Ikiwa tunafanya vita,sisi sio wakristo!
Na Angella Rwezaul,- Vatican.
Labda tutakuwa weu sana kufanya vita. Vita katika Ulaya ni matokeo yasiyofikiriwa. Lakini angalau tusisema kuwa sisi ni wakristo. Ndivyo anaandika Dk. Sergio Centofanti, Makamu Mhariri wa Baraza la Kipapa la Mawasiliano katika maoni yake kuhusu Tafakari ya Papa Francisko ya Dominika tarehe 20 Februari, lakini kwa kuiweka katika nuru la suala la vita vya ulimwengu na hasa sula la Ukraine na Urusi ambavyo vinaendelea kuzua mjadala mkubwa.
Tupo tunacheza na moto, Dk. Centofanti anaandika na kwamba, labda haitutoshi vita visivyooneka: vile vya ulimwengu ambavyo kila mwaka vinasababaisha milioni ya vifo kwa sababu ya njaa na umasikini, kwa sababu ya magonjwa yasiyozuilika, kwa sababu ya vurugu nyingi za migogoro iliyosahaulika, kwa sababu ya uhalifu wa siku zote, kwa sababu ya ajali kazini au kwa sababu ya vita vile vilivyofichika ambavyo vinaitwa upweke, kutengwa, unyonyaji na kutokujali.
Kuna vita baadaye ambavyo hatuna dhamiri zaidi ya kutosha, vile dhidi ya watoto waliotolewa mimba tumboni mwa mama zao. Labda ni vita visivyoonekana zaidi. Ni nani anajua kama siku moja vizazi vitatuhukumu kwa mauaji haya ya kimya kimya. Wale ambao hawaoni vita hivi vikuu huchukulia amani yao kidogo kuwa ya kawaida. Hatujihukumu kurudia makosa ya zamani, amebainisha Dk Centofanti.
Dk. Centofanti akiendelea na maoni yake juu ya vita hivi ameandika kuwa: “Labda janga ambalo tayari limeshtua ubinadamu wote, kuua bila ubaguzi na kuwafanya watu masikini zaidi na kuwatajirisha matajiri zaidi, haitoshi kwetu. Na leo hii vitisho vya vita pekee vinaongeza umaskini wa wengi na utajiri kwa wachache. Hasira na chuki zinazozunguka ulimwengu zinatia wasiwasi: fitna za vurugu, maneno ya dharau, milipuko ya ukatili. Makosa na matusi kati ya Wakristo wenyewe yanatia wasiwasi".
Yesu alisema watatutambua kwa upendo tutakaokuwa nao sisi kwa sisi. Badala yake, inatosha kuangalia tu kwenye mitandao ya kijamii na blogu: mara nyingi tunashuhudia migongano na uchokozi wa pande zote mbili, labda kwa jina la ukweli na haki. Mtakatifu Paulo anawaambia Wagalatia: “Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana” ( Gal 5:15 ). Lakini je ikiwa tunapigana vita sisi kwa sisi wanaoamini Injili, tunawezaje kuwaomba wengine wasifanye? Kwa kuhitimisha, Dk. Centofanti anaandika: “Injili inatutaka tuwapende adui zetu, tushinde ubaya kwa wema. Inaonekana kama kitu cha kuwazika tu. Labda tutakuwa wazimu vya kutosha kwenda vitani. Lakini angalau tusijiite Wakristo”.