Wakuu wa nchi za kimataifa na kikanda wanajadili hali ya Libya mjini Paris kwa kuzingatia uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 24 Desemba. Wakuu wa nchi za kimataifa na kikanda wanajadili hali ya Libya mjini Paris kwa kuzingatia uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 24 Desemba. 

Mkutano kuhusiana na masuala ya Libya umefunguliwa huko Paris

Wakuu wa nchi za kimataifa na kikanda wanajadili hali ya Libya mjini Paris kwa kuzingatia uchaguzi uliopangwa kufanyika tarehe 24 Desemba.Rais wa Ufaransa Macron amesisitiza hatari ya mchakato wa mpito kufutwa. Zaidi ya serikali ya umoja wa kitaifa, kiukweli kuna vituo tofauti vya nguvu,kwa mujibu wa mchambuzi Michela Mercuri

Na Sr. Angella Rwezaula – Vatican.

Mkutano wa Kimataifa kuhusu Libya, ulioitishwa  na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, kwa kushirikiana na Italia na Ujerumani, unafanyika leo hii 12 Novemba 2021  huko Paris Ufaransa kuthibitisha uchaguzi wa rais mwezi Disemba 24, katika  tarehe ya kumbukumbu ya miaka 70 ya uhuru wa nchi ya Kaskazini mwa Afrika. Tukio hilo linafanyika katika ‘Maison della Chimie’, yaani kituo cha Makongamano kilicho katika eneo la VII la mji mkuu wa Ufaransa. Mpango huo ulitangazwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, mwezi Septemba  uliopita wakati wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa.

Huu ni mkutano wa saba unaohusu mzozo wa Libya baada ya mikutano ya Paris (Mei 2018), Palermo (Novemba 2018), Abu Dhabi (Machi 2019), Berlin Mosi (Januari 2020), Berlin 2 (Juni 2021) na Tripoli (Oktoba). 2021)). Takriban wakuu ishirini wa kikanda na kimataifa wanashiriki, akiwemo Makamu wa Rais wa Marekani Bi Kamala Harris na Rais wa Misri Bwana Abdel Fattah al-Sisi. Pia nchi nyingine zinazowakilishwa ni Tunisia, Niger na Chad, nchi tatu jirani ambazo zinakabiliwa na athari kubwa zaidi za mgogoro wa Libya, katika suala la ukosefu wa utulivu, biashara ya silaha na uhalifu. Marais wa Uturuki na Urusi hawako kwenye mkutano huo, huku waziri wa mambo ya nje wa urusi Sergei Lavrov amezungumza akiwa Moscow. Rais wa Baraza la Mawaziri wa Italia Bwana Mario Draghi, Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, wawakilishi wa Umoja wa Mataifa walipanga na walikuwepo na Rais Macron. Kutoka Libya, Rais wa Baraza la Rais wa Libya, Mohamed Al Menfi na Waziri Mkuu Abdulhamid Dabaiba,

Kwa sasa suala kuu ni lile la tarehe: kura katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa rais imepangwa tarehe 24 Desemba na duru ya pili itakayowezekana imepangwa tarehe 20 Februari, wakati huo huo ikiwa pamoja na wabunge. Na badaye kuna msimamo wa mkuu wa Baraza Kuu la Serikali ya Libya, Khalid al-Mishri, ambaye aliomba kutokushiriki katika uchaguzi kutokugombea uchaguzi au kwenda kupiga kura. Al-Mishri alisema sheria za uchaguzi zilizotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa vyombo vya habari siku chache zilizopita zina dosari.

“Uchaguzi uko milangoni, alibainisha Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mkesha wa mkutano,  lakini vikosi vinavyotaka kukwamisha mchakato huo vinanyemelea”. Ni lazima kuweka vizingiti sawa aliongeza kusema  utulivu wa nchi uko hatarini. Katika wiki za hivi karibuni, Waziri wa Mambo ya Nje Najla Al-Mangoush alisimamishwa kazi kwa mara ya kwanza na kuwekewa marufuku ya kusafiri kwa"ukiukaji wa kiutawala na baadaye kurejeshwa na Waziri Mkuu Abdul-Hamid Dbeibah. Tunapitia hali ya mpito ambayo mipaka ya mamlaka haijafafanuliwa kwa usahihi, ameelezea Michela Mercuri, msomo  wa historia ya kisasa ya nchi za Mediterania.

Bi Mercuri anakumbuka kuwa Baraza la Rais na Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Tripoli zinafanya kazi. Anaeleza kuwa la kwanza, ambalo liliidhinishwa na Baraza la Wawakilishi tarehe 10 Machi 2021, kufuatia makubaliano yaliyofikiwa katika Jukwaa la Mazungumzo ya Kisiasa la Libya na upatanisho wa Umoja wa Mataifa, linafanya kazi za mkuu wa nchi. Wa pili ni mtendaji mkuu wa muda iliyoundwa kuunganisha serikali pinzani za Tobruk na Tripoli (Gna) baada ya makubaliano ya kusitisha mapigano yaliyofikiwa kati ya Khalifa Haftar na Fayez al-Serraj. Zaidi ya hayo, Bi Mercuri ametaja Baraza la Wawakilishi na Baraza Kuu la Nchi, akionesha kuwa ni vyombo viwili 'sambamba' vilivyoundwa ili kusawazisha kila mmoja na kwamba ni tarehe ya Makubaliano ya Shikrat ya 2015. Hatimaye, kuna kinachojulikana 5 + 5 kamati ya kijeshi, ambayo ni matokeo ya utaratibu wa utekelezaji wa Mkutano wa Berlin wa 2020.

12 November 2021, 14:13