Taa juu ya kaburi la pamoja huko Bucha nchini Ukraine. Taa juu ya kaburi la pamoja huko Bucha nchini Ukraine. 

Rais wa Marekani alitangaza kutuma zaidi ya dola milioni 700 kwa wanajeshi Ukraine

Rais wa Marekani alitangaza kutuma zaidi ya dola milioni 700 za msaada wa kijeshi nchini Ukraine.Putin kashinda Donbass,lakini anashutumiwa kwa matumizi ya silaha za kemikali zinazosadikika kuonekana huko Mariupol.Zelensky anapendekeza kubadilishana kwa wafungwa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

‘Mazungumzo yalikwama, katika vizingiti kipofu, kutokana na Ukraine’. Hivi ndivyo  Vladimir Putin rais wa Urussi, amesema  kuzuia mazungumzo  huku akishambulia Kiev.  Kwa  maana hiyo vita vitaendelea, alitangaza, kwa ushindi wa Donbass nzima ili kulinda idadi ya watu wanaozungumza Kirussi. Wakati huo huo, mji wa Mariupol umetoa hesabu ya awali ya watu waliokufa tangu mwisho wa Februari.  Wanazungumzia karibu watu elfu ishiriki kulingana na ripoti za vyombo vya habari katika masaa 24 yaliyopita,  na pia kuhusiana na silaha za kemikali zinazotumiwa na vikosi vya Urussi. Hiyo lakini ni habari inayotia wasiwasi kutoka Shirika la Kupiga Marufuku Silaha za Kemikali, (OPAC) ambayo ukweli wake, hata hivyo, bado haujawezekana kuthibitishwa kabisa.

Wanajeshi wa Ukraine wakiwa Donbass
Wanajeshi wa Ukraine wakiwa Donbass

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky mwenyewe amekiri kutowezekana, kwa sasa, kwa uchunguzi kamili kuhusu kutumia aina hiyo ya kemikali  katika jiji hilo. Wakati huo huo, idadi ya watoto waliouawa tangu kuanza kwa uvamizi wa Urussi imeongezeka hadi 190, wakati karibu watoto 350 wamejeruhiwa. Huko Bucha na vitongoji vingine vya mji mkuu unaokaliwa na Warussi, kulingana na wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine, imefikia zaidi ya 700 waliokufa na karibu 200 hawajulikani walipo.

Rais Zelensky wakati wa kutoa ujumbe wake
Rais Zelensky wakati wa kutoa ujumbe wake

Rais wa Marekani Bwana Joe Biden, kwa mara ya kwanza, anamshutumu rais Putin kwa mauaji ya halaiki, ufafanuzi ambao haushirikishwi na wale ambao, kama Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, wanaamini kwamba kuongezeka kwa maneno hakuwezi kusaidia sababu. Wakati huo huo Waukraine walitangaza kuzuiwa kwa mikondo ya kibinadamu inayopeleka msaada, kutokana na hatari ya hali hiyo, wakiwashutumu Warussi kwa kukiuka makubaliano ya kuwatoa raia nje ya maeneo yenye migogoro.

Mji wa Mariupol umeharibiwa kwa mabomu na makombora ya kirussi
Mji wa Mariupol umeharibiwa kwa mabomu na makombora ya kirussi

Kiev pia imetoa mapendekezo kadhaa kwa Urussi, kama vile mabadilishano kati mfungwa oligarch wa Urusi Medvedchuk, anayefikiriwa kuwa karibu na rais wa Urussi, na Waukraine waliokamatwa na vikosi vya Urussi. Medvedchuk, naibu na kiongozi wa upinzani unaounga mkono Urussi, na kuchukuliwa kuwa msaliti namna moja wa Kiev, kwa sababu alikamatwa katika operesheni ya ucunguzi huko  Ukraine. Wakati huo huo, habari zinafika kutoka Marekani kwamba utawala wa Biden utatangaza msaada mwingine wa kijeshi wa dola milioni 750 utakaopatikana hivi karibuni kwa ajili ya Ukraine.

13 April 2022, 15:21