Tafuta

Vijana wa kitanzania wametakiwa kuhakikisha kwamba, wanasoma kwa juhudi, bidii na maarifa, ili waweze kujitegemea na hatimaye kulitegemeza Taifa. Vijana wa kitanzania wametakiwa kuhakikisha kwamba, wanasoma kwa juhudi, bidii na maarifa, ili waweze kujitegemea na hatimaye kulitegemeza Taifa. 

Vijana Jiwekeeni Malengo ya Kujitegemea na Kulitegemeza Taifa

Serikali inawataka vijana wa Kitanzania wahakikishe kwamba wanajiwekea malengo ya kusoma kwa juhudi, bidii na maarifa ili kupata maarifa yatakayolisaidia Taifa kupata maendeleo. Pia, Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Elimu kufanya mapitio ya sera ili kuifanya sekta hiyo kuendelea kuboreka na hivyo kufanya vizuri zaidi na zaidi.

Na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mbulu, Manyara.

Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka vijana wa Kitanzania wahakikishe wanajiwekea malengo ya kusoma kwa bidii ili kupata maarifa yatakayolisaidia Taifa kupata maendeleo. Pia, Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Wizara ya Elimu kufanya mapitio ya sera ili kuifanya sekta hiyo kuendelea kuboreka na hivyo kufanya vizuri zaidi. Ameyasema hayo Jumatatu, Januari 24, 2022 alipokagua ujenzi wa madarasa ya shule za Sekondari za Gehandu na Nowu katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu mkoani Manyara.

Waziri Mkuu amesema kuwa Serikali kwa upande wake imejipanga ipasavyo na itaendelea kuweka mazingira bora ya kujifunza na kufundishia ili kuwawezesha kufikia malengo yao. Ujenzi wa madarasa hayo unatokana na fedha za Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19, yaani Ugonjwa wa Virusi vya Korona, UVIKO-19. “Vijana someni kwa bidii hadi mfike chuo kikuu.” Pia, Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote ziweke mpango wa ujenzi wa mabweni kupitia mapato yao ya ndani ili wanafunzi wakae shuleni na kupata muda wa kutosha wa kujisomea. Kadhalika, Waziri Mkuu amewakumbusha watumishi wa umma kutambua kuwa wanajukumu kubwa la kuwatumikia Watanzania na kutekeleza maelekezo ya ilani ya uchaguzi ya CCM.

Awali, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Gehandu, Mwalimu Gadiel Bei alimshukuru Mheshimiwa Rais Samia kwa kutoa fedha za ujenzi wa vyumba hivyo viwili vya madarasa. Alisema mbali na madarasa hayo pia wamejenga madarasa mengine matano kati yake mawili yametokana na fedha za ruzuku ya EP4R na matatu ni nguvu za wananchi na Halmashauri. Mwalimu Bei alisema kukamilika kwa madarasa hayo kutaiwezesha shule hiyo yenye wanafunzi 945 wa kidato cha kwanza hadi cha sita kuongeza tahasusi nyingine ya kidato cha tano kuanzia mwezi Julai 2022.

 

26 January 2022, 10:49