Tafuta

Rai wametolewa huko Volnovakha na kufika kijiji cha Bugas. Rai wametolewa huko Volnovakha na kufika kijiji cha Bugas. 

Ukraine:Watu wasio na hatia wakiwemo wanawake na watoto wanauawa

Mashambulizi kutoka Urusi yalianza tarehe tangu tarehe 24 Februari 2022 na watu wakalazimika kuondoka na wengine wanaendelea kutoka kwenye makazi yao,wengine walikuwa wamebaki wakifikiri mambo yanaisha lakini siku hadi siku mambo yamekuwa magumu wameanza kutolewa kutoka katika majimbo yao na mikoa yenye hatari kukimbilia maeneo ya nchi mbali na nchi jirani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika wiki mbili  tangu Urusi ianzishe mashambulizi yake nchini Ukraine, imesababisha kusambaratisha familia nyingi sana wakiwemo wanaume ambao wanalaizima kubaki Ukraine ili kupigana vita au kusaidia kwa namna moja au nyingie huku familia zao zikilazimika kukimbilia maeneo mengine ya tafia hilo au nje ya Ukraine kwa mfano nchini Poland ni karibu milioni mbili ya wakimbizi. Hali hiyo imeleta upweke kwa familia hususan ambazo wanaume wanapaswa kubaki Ukraine ili kushiriki katika mapigano ya kukomboa nchi yao. Mashambulizi kutoka Urusi yalianza tarehe 24 Februari 2022 na watu wakalazimika kuondoka kwenye makazi yao wengine walibaki wakifikiri mambo yanaisha.

Wakimbizi wengi wamekimbilia nchi za jirani barani Ulaya

Siku hadi siku, watu wengi walianza kuondoka kutoka katika majimbo kama vile ya  Donetsk wakikimbilia katika  jimbo la Zakarppatia lililoko Magharibi mwa Ukraine na majimbo mengine mengi ya mipakani na wengine kwenda Poland, Hungeria, Moldavia, Romania na kwingineko barani Ulaya. Hali bado ni ngumu na wengine wanezidi kuondolea katika maeneo, lakini maeneo mengine yamekwisha kuwa chini ya usimamizi wa wanajeshi wa Urusi. Wanaume wanaruhusiwa kusindikiza familia zao, na ikiwa familia ni zaidi ya watoto wane, mme anaruhusiwa ili akae na familia yake lakini wengine wanaamua mara baada ya kuwafikisha salama wanarudi kupambana. Serikali inataka wanaume wenye umri wa kati ya miaka 18 hadi 60 wabakie Ukraine waingie jeshini kupambana kukomboa nchi au wasadie kw vyovyot vile.

Watu waliotolewa Mariupol hadi Bezymennoye nchini Ukraine wakiwemo watoto
Watu waliotolewa Mariupol hadi Bezymennoye nchini Ukraine wakiwemo watoto

Shirika la Wakimbizi UNHCR inaendelea kuimarisha misaada Ukraine

Pamoja na mashambulizi yanayoendelea nchini Ukraine kutoka Urusi, Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la kuhudumia wakimbizi, UNHCR linashirikiana na mamlaka za mji huu kupanua huduma za kupokea wakimbizi, sambamba na kubainisha majengo ya kukarabatiwa ili yatumike kama malazi kwa wakimbizi wa ndani. Kwa kushirikiana pia na shirika la kiraia la NEEKA, UNHCR inapatia kituo hiki nguo za joto, maji, chakula, na vifaa vinavyohitajika zaidi vya jikoni kama vile majokofu na majiko ya kupashia vyakula. Pamoja na mashirika haya ya kiraia lakini yapo mengine ya kidini ambayo ni mengi mno yanasidia kupokea wakimbizi.

