Ufaransa:Rais Macron achaguliwa tena kwa awamu ya pili
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Nchini Ufaransa ina mshangilia Rais Emmanuel Macron kwa ushindi wa awamu nyingine tena ya pili baada ya kushinda kwa duru ya pili ya uchaguzi Dominika tarehe 24 Aprili 2022 dhidi ya mpinzani wake Bi Marine Le Pen. Macron ndiye rais wa kwanza wa Ufaransa katika miongo miwili kushinda muhula wa pili, lakini ushindi wake ulikuwa na mpinzani wake wa siasa kali za mrengo wa kulia ambao wachambuzi wanasema hata hivyo haukuwa na nguvu zaidi kama ule wa mwaka 2017 kati yao kulinganisha na asilimia 66.1 dhidi ya asilimia 33.9, katika mwaka wa 2002, na Bwana Jacque Chirac alipochaguliwa kwa muhula wa pili.
Kwenye hotuba yake Bi. Le Pen mwenye umri wa miaka 53 alikiri kushindwa kwake lakini akasema kwamba matokeo hayo ni ushindi kwao na sasa ni wakati wa kuangazia uchaguzi wa bunge mwezi Juni. Hata hiyo kwa wachambiz pia wamesema kwamba ushindi wa Bwana Macron ulitoa uafadhali mkubwa kwa Bara la Ulya mara baada ya kuwa na hofu kuwa urais Le Pen ungeliacha bara hilo katika hali mbaya kufuatia suala la Brexit na kuondoka kutoka ulingo wa kisiasa wa Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel.
Waziri Mkuu wa Italia Bwana Mario Draghi katika kumpongeza kuhusu ushindi wa Macron ameuita kuwa ni habari njema kwa wote barani Ulaya wakati Kansela wa Ujerumani Bwana Olaf Scholz amesema wapiga kura wa Ufaransa wamepiga kura muhimu ya kuwa na Imani barani Ulaya. Naye Rais wa Baraza la Ulaya Bwana Charles Michel amesema umoja huo sasa unaweza kuitegemea Ufaransa kwa miaka mitano zaidi wakati rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Bi rsula von der Leyen pia amempongeza Bwana Macron kwamba anafuraha kuendeleza ushirikiano wao bora zaidi.
Na huko Marekani imesema Ufaransa ni mshirika wa jadi na muhimu katika kushughulikia changamoto za ulimwengu. Rais Joe Biden amesema watashirikiana kwa karibu ikiwemo kuisaidia Ukraine, kutetea demokrasia, na kupambana na mabadiliko ya tabia nchi. Kwa kipindi hiki kigumu barani Ulaya kwa hakika viongozi wengi wamefurahishwa na ushindi wa Bwana Macron!