Tamasha la Muziki wa Kikristo,Sanremo:Namna ya kueneza upendo
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Masafa kuelekea mkoa wa bahari na yale ya Radio Vatican, yanaendelea kutoa sauti katika tamasha zuri la Muziki wa Kikristo huko Sanremo 2022, lililofunguliwa siku ya Alhamisi tarehe 3 Februari 2022. Hili ni tamasha jipya la Kikristo kufanyika karibu lile la kihistoria la72 la kwenye ukumbi wa Ariston katika mashindano ya wanamuziki kijamii nchini Italia. Toleo la Muziki wa Kikristo lilifunguliwa katika uwanja wa Mtakatifu Clotilde kwenye huduma ya Padre Orione ambapo kwa siku tatu litawaona washiriki wa mashindano ya muziki 24. Awali ya yote lilifunguliwa na Misa iliyoadhimisha na Padre Michele Madonna na Baraka ikatolewa na Askofu Antonio Suetta, wa Jimbo Katoliki la Ventimiglia –Sanremo, Italia. Mkurugenzi wa tamasaha hilo la Sanaa na mtunzi, na mwimbaji Fabrizio Venturi katika kufafanua tukio hili na Vatican News amebainisha umuhimu wa mazungumzo kati ya aina za muzika na kwamba muziki hauna mipaka.
Katika ufafanuzi wake Bwana Veturi amesema mpango huo ni wenye hisia ya kuvutia sana na ni mpango wa Mungu. “Kuzungumza na Bwana wetu kwa njia ambazo zina nguvu ya Mungu. Muziki unapaswa kusaidia kuzungumza kama ilivyo mji wa Sanreamo na kila mahali kwa sababu muziki wa kikristo kila anayeimba anasali mara mbili. Na muziki hausimami kwa sababu ni kama hewa. Ujumbe unooongoza mtindo huo katika ufunguo wa muzikia unabaki daima”. Tangu zamani, amesisiza kuwa inatosha kutazama nyuma ya wakati, kwa sababu muziki umekuwa daima kielelezo cha kizamani cha ulimwengu.
Kati ya wasanii 24 ambao wanatafuta ushindi, yupo mmoja wapo ambaye ni wa kipekee kwa sababu amesema kwamba alimkasirisha Mungu, kwa mujibu wa maelezo yake ili amfikie. Yeye aAlitaka, anataka, na alifanya mambo yasiyosemeka, lakini baadaye Bwana akasikia kilio chake. Mtu huyo bila kutajwa jina amesema alikuwa mlevi wa madawa ya kulevya, sasa ni mtu mzuri, na anatunga maneno mazuri. Anaufanya wimbo wake kwa namna anayopendelea, yaani muziki wa rap.
Bwana Venturi akielezea kwa maoni yake kuhusu lengo la tamasha hilo amesema ni sehemu ya kuanzia na mahali pa kufikia. Wanatazamia kuona mazuri miaka michache ijayo, lakini tayari wameweza kuweka muziki wa Kikristo katikati. Nyimbo zimeandikwa kwa kutazama wanamichezo, wanyama na wapokeaji ni maelefu na hivyo ni wazi kwamba Mungu ndiye kitovu. Vile vile amesisitiza kuwa lengo ni kufanya mazungumzo ya muziki wa Kikristo na aina nyingine kwa sababu Muziki ni muziki, hauna mipaka. Muhimu ni kuwa na lugha ambayo inafaa kumaanisha, na kuwasilisha ujumbe halisi. Kwake yeye hakuna wimbo mzuri au mbaya lakini kuna uliofanywa vizuri na ambao hauwezi kukataliwa kwa maana nyimbo zote ni sifa kwa Mungu.
Muziki wa kikristo ni sifa kwa Bwana, na katika kipindi hiki cha janga upendo wa Mungu umewekwa kwa kila mtu. Sasa zaidi ya hapo awali ni muhimu kuelewa kwamba kuna kamba ambayo inatoka mbinguni na inaweza kuegemewa na kila mtu, kwa maana ni Mkono wa Mungu. Tamasha hilo limezaliwa katika jiji la muziki, Sanremo na ndiyo mji mkuu wa muziki! Kuishi toleo la kwanza hapo, katika mbio hizo ni bora za kupokezana na kijiti cha Ariston! Na ndicho kitu kizuri zaidi kinachoweza kuwepo, amesisitiza Bwana Venturi.