Tafuta

Rita Levi Montalcini mwana sayansi maarufu nchini Italia Rita Levi Montalcini mwana sayansi maarufu nchini Italia 

Siku ya Kimataifa ya Wanawake na wasichana katika fani ya sayansi

“Ulimwengu unaweza na ni lazima kuchukua hatua kwa kuwa na sera zinazojaza madarasa na wasichana wanaosoma teknolojia,fizikia,uhandisi,hesabu,pamoja na hatua zinazolenga kuhakikisha fursa za wanawake kukua na kuongoza katika maabara,taasisi za utafiti na vyuo vikuu”.Ni ushauri wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa katika fursa ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake na wasichana katika fani ya Sayansi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya viwango vya chini vya wanawake wanaofanya kazi katika masuala ya Akili Bandia (AI), na kanuni za hovyo za upendeleo wa kijinsia ambazo huchukulia wanaume kama watu wa viwango na wanawake kama tu ilimradi. Bwana Guterres amesema hayo kupitia katika ujumbe wake wa siku ya kimataifa ya wanawake na wasichana katika  fani ya Sayansi, ifanyikayo kila tarehe 11 Februari na kwamba hivi sasa ni mtu mmmoja tu kati ya watafiti watatu wa sayansi na uhandisi ulimwenguni ambaye ni mwanamke na kwamba vikwazo vya kimuundo na kijamii vinazuia wanawake na wasichana kuingia na kuendelea katika fani ya sayansi.  Bwana Guterres ameeleza kwamba janga la UVIKO-19 limeongeza zaidi ukosefu wa usawa wa kijinsia, kuanzia kwenye kufungwa kwa shule hadi kuongezeka kwa vurugu na mzigo mkubwa wa huduma nyumbani.  “Ukosefu huu wa usawa unanyima ulimwengu wetu vipaji na ubunifu mkubwa ambao haujatumiwa. Tunahitaji mitazamo ya wanawake ili kuhakikisha sayansi na teknolojia inafanya kazi kwa kila mtu”, alisema Bwana Guterres.

Bwana Guterres aidha katika hili alishauri hatua ambazo anaona ni muhimu kuzichukua na kwamba: "Ulimwengu unaweza na ni lazima kuchukua hatua kwa kuwa na sera zinazojaza madarasa na wasichana wanaosoma teknolojia, fizikia, uhandisi, hesabu. Pamoja na hatua zinazolenga kuhakikisha fursa za wanawake kukua na kuongoza katika maabara, taasisi za utafiti na vyuo vikuu. Kwa dhamira ya kukomesha ubaguzi na mila potofu kuhusu wanawake katika sayansi. Na kwa juhudi kali zaidi za kupanua fursa kwa wanawake wa jamii za watu wachache".  Bwana Guterres amethibitisha kwamba:"Haya yote ni muhimu katika uwanja muhimu wa akili bandia".  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliendelea kusisitiza kuwa dunia inahitaji wanawake zaidi wanaokuza akili bandia ambayo inamuhudumia kila mtu na kufanya kazi kwa usawa wa kijinsia na kwamba inahitaji pia kubadilisha mienendo ambayo inawazuia wanasayansi wanawake vijana kusoma taaluma ambazo hutusaidia kushughulikia majanga ya tabianchi na mazingira. Kwa kutoa mfano binafsi alisema: “Nilifundisha uhandisi. Ninajua kutokana na uzoefu binafsi kwamba wasichana na wanaume wana uwezo sawa na wanavutiwa sawa na sayansi, iliyojaa mawazo na wako tayari kuendeleza ulimwengu wetu mbele.” Bwana Guterres vile vile  amesema:"ni lazima tuhakikishe kwamba wanapata fursa sawa za kujifunza na kufanya kazi kwenye uwanja sawa" na kusisitiza kuwa: “katika Siku hii ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika fani ya Sayansi, ninatoa wito kwa kila mtu kuunda mazingira ambapo wanawake wanaweza kutambua uwezo wao wa kweli na wasichana wa leo wanakuwa wanasayansi na wavumbuzi wakuu wa kesho, wakiunda mustakabali mzuri na endelevu kwa wote.”

