WHO inahimiza  kupata chanjo ili kupambana na UVIKO-19 hasa wakati huu ambapo wimbi la nne liitwalo Delta linasambaa kwa kasi sana WHO inahimiza kupata chanjo ili kupambana na UVIKO-19 hasa wakati huu ambapo wimbi la nne liitwalo Delta linasambaa kwa kasi sana 

UVIKO-19:WHO yazindua tahadhari kuhusu wagonjwa mahututi

Ulaya iko katika mtego wa virusi vya Uviko-19 kwa mara nyingine tena.Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO)linaonya juu ya dhana ya waathirika milioni mbili kufikia kipindi cha mwezi wa tatu 2022 ikiwa hatutajikinga kupitia chanjo na hatua nyingine za kiafya.

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Covid-19 au UVIKO-19 ndio sababu kuu ya vifo barani Ulya na Asia ya Kati. Ujumbe wa Shirila la Afya Ulimwenguni ( WHO) unaonesha kuwa katika Bara la Kale vifo vinavyohusishwa na virusi vimezidi kuongezeka kwa 4,200 kila siku ya  wiki iliyopita, mara mbili ikilinganishwa na mwezi  Septemba. Kwa mujibu wa Shirika linasema “ Tunaweza kutabiri  shinikizo la juu au kali juu ya vitanda vya hospitali katika nchi 25 za Ulaya na shinikizo kubwa au kali kwa vyumba vya wagonjwa mahututi katika nchi 49 kati ya nchi 53 kufikia mwezi Machi 2022.”

Kwa mujibu wa WHO, ili kubadilisha hali hii ni muhimu kuimarisha usimamizi wa chanjo. Miongoni mwa sababu zilizosababisha hali hii zaidi ni kuenea kwa aina nyingine ya vursu iitwayo Delta, inayoambukiza zaidi; Maelekezo kutoka baadhi ya nchi ni kwamba dharura iko juu yetu kwa sababu ya uwepo wa idadi kubwa  ya watu ambao bado hawajachanjwa.

Nchini Italia, hatua dhidi ya wimbi la nne inasimamiwa kwa uchunguzi wa Green Pass au kadi ya kijani za asili tofauti kwa waliochanjwa na wasio na chanjo na wajibu wa dozi ya tatu kwa wataalamu wa kiafya. Dozi ya nyongeza ya chanjo imetarajiwa kutoka miezi 6 hadi 5 na kwa watu kuanzia umri wa miaka 40 hadi 59. Nchini Austria, wametangulia kwa miezi minne baada ya dozi ya  mwisho. Huko Ubelgiji, kiwanda cha Audi huko Brussels, moja ya sehmu kubwa zaidi ya utengenezaji wa magari nchini Ubelgiji, kimeamua kusimamisha uzalishaji kwa wiki kutokana na kuongezeka kwa visa vya UVIKO kati ya wafanyakazi. Marekani Jumanne ilitangaza kuwa imetuma dozi nyingine milioni 4.1 za chanjo hiyo nchini Vietnam na kufanya jumla ya dozi zinazotolewa na Marekani duniani kote kufikia karibu milioni 270.

24 November 2021, 13:20