Tafuta

Migogoro nchini Afghanistan. Migogoro nchini Afghanistan. 

Ulimwengu:Migogoro ya nchi,siasa,jamii na mazingira

Kuanzia kusini hadi kaskazini,kuanzia magharibi hadi mashariki ya ulimwengu,hali halisi ya nchi kwa upande wa usalama na amani,mazingira na afya bado vipo mashakani.Wasiwasi mkubwa kwa nchi ya Afhanistani,temeko Haiti,moto unaozidi kuwaka kila kona.Wasi wasi mkubwa wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO kwa kisa cha Ebola huko Ivory Coast.

Na Sr. Angela Rwezaula – vatican.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linafanya kikao cha dharura leo kujadili hali nchini Afghanistan baada ya  kuinyakulia baada ya Watalibani kuunyakua mji mkuu wa nchi hiyo, Kabul hapo Jumapili 15 Agosti 2021. Hata hivyo Ofisi ya Katibu Mkuu wa umoja huo, kupitia msemaji wake, Stephane Dujarrick, mjini New York Marekani Jumapili Agosti 15 amesema kuwa, Katibu wa Umoja wa Mataifa (UN), Bwana Antonio Guterres anafuatilia yanayojiri Afghanistan kwa wasiwasi mkubwa, na anawahimiza Wataliban na pande zote zinazohusika kuchukua kila tahadhari katika kuyalinda maisha ya watu na kuhakikisha upatikanaji wa mahitaji ya kibinadamu. Ripoti kutoka Afghanistan zinasema kuwa Wataliban wamechukua udhibiti kamili wa serikali, baada ya aliyekuwa rais, Ashraf Ghani kuikimbia nchi hapo jana. Marekani imeondoka katika ubalozi wake mjini Kabul na kuwahamishia raia wake katika uwanja wa ndege ambao sasa imeuweka chini ya ulinzi wake. Ujerumani pia imewaondoa raia wake kutoka Afghanistan na nchi nyingine nyingi miongoni mwaka hata Italia. Katibu Mkuu ana wasiwasi hasa juu ya mustakabali wa wanawake na wasichana, na haki zao ambazo zilipatikana kwa taabu lazima zilindwe. Umoja wa Mataifa pia umetangaza utayari wake wa kutoa msaada wa kibinadamu kwa Waafghanistan wote walio katika uhitaji

Tetemeko Haiti: Wakati wakiendelea kuchimba kwenye vifusi kwa kutafuta waliopotea, takwimu mpya zinazungumzia karibu watu 1300 wamekufa. Mahospitali yamejaa na wamewapokea majruhi 5,700 na maelfu waliobaki bila kuwa na nyumba. Hata hivyo hatari mpya inakuja na njia ya dhoruba ya kitropiki iitwayo Neema.

Magofu na vifusi huko Haiti
Magofu na vifusi huko Haiti

Nchini Zambia Tume ya taifa ya uchaguzi nchini Zambia imemtangaza Hakainde Hichilema kuwa mshindi katika uchaguzi wa rais uliofanyika Alhamisi 12 Agosti  iliyopita, akimbwaga rais wa sasa Edgar Lungu. Mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi ya Zambia Esau Chulu ameyatangaza matokeo rasmi asubuhi ya Jumatatu 16 Agosti, baada ya kupatikana hesabu za majimbo yote isipokuwa moja tu. Hesabu hizo zimeonesha kuwa Hakainde Hichilema wa chama cha United Party for National Development (UPND) amepata kura 2,810,777 akimpita kwa mbali rais wa sasa Edgar Lungu kutoka chama cha Patriotic Front (PF) aliyepata kura 1,814,201. Wapiga kura milioni 7 walikuwa wamejiandikisha kupiga kura katika nchi hiyo yenye idadi jumla ya wakaazi karibu milioni 19.

RAIS MTEULE HICHILEMA AKITOA NENO NYUMBANI KWAKE LUSAKA 16 AGOSTI 2021
RAIS MTEULE HICHILEMA AKITOA NENO NYUMBANI KWAKE LUSAKA 16 AGOSTI 2021

Cameroon/Chad: Kuna karibu wakameroon elfu kumi ambao kwa siku hizi kutokana na vurugu zao za ndani wamepata kimbilio nchini Chadi mahali ambapo hata hivyo ni hali ngumu ya kibinadamu kwa mujibu wa Umoja wa mataifa ambao wamthibtishisha ni nzito sana.

Cambodia: Leo hii umeanza mchakato wa kukata rufaa kwa kiongozi wa mwisho hai  wa Khmer Rossi, kiongozi wa zamani wa nchi mwenye umri wa miaka 90 Khieu Samphan. Mara ya kwanza alipatikana na hatia ya mauaji ya kimbari kwa uhalifu uliofanywa kati ya mwaka 1975 na 1979.

Ivory Coast: Wasi wasi mkubwa wa Shirika la Afya Ulimwenguni WHO juu ya kisa cha Ebola kugunduliwa huko Abidjan, ya kwanza kwa karibu miaka 30. Kijana aliyeambukizwa amefika kutoka Guinea, miezi miwili baada ya kutangazwa kumalizika kwa janga hilo nchini humo.

MHUDUMU KWA WAGONJWA WA EBOLA HUKO GUINEA
MHUDUMU KWA WAGONJWA WA EBOLA HUKO GUINEA

Moto: Mamlaka wanauita moto kaskazini mwa Algeria kuwa chini ya udhibiti. Huko Hispania, mkoa wa Avila unawaka, ambapo zaidi ya watu 600 wamehamishwa. Moto a ambao umechoma milima ya Uyahudi pia ulikuwa mkubwa sana na ulilazimisha zaidi ya watu elfu 10 waondoke nyumbani mwao. Miali ya moto bado ipo katika maeneo mengi ya Italia na hatua kadhaa za vikosi vya zima moto vinaendelea.

MOTO UMEZIDI KUTEKETEZA MILIMA,MISITU NA MAKAZI
MOTO UMEZIDI KUTEKETEZA MILIMA,MISITU NA MAKAZI
16 August 2021, 11:53