Hata hivyo kwa kujikita kwa kina juu ya fani ya Sayansi kwa wanawake, kwa hakika wamechangia kwa kiasi kikubwa maendeleo yake tangu nyakati za kale (kwa mambo ya kale unaweza kutazama pia kuingia kwa wanawake katika falsafa). Wanahistoria wanaopenda uhusiano kati ya jinsia na sayansi wameweza kupanua mtazamo wao juu ya juhudi za kisayansi zinazofanywa na wanawake na mafanikio yao, juu ya vikwazo ambavyo wamelazimika kukumbana navyo na kuvishinda, na juu ya mikakati iliyotekelezwa ya kuwafanya wachunguzwe na kukubaliwa (Taz.mapitio ya rika)kazi zao katika majarida ya kisayansi na machapisho mengine. Utafiti wa kihistoria, muhimu na wa kijamii wa masuala haya umekuwa taaluma ya kitaaluma yenyewe. Ushiriki wa wanawake katika uwanja wa dawa ulifanyika katika ustaarabu mwingi wa kale, wakati utafiti wa falsafa ya asili katika Ugiriki ya kale ulikuwa wazi kwa wanawake; pia walichangia (protoscience ya alchemy) katika mchakato wa karne ya I - II. Katika Zama zote za Kati, monasteri za Kikristo ziliwakilisha kituo au  sehemu muhimu zaidi cha elimu na cha kukusanya na kuhifadhi hekima ya kale; baadhi ya jumuiya hizi pia zimeweza kuruhusu wanawake kuchangia katika utafiti wa kisayansi.

Ingawa karne ya XI iliona kuzaliwa na maendeleo ya vyuo vikuu vya kwanza, katika Enzi za Kati, wanawake katika sehemu kubwa hata hivyo walitengwa na aina yoyote ya elimu ya umma. Mtazamo wa kuwaelimisha wanawake katika nyanja ya kitiba katika Peninsula ya Italia inaonekana kuwa huria zaidi kuliko katika maeneo mengine. Na mwanamke wa kwanza anayejulikana kupata nafasi ya chuo kikuu katika uwanja wa masomo ya kisayansi alikuwa mwanasayansi wa Kiitaliano Laura Bassi mnamo 1732 katika Chuo Kikuu cha Bologna. Ingawa jukumu la jinsia lilibakia kwa kiasi kikubwa kufafanuliwa wakati wa karne ya 18, wanawake walipata maendeleo makubwa katika sayansi. Wakati sehemu kubwa ya  karne ya kumi na XIX walisalia kutengwa na mafunzo rasmi zaidi ya kisayansi, lakini hata hivyo walianza kupokelewa kwa jamii za wasomi na wasomi hasa katika kipindi hiki. Mwishoni mwa karne ya XIX,  kuongezeka kwa vyuo vilivyoanzishwa kuhusiana na ili kukuza elimu ya wanawake kulitoa kazi kwa wanasayansi wa kike na fursa kuu za kwanza za elimu rasmi. Marie Curie, mwanamke wa kwanza kupokea Tuzo ya Nobel mwaka wa 1903 (kwa ajili ya fizikia), aliweza kupata nyingine mwaka wa 1911 (kwa kemia), kwa ajili ya masomo yake juu ya radioactivity.

Watambue Wanawake arobaini waliopata Tuzo ya Nobel kati ya 1901 na 2010; miongoni mwao, 17  ni  katika nyanja za kimwili, kemikali na kisaikolojia-matibabu: Dorothy Hodgkin (1910-1994), Grace Hopper (1906-1992), Maryam Mirzakhani (1977-2017), Maria Goeppert Mayer (1906-1972) – Sally Ride (1951-2012), Rosalind Franklin (1920-1958), Jennifer Doudna (1964), Rachel Carson (1907-1964), Marie Curie (1867-1934), Gerty Cori (1896-1957), Jane Cooke Wright (1919-2013), Vera Rubin (1928-2016), Sunetra Gupta (1965), Gertrude Belle Elion (1918-1999), Nina Tandon (1980), May-Britt Moser (1963), Inge Lehmann (1888-1993), Cynthia Kenyon (1954), Maria Sibylla Merian (1647-1717), Marica Branchesi (1977), Valentina Tereškova (1937), Helen Taussig (1898-1986), Nancy A. Moran (1954), Lydia Villa-Komaroff (1947), Emmy Noether (1882-1935), Elisabeth S. Vrba (1942), Chien-Shiung Wu (1912-1997), Elena Lucrezia Cornaro (1646-1684), Rosalyn Yalow (1921-2011), Lynn Margulis (1938-2011), Wangari Maathai (1940-2011), Esther Lederberg (1922-2006), Trotula de Ruggiero (? - 1097), Mary Leakey (1913-1996), Nicole King (1970), Mary-Claire King (1946), Doris F. Jonas (1916-2002), Caroline Herschel (1750-1848), Annie Easley (1933-2011), Ruth Benerito (1916-2013), Patricia Era Bath (1942), Francoise Barre-Sinoussi (1947), Rita Levi-Montalcini (1909-2012), Barbara McClintock (1902-1992), Laura Bassi (1711-1778), Elizabeth Garrett Anderson (1836-1917), Lise Meitner (1878-1968), Eva Crane (1912-2007), Maria la Giudea (karibia karne ya I-III baada ya Kristo), Mary Anning (1799-1847).

SIKU YA KIMATAIFA YA WANASAYANSI WANAWAWAKE NA WASICHANA
13 February 2022, 11:10