Tafuta

Ili kuthibiti maambukizi zaidi ya Uviko ambayo bado yanaendelea,uvaaji wa barakoa aina ya FFP2 inashauriwa katika maeneo yalifungwa. Ili kuthibiti maambukizi zaidi ya Uviko ambayo bado yanaendelea,uvaaji wa barakoa aina ya FFP2 inashauriwa katika maeneo yalifungwa. 

UVIKO-19:CEI imetaarifu ulazima wa kuvaa barakoa katika Kanisa

Matumizi kuvaa barakoa aina ya FFP2 inabakia kuwa lazima katika matukio yote yaliyo wazi kwa umma yanayofanyika ndani ya nyumba:Kanisani,vyumba sawa na sinema,kumbi za tamasha na kumbi za maonyesho.Baraza la Maaskofu CEI wameto mwongozo mpya,kwa kufuatia kanuni zinazoendana na Serikali ya Nchi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Mwenendo wa maambukizi umekuwapo mara kwa mara katika wiki chache na takwimu hizo zinasababisha kuthibitisha maelekezo ya kutoka kwa Rais wa Baraza la  maaskofu iliyokuwa imetolewa mnamo tarehe 25 Machi, akibainisha hata hivyo kwamba matumizi ya barakoa aina ya FFP2 inabakia, kuwa sehemu madhubuti, iliyopendekeza katika shughuli zote zinazohitaji ushiriki wa moja kwa moja wa  watu katika maeneo ya ndani kama vile Kanisani,  sherehe, katekesi, sinema, kumbi za tamasha na kumbi za maonesho.

Maelekezo ya kuendelea kuvaa barakoa FFP2 hadi Juni 15 katika kanisa na maeneo ya ndani

Yote hayo yanasomeka katika Barua iliyotumwa tena na rais wa Baraza la Maaskofu Italia (CEI ) kwa maaskofu wote ikiwa na baadhi ya maelekezo kuhusu matumizi ya barakoa kuanzia Mei Mosi hadi tarehe 15 Juni 2022. Ikumbukwe, pamoja na mambo mengine, kwamba kuanzia Mei Mosi 2022 hakuna ulazima tena wa Green Pass kwa shughuli zilizoandaliwa na Parokia. Vile vile, Green Pass haihitajiki ili kufikia maeneo ya kazi kwa wafanyakazi wanaoshirikiana na watu wa kujitolea.

29 April 2022, 16:08