Kadiri muda unavyosonga mbele hali inakuwa ngumu

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana  Antonio Guterres kwa mara nyingine tena amezungumza na waandishi wa habari jijini New York, Marekani tarehe 14 Machi 2022  na kusema Ukraine inazidi kuteketea mbele ya macho ya dunia na madhara ya vita kwa wanancih  hayana kipimo. “Watu wasio na hatia wakiwemo wanawake na watoto wanauawa. Baada ya kushambuliwa na majeshi ya Urusi, barabara, viwanja vya ndege na shule vimesalia magofu”. Katibu Mkuu amesema kadri muda unavyosonga mbele mambo mawili yako dhahiri; Mosi; hali inazidi kuwa mbaya na pili, chochote kile kitakachotokea, vita hii haitakuwa na mshindi bali kila mtu atakuwa ameshindwa. Umoja wa Mataifa na wadau wake wanafanya kazi kuhakikisha kuna njia salama ya kupita ili kufikisha misaada kwenye maeneo yaliyozingirwa na kwamba “hadi zaidi sasa zaidi ya watu 600,000 wamepatiwa aina mbalimbali za misaada.” Ni kwa kutambua ongezeko la mahitaji, Katibu Mkuu ametangaza kuwa Umoja wa Mataifa kupitia mfuko wake wa usaidizi wa dharura, CERF umetoa dola milioni 40 zaidi ili kuongezea misaada ya  haraka kwa wahitaji. Misaada kama vile maji, chakula, dawa pamoja na fedha taslimu zitapatiwa wahitaji. Ingawa ametaka pande zote ziheshimu sheria za kimataifa za kibinadamu ili misaada hiyo ifikiwe walengwa.

Wanawake na wazee wanasidiwa na wanajeshi
Wanawake na wazee wanasidiwa na wanajeshi

Kwa wauaji na waharifu vita sio janga bali ni fursa

Bwana Guterres ametaka kila hatua zichukuliwe ili kunusuru makundi yaliyo hatarini kama vile wanawake na watoto kutumbukia kwenye midomo ya wauaji na wasafirishaji  haramu akisema, “kwa wauaji na wasafirishaji haramu vita si janga bali ni fursa. Nitaendelea kupazia sauti adha wanayopata wananchi wa Ukraine kama ninavyofanya tena leo hii.”Aidha Katibu Mkuu amebainisha kuwa madhara ya vita nchini Ukraine yanavuka mipaka na waathirika wakuu ni nchi maskini pamoja na zile zinazotegemea bidhaa kutoka Ukraine na Urusi. “Tegemeo la chanzo cha chakula limepigwa bomu. Urusi na Ukraine zinachangia zaidi ya nusu ya mafuta ya alizeti na takribani asilimia 30 ya unga wa ngano unaotumika duniani kote,".

Utegemezi wa mazao ya nafaka

Ukraine peke yake inatoa zaidi ya nusu ya unga wa ngano unaosambazwa na shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP. Bei za chakula, mafuta na mbolea zinaongezeka kwa kasi kubwa. Minyororo ya usambazaji wa bidhaa imevurugwa na gharama za usafirishaji na kuchelewesha bidhaa zinazoagizwa kutoka nje pindi zinapopatikana nazo zimefikia kiwango cha juu kuwahi kufikiwa. Ngano inayotegemewa kutoka Ukraine na Urusi sasa hatarini. Nchi 45 za Afrika na nyingine zinazoendelea huagiza theluthi moja ya ngano kutoka Ukraine au Urusi, na 18 kati ya hizo zinaagiza takribani asilimia 50. Nchi hizo ni pamoja na Burkina Faso, Misri, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Lebanon, Libya, Sudan na Yemen. “Lazima tuchukue hatua zozote zinazowezekana kuepusha kimbunga cha njaa na kusambaratika kwa mfumo wa chakula duniani,” amesisitiza Katibu Mkuu.

Viongozi duniani acha kupeleka fedha katika bajeti ya silaha

Bwana Guterres kwa maana hiyo ametoa mwaliko kwa viongozi wa duniani kujizuia kupeleka fedha zaidi katika bajeti za silaha na badala yake zielekeze kwenye misaada rasmi ya maendeleo na hatua kwa tabianchi wakati huu ambapo mataifa maskini yanahaha kupata fedha kujikwamua kutoka madhara ya janga la ugonjwa wa Corona au UVIKO-19. Janga hili amesema lazima likome na katu “hatujachelewa kutumia diplomasia na mazungumzo. Tunahitaji amani, amani kwa ajili ya wanachi wa Ukraine.

15 March 2022, 13:49