara hilo lisigeuka kuwa uwanjawa mzozo kati ya mataifa makubwa ya kimataifa. Leo, hii zaidi sana baada ya uvamizi wa Urusi kwa Ukraine na mgawanyiko kati ya nchi zinazounga mkono upande mmoja au mwingine, ubora ya umoja na ukombozi inaoashiriwa na Siku ya Afrika.

'Kusheherekea na kuimarisha mifumo ya kilimo'

Kwa maana hiyo siku hiyo inachukua umuhimu mkubwa zaidi, hasa katika kazi ya kielimu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na vizazi vipya. Na kwa hiyo ni muhimu kwamba kwa mwaka huu 2022 Umoja wa Afrika umechagua kauli mbiu  ya “haja ya kusherehekea na kuimarisha mifumo ya kilimo cha chakula, afya na ulinzi wa kijamii” ili kuhakikisha usalama wa chakula na maendeleo ya kweli ya mtaji wa watu na kijamii. Bara la Afrika, wakati Umoja wa Mataifa umewataja vijana wa Afrika na wanadiaspora kuwa wahusika wakuu wa maadhimisho hayo, ikumbukwe kwamba mustakabali wa Afrika upo mikononi mwao, ili mradi tu wahakikishiwe fursa muhimu za kuwa na mustakabali. Hata hivyo Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa nchini Italia inashiriki kuadhimisha siku ya “Siku ya Afrika” kila ifikapo tarehe hiyo. Maadhimisho haya yana madhumuni mawili ya kutafakari umuhimu wa ushirikiano kwa pande zote na Afrika na kuimarisha utajiri wa kihistoria, kisanii na kitamaduni katika bara la Afrika.

Siku ya Afrika 2021

Siku ya Afrika kwa mwana 2021 iliongozwea na mada ya utamaduni na sanaa, kupitia uundaji wa maonesho ya mtandaoni. Mchango huo wa video ulibuniwa kama uchunguzi wa ulimwengu wa kisanii wa Kiafrika, ukiingia kwenye mafunzo ya wasanii, ili kujaribu kuelewa maono yao ya sanaa na maisha, kushinda mtazamo wa kitaaluma na wa taasisi  za elimu na  makumbusho. Pamoja na sauti za wasanii, watumiaji walioshiriki katika maonesho ya mtandaoni waliweza kupendezwa kazi zao, shughuli zao ambazo bora kuliko picha nyingine yoyote zinaweza kuelezea nguvu ya utambulisho wa uzalishaji wa tajiri, wa awali na wa uhuru. Tukio hilo, lililofadhiliwa na Kituo cha Kimataifa cha Utafiti cha Uhifadhi na Urejeshaji wa Urithi wa Kiutamaduni (ICCROM), linapatikana kwa uhuru kwenye majukwaa ya kidijitali na mitandao ya kijamii ya MAECI.

Siku ya Afrika 2020

Maadhimisho ya Siku ya Afrika 2020 yalifanyika kwa kuchapishwa kwenye chaneli ya YouTube ya MAECI ya mbio za video zinazojumuisha michango mbalimbali ya miziki ya wasanii wa Kiafrika na Italia, pamoja na hotuba fupi za watu wa kisiasa, zilizolenga kusisitiza umuhimu wa uhusiano wa kihistoria kati Italia na Afrika. Sambamba na mbio za video, onesho la mtandaoni la picha  lilioongozwa na mada ya “Kukutana na Italia-Afrika kwa malengo” liliandaliwa, kumbukumbu kwa ulimwengu huu ulio hai, wa ajabu na uliojaa ukinzani, ulioelezewa kupitia lenzi ya wapiga picha wengine wa Italia ambao wamefanya kazi au kuishi huko katika nchi za Afrika.

Siku ya Afrika 2019

Kwa Siku ya Afrika 2019, Wizara ya Mambo ya Nje iliandaa hafla ya sherehe makao makuu ya Farnesina, kwa ushiriki wa Mabalozi wa Afrika, mamlaka ya Italia, pamoja na wawakilishi wa taasisi, ulimwengu wa biashara, mashirika ya kiraia na sekta ya kitamaduni. Katika hafla hiyo hiyo, waandaaji walibainisa kwamba walitaka kuboresha Maonesho ya Africa ya zamani, moja ya maonesho muhimu zaidi ya sanaa ya Kiafrika yaliyoanzishwa katika nchi ya Italia , iliyozinduliwa kwa hafla ya toleo la pili la Mkutano wa Italia-Afrika 2018 na kuzinduliwa mnamo Aprili 2019 katika  Makumbusho ya kiriai ya Bologna.

25 May 2022, 17:05