Afghanistan: Unicef inashukuru Polis kwa ukarimu wa watoto na vijana wadogo. Afghanistan: Unicef inashukuru Polis kwa ukarimu wa watoto na vijana wadogo. 

Unicef:hatuwezi kuwaacha watoto wa Afghanistan wakati wa uhitaji

Unicef inaripoti kuwa karibu milioni ya watoto chini ya miaka 5 watateseka na utapiamlo wa kukithiri,ambao ni hatari kwa maisha kutokana na migogoro inayoendelea nchini Afghanistan.Ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Kanda wa UNICEF,George Laryea-Adjei.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Zaidi ya watoto milioni 4 miongoni mwao milioni 2,2 ni wasichana ambao hawaendi shule. Karibia watoto 300,000 wamelazimika kuacha nyumba zao wakiwa wamelala. Watoto na vijana wako wanapambana kwa hisia mbaya na hofu na wengi wao wameona mambo ambayo hayakupaswi kuonwa kamwe na watoto hao, na wanahitaji msaada wa kisaikolojia.  Watoto na vijana wako wanapambana kwa hisia mbaya na hofu na wengi wao wameona mambo ambayo hayakupaswi kuonwa kamwe na watoto hao. Ni kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mkurugenzi wa Kanda wa UNICEF George Laryea-Adjei. Katika wiki za mwisho, kutokana na kuongezeka kwa migogoro na ukosefu wa usalama, ni watoto wasio kuwa na hatia katika mgogoro wa Afghanistan wanalipa gaharama nzito sana. Sio hilo tu bali wengine wamelazimaka kuacha nyumba zao, wameondolewa na kukatisha masomo shuleni wakiwa wanajisomea vitabu vyao, na kupelekwa mbali na marafiki na kukosa hata huduma msingi ya afya inayoweza kuwaokoa na magonjwa kama vile polio na pepopunda.

Watoto wengi wameondilewa shuleni kwa kukimbia vita huko Afghanistan
Watoto wengi wameondilewa shuleni kwa kukimbia vita huko Afghanistan

Kwa mujubu wa mwakilishi wa Unicef amesema kuwa “Tunajua kuwa washirika wengine wanafikiria kukata misaada kwa Afghanistan. Hii inatia wasiwasi sana na inaleta maswali muhimu: Je! Tutakuwa na rasilimali za kutosha kuweka vituo vya afya kuendelea na kuhakikisha kuwa wajawazito wanaweza kuzaa bila kuhatarisha maisha yao? Je! Tutakuwa na rasilimali za kutosha kuweka shule wazi na kuhakikisha kuwa wasichana na wavulana wanaweza kutumia miaka yao ya ujifunzaji katika nafasi salama na za kukaribisha? Je! Tutakuwa na rasilimali za kutosha kuokoa maisha ya mamia ya maelfu ya watoto wenye utapiamlo wa kukithiri?

JE MSAADA UTATOKA WAPI KUOKOA MAISHA YA MAMIA ELFU YA UTAPIAMLO?
JE MSAADA UTATOKA WAPI KUOKOA MAISHA YA MAMIA ELFU YA UTAPIAMLO?

UNICEF imekuwa Afghanistan kwa miaka 65 imesambaza vituo vyake katika nchi yote. Katika miaka hii wamekuwa wakiwashirikisha wadau wote ili waweze kuongeza mwitikio wao katika mikoa yote. Tayari wanasaidia timu za afya na lishe lukuki  katika kambi zao zilizofunguliwa na ambazo zimejaa , walinzisha nafasi za kupendeza kwa ajili ya watoto, vituo vya lishe na maeneo ya chanjo, kuweka nafasi ya mapema misaada ya kuokoa maisha, na kusaidia maelfu ya wanafunzi katika madarasa ya elimu katika jumuiya. Lakini rasilimali zaidi ni muhimu kabisa amesema kwani vijana na watoto wamewambia  kuwa wanahitaji sana vifaa na huduma  msingi  mahitaji ambayo, ikiwa yakisaidiwa, jamii ya kibinadamu inaweza kujibu kwa urahisi. UNICEF hivi karibuni ilizindua ombi la Dola za kimarekani milioni 192 na wanawahimiza wafadhili kuongeza msaada wao kwa familia zilizo hatarini na watoto ambao wanajitahidi wakati wa mzozo wa kibinadamu unaoendelea kukua. Mahitaji ya watoto wa Afghanistan hayajawahi kuwa makubwa zaidi kulika sas ana wao hawawezi kuwatelekeza peke yao.

30 August 2021, 14:22