Vikosi vya uokoaji vinaendelea guko Haiti kutokana na tetemeko kali la ardhi. Vikosi vya uokoaji vinaendelea guko Haiti kutokana na tetemeko kali la ardhi. 

Haiti:vifo vimefikia 1300 kufuatia na tetemeko la ardhi!

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Haiti, vifo vinazidi kuongezeka,kwani hadi sasa vimefika 1300 baada ya tetemeko la ardhi,wakati huo majeruhi zaidi ya elfu tano na wengine bado hawajulikani kutokana na kufunikwa vifusi.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Idadi ya waathiriwa imeongezeka  kwa kushangaza siku mbili baada ya mtetemeko wa ardhi wenye nguvu wa 7.2 Richter ambao Jumamosi asubuhi 14 Agosti 2021 umeleta hofu na uharibifu mkubwa hasa katika eneo la kusini-magharibi mwa nchi, Haiti. Wakati dunia ikiendelea kutetemeka kwa matetemeko kama hayo ya ardhi, habari inayofika sasa inazungumza juu ya watu 1300 ambao wamekufa na zaidi ya watu 5000 wamejeruhiwa, na idadi isiyojulikana bado haijapatikana, kwa maana hiyo tunafikia takwimu za kutisha ambazo watu wa kisiwa hicho wana kumbukumbu iliyo wazi ya tetemeko la ardhi la miaka kumi na moja iliyopita (2010).

Harakati za kutafuta waliofunikwa kwenye vifusi
Harakati za kutafuta waliofunikwa kwenye vifusi

Sala ya pamoja kwa Bikira Maria na baadaye kuungana na Kanisa zima la Bara na ulimwengu kwa ajili ya kuomba mshikamano na kujitoa katika ngazi zote ìili kupunguza athari za janga hili ambalo bado iko hai, alifanya hivyo Papa Francisko mara baada ya tafakari na sala ya Malaika wa Bwana kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro Vatican, wakati Mama Kanisa anadhimisha Siku Kuu ya Kupalizwa Bikira Maria Mbinguni. Kufuatia na suala hili, ukusanyaji wa zana kwa upande wa Caritas internationalis umeanza mara moja na mfuko tayari wa euro elfu 50, ambao kwa watu wote wenye mapenzi mema wanaomba na wanaweza kushiriki kupitia katika Tovuti ya: www.caritas.org/donate-now/haiti-earthquake 2021: kwa ajili kuhudumia chakula , maji, mahema, usafi na vifaa vya huduma ya kwanza.

Kanisa Kuu limehabribiwa na tetemeko huko Haiti
Kanisa Kuu limehabribiwa na tetemeko huko Haiti

Tetemeko hilo lenye ukubwa wa 7.2 katika kipimo cha Richter lililotokea Jumamosi lipiga takriban maili 100 upande wa magharibi mwa mji mkuu wenye wakazi wengi wa Port-au-Prince, ambao pia uliharibiwa vibaya na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea mwaka 2010. Shirika la ulinzi wa raia limesema majengo 13,600 yameporomoka na zaidi ya 13,700 yameharibiwa, huku mamia ya watu wakifunikwa chini ya vifusi na wengine zaidi ya 5,700 wakijeruhiwa. Hali hiyo wanasema  ni makisio ya chini kwani  kiwango cha maafa kamili bado hakijaonekana. Janga la Jumamosi limetokea wakati nchi hiyo ikikumbwa na mzozo wa kisiasa kufuatiwa kuuawa kwa rais wake, Jovenel Moise mwezi uliopita. Waziri mkuu Ariel Henry ametangaza hali ya dharura ya mwezi mzima na kuwataka Wahaiti kuonesha mshikamano.

Huduma kuasaidia majeruhi Haiti
Huduma kuasaidia majeruhi Haiti
16 August 2021, 13:43