UN:Dharura ya Tabianchi ni kukomesha kujiangamiza wenyewe
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Yote hayajapotea lakini lazima tuchukue hatua za haraka ifikapo 2030. Ongezeko la joto duniani linaongezeka kwa kasi zaidi kuliko ilivyotarajiwa na Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena umetoa wito wa uingiliaji kati mkubwa na madhubuti ili kupunguza sababu za athari kwenye hali ya tabianchi ya sayari yetu. Umoja wa Mataifa kwa mara nyingine tena unazionya taasisi za kitaifa na kimataifa juu ya uwezekano mkubwa sana wa kuongezeka kwa majanga ya mazingira kutoka mara 5 hadi 14 na matokeo ambayo hayawezi kuzuilika tena. Kukomesha hali hii ya kujiangamiza ndiyo njia pekee ya kutokea. Kwa munubu wa ripoti ya kila mwaka ya Global Energy Monitor, iliyotolewa wiki iliyopita, dunia bado ina mipango ya kujenga au kupanua mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia makaa ya mawe katika nchi 34 tofauti, hasa nchini China.
Miongoni mwa maombi ya dharura yaliyozinduliwa na Umoja wa Mataifa, yale ya kiangazi kilichopita na Aprili 4 mwaka huu, tayari walikuwa wameonya juu ya hatari ya kutoweza kutenguliwa maafa ya tabianchi kutokana na gesi chafuzi. Katika ripoti hizo mbili, Jopo la Umoja wa Kiserikali za Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (IGCC) lilisema ili kupunguza ongezeko la joto duniani, kama inavyofafanuliwa na Makubaliano ya Paris ni muhimu kuchukua hatua sasa au kamwe. Vinginevyo, haitawezekana tena kupunguza ongezeko la joto chini ya nyuzi 1.5°C ikilinganishwa na viwango vya kabla ya viwanda. Hii ina maana kwamba, hata hivyo ni kidogo, muda unaopatikana kwa ajili ya mabadiliko ya kiikolojia bado upo.
Akizungumza katika Mazungumzo ya Raisina huko New Delhi, nchini India, Rais wa Tume ya Ulaya, Bi Ursula von der Leyen, alitaja jukumu muhimu la Ulaya na India katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. “Ni wazi kwamba India na Umoja wa Ulaya ni muhimu katika mpito kuelekea mustakabali endelevu na wa kijani kwa ajili ya sayari yetu. Kwa hivyo ni lazima tuunganishe nguvu katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Hili ni jukumu letu la pamoja katika kuelekea jumuiya ya ulimwengu”, alisisitiza Bi Ursula von der Leyen