Tafuta

Mwaka jana kaskazini mashariki walirekodi zaidi ya asilimia 70% ya ukiukwaji mbaya sana dhidi ya watoto nchini Siria. Mwaka jana kaskazini mashariki walirekodi zaidi ya asilimia 70% ya ukiukwaji mbaya sana dhidi ya watoto nchini Siria.  

Siria:vurugu bado zinaendelea na watoto wawili wameuawa

Wiki hii kituo cha maji yanayosaidiwa na UNICEF kilishambuliwa na kubomolewa katika kijiji cha Arshani, nje ya Idlib nchini Siria.Shambulizi hili limesababisha kukosekana kwa huduma ya maji kwa zaidi ya watu 241,000 na walio wengi ni wasio na makazi.Watoto na huduma zao hawawezi kabisa kushambuliwa,UNICEF imethibitisha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ilikuwa ni siku ya nne tu, tangu mwaka 2022 uenze lakini kutokana na vurugu zinazoendelea, watoto wawili wameuawa na wengine watano wamejeruhiwa huko Kaskazini magharibi mwa Siria. Mwaka jana kaskazini mashariki walirekodi zaidi ya asilimia 70% ya ukiukwaji mbaya sana dhidi ya watoto nchini Siria. Hayo yamesemwa na Kambou Fofana mkurugenzi wa UNICEF f wa Kaskazini mwa Nchi za Mashariki ya Katina Afrika Kaskazini. Wiki hii kituo cha maji yanayosaidiwa na UNICEF kilishambuliwa na kubomolewa katika kijiji cha Arshani, nje ya Idlib.  Shambulizi hili limesababisha kukosekana kwa huduma ya maji kwa zaidi ya watu 241,000 na walio wengi wakiwa ni wasio na makazi. Watoto na huduma zao hawawezi kabisa kushambuliwa. Ni miaka 11 sasa ya vita mbaya dhidi ya watoto wa Siria. Kwa kipindi kirefu sasa inawezekana kuendelea hivi? Anauliza msemaji huyo wa UNICEF.

Lakini ni kwa nini ukimya huo juu ya vurugu dhidi ya watoto Siria: Iacomini-Italia

Naye Andrea Iacomini, Mwakilishi wa UNICEF nchini Italia amesema vita nchini Siria havijaisha hata kama haisemwi tena au kutangazwa kwenye vyombo vya habari na kijamii. Ikifika mwezi wa tatu, itafikisha miaka 12 tangu kuanza kwa vita hivyo.  Vimekuwa vita na vurugu nyingi dhidi ya watoto wote kike, vita ambavyo utafikiri haviishi. Je ni nanma gani ya kwenda mbele na kwa sababu gani ya ukimya huo? Ni swali la mwakilishi wa Unicef Italia, baada ya kuwakilisha Nchi za Mashariki na Afrika Kaskazini amezungumzia juu ya tukio la kuuawa kwa watoto 2 vile vile kuhusu kushambuliwa kwa vituo vya maji. Na kwa maana hiyo anasikitika na kusema kwamba watoto na huduma zao zinazowahudumia hao hazipaswi kushambulia kamwe.

Afghanistan, theruji inazidisha hali mbaya na watoto

Kama ilivyokuwa imetabiriwa miezi iliyopita nchini l’Afghanistan wanaishi kipindi cha kutisha kwa sababu ya kufikia kwa baridi na theruji kwa mfano mjiniKabul. Amebainisha hayo msemaji wa UNICEF wa Italia  Andrea Iacomini kuwa  joto limeweza kushuka hadi -9 wiki hii. Wahudumu wao wamesimulia kuwa wamesikia historia za watu na familia zinazochoma fanicha, viatu au matairi ili kuwapa joto watoto wao, wasichana na wavulana ambao hawana mahali pa kujikinga na baridi, kuna hatari ya mauaji. Kutokana na kuporomoka kwa uchumi, Waafghanistan hawana chochote cha kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya mwanzo wa majira ya baridi na maelfu ya familia zilizokimbia makazi ndizo zilizo katika hatari zaidi. Ni lazima kuchukua hatua haraka kwa sababu theluji na barafu hivi karibuni vitafunga barabara nyingi nchini Afghanistan na hatari ya kuacha maelfu ya watu bila upatikanaji wa bidhaa na huduma muhimu kwa miezi

05 January 2022, 16:37