Tafuta

Dawa iliyofanyiwa uzoefu wa tiba ya UVIKO-19 ambayo inaitwa Molnupiravir. Dawa iliyofanyiwa uzoefu wa tiba ya UVIKO-19 ambayo inaitwa Molnupiravir. 

UNICEF Imetia saini ya mkataba wa kusambaza dawa mpya Molnupiravir ya kuzuia virusi

UNICEF ilitia saini mikataba kadhaa ya muda mrefu na wasambazaji kwa ajili ya usambazaji wa dawa mpya ya Molnupiravir ya kuzuia virusi vya UVIKO-19.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Usambazaji wa dawa mpya ya Molnupiravir kwa upande wa UNICEF,  unategemea mapendekezo ya kimatibabu, vibali vya udhibiti na utiifu wa mahitaji ya uhakikisho wa ubora wa UNICEF. Mnamo Desemba, Utawala wa Chakula na Dawa wa Marekani ulifuta matumizi ya dharura ya Molnupiravir katika kutibu UVIKO-19 kwa wagonjwa wengine. Dawa ya Molnupiravir kwa sasa iko chini ya tathmini na uangalizi  wa Shirika la Afya Duninai (WHO). Kwa njia hiyo UNICEF imetia saini mikataba kadhaa ya muda mrefu na wasambazaji kwa ajili ya usambazaji wa dawa mpya hiyo ya Molnupiravir ya kuzuia virusi vya UVIKO-19.

Kipato cha chini na kati kufikiwa matibabu mapya 

Makubaliano haya yatasaidia kuhakikisha kuwa nchi za kipato cha chini na cha kati zina ufikiwaji kwa wakati wa matibabu mapya ya UVIKO-19. UNICEF itaendelea kufanya kazi na washirika na makampuni ya ACT-A (Upatikanaji na Kuharakisha Zana za UVIKO-19) ili kuhakikisha upatikanaji wa vifaa, kufikia bei nafuu na kuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya nchi. Vifaa hivyo pia vitapatikana kwa washirika wa ACT-A wanaotaka kusambaza dawa mpya ya Molnupiravir katika nchi. UNICEF itafanya kazi pamoja na washirika wengine wa ACT-A, kama vile Shirika la Afya Duniani (WHO), Mfuko wa Fedha Duniani na Unitaid ili kuhakikisha upatikanaji sawa wa dawa kwa nchi za kipato cha chini na cha kati.

19 January 2022, 10:44