Msumbiji:watu wanatafuta mahali pa kukaa kutokana na uharibifu na mauaji yaliyofanywa na waasi katika mji Palma huko Cabo Delgado Msumbiji:watu wanatafuta mahali pa kukaa kutokana na uharibifu na mauaji yaliyofanywa na waasi katika mji Palma huko Cabo Delgado 

Msumbiji:Mashambulizi makali huko mji wa Palma Jimbo Cabo Delgad

Makumi kadhaa ya watu wameuawa wakati wa mashambulio ya kikatili katika mji wa Palma jimbo la Cabo Delda nchini Msumbiji kutoka kwa waasi waliojihami ambayo yameripotiwa kuingia jijini humo mwishoni mwa mwezi Machi.Watu zaidi wamekimbia wilaya hiyo kuelekea maeneo mengine ikiwemo hata mpakani na Tanzania,kwa ujibu wa msemaji wa Kuratibu misaada ya Dharura(OCHA).

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yameripoti kuwepo kwa mashambulizi dhidi ya raia kwenye mji wa Palma jimboni Cabo Delgado nchini Msumbiji na kusababisha maelfu ya watu kukimbilia maeneo ya jirani ikiwemo mpakani na Tanzania. Mashirika hayo lile la uhamiaji, IOM, mpango wa chakula duniani, WFP, ofisi ya kuratibu misaada ya dharura, OCHA na lile la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, yamesema makumi kadhaa ya watu wameuawa wakati wa mashambulio hayo kutoka kwa waasi waliojihami ambayo yameripitiwa kuingi amhini humo mwishoni mwa wiki

Bwana Jens Laerke ambaye ni msemaji wa Kutaribu misaada ya Dharura ( OCHA), amesema kile kinachoendelea Palma ni ukatili dhidi ya raia kutoka kwa makundi yaliyojihami yasiyo ya kiserikali, “na ndio maana nasema wamefanya vitendo vya kikatili, wanaendelea kufanya na tumepata ripoti mashambulizi yanaendelea na tunazungumzia uwezekano wa watu zaidi kukimbia wilaya ya Palma kuelekea maeneo mengine ikiwemo mpakani na Tanzania.”  Naye Paul Dillon ni msemaji wa Shirika la Uhamiaji la IOM amefafanua kuwa hadi tarehe 30 Machi, watu 3,361 ambao ni familia 672 wamesajiliwa na shirika hili ( IOM) na kwamba, “watu hao wanawasili wilaya za Ulongwe, Mueda, Montepuez na Pemba wakitokea  Palma kwa mguu, mabasi na  ndege.”

Kwa upande shirika la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) linasema familia zimekimbia ghasia na zinatafuta hifadhi misituni huku zaidi ya watu 100 wamesafiri kwa boti kutoka Palma hadi Pemba. Tangu mashambulizi dhidi ya raia yaanze huko Cabo delgado mwezi Oktoba mwaka 2017, zaidi ya watu 670,000 wamekimbia makwao, imesema shirika la wahamiaji ( IOM) huku nusu yao wakiripotiwa kuwa ni watoto wanaohitaji msaada wa dharura.

Likiangazia athari za mashambulizi hayo kwa raia, UNHCR kupitia msemaji wake Andrej Mahecic imesema watu wanauawa, wanakatwa viungo, mali zao zimeporwa na mashamba yameharibiwa.  “Watu wamefukuzwa kwenye nyumba zao wakiwa na virago vichache mno. Wanawake na watoto wa kike wanatekwa na kulazimishwa kuolewa, katika matukio mengine visa vya kubakwa au aina nyingine ya ukatili wa kingono vimeripotiwa. Huku kukiweko ripoti pia za watoto kutumikishwa na waasi waliojihami.”

Shirika la Mpango wa Chakula (WFP) pamoja na kwamba limekwisha sambaza misaada ya tani 250 ya chakula kwa watu 16,000 huko Palma, bado linasema msaada zaidi umesitishwa kutolewa kutokana na ghasia zinazoendelea, ingawa wahudumu wa afya imebidi wapelekwe ili kutoka huduma za dharura kwa majeruhi na wenye uhitaji zaidi.

02 April 2021, 16:07