Tafuta

Askofu Mkuu Adalberto Martínez Flores,wa Jimbo Kuu Katoliki la Asunción na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Paraguay (CEP). Askofu Mkuu Adalberto Martínez Flores,wa Jimbo Kuu Katoliki la Asunción na Rais wa Baraza la Maaskofu nchini Paraguay (CEP). 

Paraguay:Waandishi,waamini na wasioamini dumisheni wito wa huduma ya ukweli

Askofu Mkuu amekumbusha kuwa kwa ajili ya Kanisa,taaluma adhimu ya mwandishi wa habari ina maana ya umisionari na utume kwa mujibu wa mafundisho ya Mwalimu asemaye:“Ukweli utakufanya kuwa huru (Yh 8,32).Amesema hayo katika muktadha ya kuadhimisha Siku ya Mawasiliano nchini Paraguay iliyofanyika mnamo Aprili 26.Kutoa habari ni kuunda,ni kuhusuka katika maisha ya watuhivyo ni liw na uhakika wa vyanzo.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Sughuli za mwandishi wa habari ni zile za kutafuta na kuwasilisha ukweli, iwe kwa matendo na habari zenyewekwa njia ya ripoti za uchunguzi, za kutafsiri matukio, na zile za mlolongo wa maoni na zaidi utafutaji na mwasiliano ya kweli yanaoongoza kazi yake.  Ameandika hivyo Askfofu Mkuu  Adalberto Martinez Flores, wa  Jimbo Kuu Katoliki la Asunción, katika Ujumbe wake kwa siku ya Waandishi wa Habari ambapo nchini Paraguay wameadhimisha tarehe 26 Aprili 2022. Katika maadishi yake yaliyochapishwa na Shirika la Habari za kisionari Fides, Askofu Mkuu Flores  amekumbusha  katika  suala la  Kanisa, taaluma adhimu ya mwandishi wa habari ina maana ya umisionari na utume kwa mujibu wa mafundisho ya Mwalimu asemaye :“ U kweli utakufanya kuwa huru(Yh 8,32). Katika shughuli yake ya kutoa habari mwandishi anao ukweli na utume wake ili kukumbusha kuwa kiini cha habari si kwa sababy ya uharaka wa kuitoa, na muktahda wa maoni ya umma,  badala yake ni watu.

Kutoa habari ni kuunda na kuhusika katika maisha ya watu

Kwa kutoa habari ni kuunda, ni kuhusika katika maisha ya watu, amesisitiza Askofu Mkuu Flores, na kwamba kuhakiki vyanzo na kulinda mawasiliano yanakuwa kweli na mchakato mzima wa maendeleo ya wema ambao unazaa imani na njia zilizo wazi za muungano na  wa amani. Uhuru wa kujieleza na unaohusu kuchapisha ni mantiki mbili msingi kwa kazi hiyo ya kitaaluma  katika. Utafutaji wa ukweli unahusu uhuru wa kujieleza kwa mwandishi ambao inajikita katika zoezi kwenye muktadha wa kiadili na uwajibikaji kijamii, na naohusu kuchapisha kama msaada na injini ya mawasiliano, upelelezi na kutafsiri matukio yanayohusiana na jamii yenyewe.

Waandishi,waamini na wasioamini dumisheni wito wa huduma ya ukweli

Askofu Mkuu Flores  wa Parugay akiendelea  kuwatia moyo na pongezi waandishi wa habari kwa kazi yao wanayojikita nayo katika huduma ya wazalendo,  amewashauri waandishi wa habari, waamini na wasio waamini, kuendelea kuongeza nguvu katika wito wao wa huduma ya ukweli licha ya wote kupata vizingiti na vikwazo wanavyokutana navyo katika kutimiza kazi yao ya kila siku na ambayo wakati mwingine haitambuliwi, haihesabiwi,na kuthamanishwa katika haki na ukuu wake. Kwa kumtaja Papa Francisko ambaye daima anawasihii waandishi wa habari kwa namna ya pekee kuwa na umakini wa ukweli, wa wema na uzuri, Askofu Mkuu  Adalberto Martinez Flores amesisitiza juu ya changamoto ya pamoja ambayo inawaunganisha katika Kanisa, kwa kuwaalika wasaidiane kwa ajili ya kuhabarisha matumaini na maisha ya watu wao.

29 April 2022, 14:17