Tafuta

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa Kiev nchini Ukraine. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa akiwa Kiev nchini Ukraine. 

Ukraine:Karibu Mkuu Guterres amefanya mazungumzo na Zelenskyy

Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa ametembelea Kiev na kufanya mazungumzo na Rais Zelenskyy.Ametembelea pia miji ya Bucha,Irpin na Borodianka.Kwa mujibu wake amesema uchunguzi wa kina unahitajika na Moscow lazima itoke ushirikiano na Mahakama ya kihalifu kimataifa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katikbu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana António Guterres akiwa katika maeneo ya kivita, ameomba uchunguzi wa kina ufanyike kuhusiana na suala la uhalifu wa vita ili waweza kuwatambu wahusika ,baada ya kutembelea mji wa Bucha nchini Ukraine “Nilipoona eneo hilo la kutisha nimetambia jinsi gani ilivyo muhimu kufanya uchunguz wa kina na uwajibiakaji wa kina” amesema Bwana Guterres kwa waandishi wa habari huko Bucha. Ninaunga mkono kwa dhati Mahakama ya kihalifu ya Kimataifa na ninatoa wito kwa Shirikisho la Urusii ili wakubali kushirikishana na Mahakama ya kihalifu ya kimataifa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametembelea Ukraine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametembelea Ukraine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametembelea Ukraine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametembelea Ukraine

Lakini tunapozungumzia juu ya uhalifu wa vita hatuweza kusahahu ubaya wa uhalifu ni vita vyenyewe”. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, amekuwa huko Kiev na kufanya mazungumzo na Rais wa Ukraine Bwana Volodymyr Zelenskyy na wakuu wengine wa nchi. Katika kutembela mji wa Buryanka, Bwana Guterres alisema: “Ninapoona majengo yaliyoharibiwa, lazima niseme kile ninachohisi. Niliwazia familia yangu katika mojawapo ya nyumba  kama hizo ambazo sasa zimeharibiwa na nyeusi. Ninaona wajukuu zangu wakikimbia kwa hofu, huku sehemu ya familia ikiuawa ... Na tunapoona hali hizi, mioyo yetu, bila shaka, iko upande wa waathirika”. Akiwasili mjini Kiev, Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alitembelea miji ya Bucha, Irpin na Borodianka, maeneo unyanyasaji unaoshutumiwa na Waukraine kutokana na kuvamiwa na jeshi la Urussi.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametembelea Ukraine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametembelea Ukraine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametembelea Ukraine
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametembelea Ukraine
29 April 2022, 15:42