Licha ya mkataba wa haki za wakimbizi kwa miaka mingi,wataalamu  na wachambuzi wanasema bado hadi sasa hakuna nia ya dhati ya kisiasa ya kulinda haki za wakimbizi Licha ya mkataba wa haki za wakimbizi kwa miaka mingi,wataalamu na wachambuzi wanasema bado hadi sasa hakuna nia ya dhati ya kisiasa ya kulinda haki za wakimbizi 

Leo ni miaka 70 ya mkataba wa wakimbizi

Leo ni maadhimisho ya miaka 70 ya Mkataba wa Wakimbizi.Ni mkataba wa kimataifa na msingi katika maisha ya walio wengi.Katika fursa hii UNHCR,Wakala wa Wakimbizi wa UN,inasema kuwa upyaisho wa kujitolea katika roho na kanuni msingi za Mkataba haujawahi kuwa wa haraka na dharura kuliko leo hii.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ni miaka 70 tangu kusainiwa kwa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa kuwalinda wakimbizi 1951. Mkataba wa kuwalinda wakimbizi uliotiwa saini huko  Geneva  Uswiss ni msingi katika kuwalinda wakimbizi. Mkataba huo inaeleza mkimbizi ni mtu wa namna gani, na ni haki zipi na wajibu wao walio nao. Watu walioondoka nchini mwao kutokana na hofu ya kuteswa kutokana na rangi zao, dini, utaifa, uanachama wao katika kundi fulani la kijamii ama kutokana na misimamo yao ya kisiasa kama ilivyoainishwa kwenye maandishi ya mkataba huo, wana haki ya kuwa kwenye kundi hilo. Kutokana na vita ya pili ya Dunia na kukua kwa mivutano; Umoja wa Mataifa ulipitisha makubaliano hayo mjini Geneva mwaka 1951. Mwanzoni, hata hivyo mkataba huu ulijikita kuwalinda baadhi ya watu pekee hasa wakimbizi wa Ulaya mara baada ya vita ya pili ya dunia. Ili kutenda haki kutokana na mabadiliko ya hali halisi duniani kote, makubaliano yalitanuliwa mwaka 1967, na nchi 149 zimetia sahihi moja ya mikataba au yote miwili.

Kwa mujibu wa Bwana Filippo Grandi, Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi katika fursa ya siku hii amesema “Mkataba unaendelea kulinda haki za wakimbizi ulimwenguni kote.  Shukrani kwa Mkataba huo, mamilioni ya maisha ya wanadamu yameokolewa. Miaka sabini baada ya kuandikwa kwake, ni muhimu sana kwamba jamii ya kimataifa itetee kanuni ambazo inazitaja”. Hata hivyo Kamishna Mkuu ameonesha wasiwasi mkubwa juu ya majaribu ya hivi karibuni yaliyofanywa na serikali kadhaa yaliyolenga kupuuza au kukwepa kanuni za Mkataba, kutoka kufukuzwa na vifaa vya wakimbizi na waomba hifadhi katika mipaka ya ardhi na bahari, hadi mapendekezo ya kuhamisha kwa nguvu kwa nchi watu wengine kuchukua maombi ya ulinzi wa kimataifa bila ulinzi wa kutosha wa kisheria.

Miaka 70 baada ya siku ambayo Mkataba wa 1951 unaohusiana na Hadhi ya Wakimbizi uliwasilishwa kwa Nchi zao ili watie saini, Bwana Filippo Grandi amethibitisha kwamba mkataba huo ni sehemu msingi ya sheria ya haki za binadamu ya kimataifa na kwamba inaendelea kuwa muhimu sana leo hii, kama ilivyotayarishwa na kukubaliwa. “Lugha ya Mkataba iko wazi juu ya haki za wakimbizi na inaendelea kutumika katika muktadha wa changamoto na dharura za kisasa, kama vile janga la COVID-19”, amesisitiza Bwana Grandi.

Mkataba wa Wakimbizi wa 1951 na Mkataba wa hivi karibuni wa Global Compact juu ya Wakimbizi unaoomba suluhisho la kupatikana kwa haki sawa kwa wale ambao wanalazimika kukimbia kupitia ushirikiano wa kimataifa. Bwana Grandi amesisitizia juu ya hitaji la jumuiya ya kimataifa kutetea kanuni kuu kuhusu  ulinzi wa wakimbizi uliowekwa katika Mkataba, pamoja na haki ya kukimbia aina zote za mateso na kutolazimishwa kurudi katika hali ambazo zinawaweka dhuluma au hatari. Maadhimisho ya miaka 70 ya Mkataba wa Wakimbizi unakuja miezi michache tu baada ya Shirika la kuhudumia wakaimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) lenyewe kusherehekea miaka sabini tangu ilipoteuliwa kama shirika lililopewa jukumu la kulinda watu waliolazimika kukimbia.

29 July 2021, 15:40