Ghasia za Israeli na Palestina zinaendelea Ghasia za Israeli na Palestina zinaendelea 

Machafuko yanayoendelea Yerusalemu ni ukiukwaji wa haki za binadamu

Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa Bi Michelle Bachelet ameelezea wasiwasi wake mkubwa kuhusiana na mwendelezo wa ghasia katika maeneo yanayokaliwa ya wapalestina ikiwemo Yerusalemu mashariki na Israeli katika siku za hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Bi Bachelet, ambaye ni Kamishna mkuu wa haki za binadamu wa umoja wa mataifa, Bwana Rupert Colville wakati akizungumza na waandishi wa habari tarehe 11 Mei 2021 mjini Geneva Uswisi, amesema machafuko yanayoendelea ni ukiukwaji wa haki za binadamu akinukuu takwimu kuhusu majeruhi na vifo hadi sasa.

Kwa mujibu wa Shirika la wapalestina la  Hilal nyekundu, wapalestina 915 wamejeruhiwa kati ya tarehe 7 na 10 Mei  2021 huko Yerusalemu mashariki na zaidi ya watu 200 ukingoni mwa Magharibi ya Mto Yordan kutokana na mashambulizi kutoka vikosi vya usalama vya Israeli.  Mpalestina mmoja mwenye uraia wa Israeli ameripotiwa kuuwawa nchini Israeli. Mpaka sasa ni zaidi ya askari 20 wa Israeli ambao wamejeruhiwa kutokana na machafuko hayo.

Bwana Colville ametoa rahi kwa vyombo vya usalama vya Isareli ili kuhakikisha vinalinda haki za binadamu na uhuru wa kijieleza na mkusanyiko :“ Hakuna haja ya kutumia nguvu kwa wale wanaotekeleza haki yao ya kujieleza na kukusanyika, na iwapo kutakuwa na uhitaji wa kutumia nguvu basi itatakiwa kufuata muongozo wa kimataifa wa haki za binadamu. Tuna wasiwasi zaidi na athari zinazowapata watoto na tunatoa wito kwa UNICEF kuhakikisha watoto wanalindwa na kuondolewa kwenye hatari ya kupata madhara.”  Bwana Rupert Colville pia ametoa wito kuhusiana na watu waliokamatwa kutokana na ghasia zinazoendelea waachiliwe huru.

12 May 2021, 14:36