MLIPUKO WA VOLKANO HUKO MTAKATIFU VINCENT KISIWANI CARIBEAN. MLIPUKO WA VOLKANO HUKO MTAKATIFU VINCENT KISIWANI CARIBEAN. 

Caribbean-UNICEF:msaada wa kwanza watolewa kwa watoto wapatao elfu 5!

Mlipuko wa volkano huko mtakatifu Vincent na Grenadines umesababaisha watu kukimbia makazi yao ambao msaada karibia wa watoto 5000 umeanza kutolewa na Unicef.Utapiamlo uliokithiri au unyafuzi ni tishio kubwa la uhai kwa watoto nchini Sudan Kusini.Watu 34 wamekufa maji baada ya boti kutoka Yemen kuzama kwenye bahari ya Sham ikiwa njiani kuelekea Djibouti.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Kati ya watu 16.000 na 20.000 wakiwemo watoto wameokolewa dhidi ya mlipuko wa Volkano ‘La Soufriere’ huko Mtakatifu  Vincent na Grenadine siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita kwa mujibu wa Unicef katika Kisiwa cha Caribbien.  Pamoja na wadau wa l’UNICEF wameanza kwa haraka kutoa msaada wa kibinadamu karibia kwa watoto 4.800 ambao wanahitaji msadda na ambao wako katika ukimbizi. Na zaidi wanatarajia familia zaidi ya 1000 zilizohama na hali mbaya ambao wanahitaji msaada wa kiuchumi wa haraka kutokana na kukatishwa kwa msaada wao kuweza kuihsi. Jumla ya makazi 62 ​​yamefunguliwa katika kisiwa hicho na ni makazi ya watu wasiopungua 3,200. Katika masaa 24 kufuatia mlipuko huo, UNICEF iliwapatia takriban watu 9,000, pamoja na watoto, upatikanaji wa maji salama na usafi wa mazingira katika makao ya uokoaji. Vifaa hivi muhimu ni pamoja na makopo ya maji yanayoweza kukukunywa na makontena, vidonge vya kuyatakasa na vifaa vya binafsi.

Wasi wasi wasi kwa usalama  wa familia za Mtakatifu Vincent na Grenadines

“Wasiwasi wetu mkubwa ni ustawi na usalama ambao sio tu ya watoto takribani 5,000 na familia zao katika maeneo ya hatari ya haraka lakini pia kwa wale wote waliko Mtakatifu Vincent na Grenadines”, kwa mujibu wa  Aloys Kamuragiye, Mwakilishi wa UNICEF huko Carribien Mashariki. “Chini ya masaa 24 tumesambaza msaada wa maji na kuokoa mazingira huko Mtakatifu Vincent, lakini rasilimali zaidi zinahitajika kutoa msaada wa kibinadamu kwa familia ambazo bado zinahitaji msaada huu” amesisitiza." Kulingana na makadirio ya awali, UNICEF inaomba zaidi ya dola za kimarekani 900,000 ili  kukidhi mahitaji ya haraka kwa wiki 6 zijazo, pamoja na maji ya kuokoa maisha na usafi wa mazingira.

Utapiamlo Sdan Kusini  tishio kubwa kwa watoto

Utapiamlo uliokithiri au unyafuzi ni tishio kubwa la uhai kwa watoto nchini Sudan Kusini ambako shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF kwa kutambua hilo linachukua hatua na sasa ya kuhakikisha wanasaidia watoto hao  chini Sudan Kusini  ambapo mwaka huu pekee watoto milioni 1.4 wako hatarini kukumbwa na Utapiamlo uliokithiri, lakini kwa msaada, ugonjwa huo unaweza kutibiwa na pia kuzuilika.

Watu 34 wamekufa maji baada ya boti kutoka Yemen kuzam bahari ya Sham 

Watu 34 wamekufa maji baada ya boti walimokuwa wakisafiria kukimbia machafuko nchini Yemen kuzama kwenye bahari ya Sham ikiwa njiani kuelekea Djibouti. Na taarifa ya shirika la uhamiaji la Umoja wa Mataifa, IOM, tarehe 12 Aprili 2021  huko Obok, nchini Djibouti imesema boti inayo milikiwa na wasafirishaji haramu wa binadamu ambayo ilikuwa imebeba wahamiaji 60 na imezama asubuhi kwa saa za Djibouti. Tukio hili la karibuni ni miongoni mwa matukio yanayotokea kila mwaka kwenye eneo hilo ambapo maelfu ya vijana wa kiafrika wanafanya safari za hatari kutoka nchi kama vile Somalia, Eritrea na Somalia wakipitia Djibouti na Yemen ili kwenda kutafuta maisha bora katika nchi za ghuba. IOM inasema janga la COVID-19 linalazimisha watu kurejea nyumbani kutokanana mipaka kufungwa.  Mwezi uliopita, wasafirishaji haramu wa binadamu waliwatupa kwenye bahari ya Sham watu 80 waliokuwemo kwenye boti kwa madai kuwa boti hiyo ilikuwa inazama baada ya kubeba watu wengi kupindukia. Watu watano kati ya hao walikufa maji.

Wahamiaji wanaendelea kumiminika Djbouti kutokea Yemen licha ya hatari hizo

Licha ya hatari hizo, wahamiaji wanaendelea kumiminika Djibouti kutokea Yemen ambapo mwezi Machi pekee, wahamiaji zaidi ya 2,343 waliwasili Djibouti kutokea Yemen, ikilinganishwa na mwezi uliotangulia wa Februari ambapo idadi illikuwa 1,900. Idadi kubwa walikuwa wanarejea nyumbani Ethiopia na Somalia. Mkuu wa IOM nchini Djibouti, Stephanie Daviot anasema kile ambacho IOM inafanya hivi sasa ni kushirikiana na mamlaka za Djibouti na mashirika ya kiutu na wahisani ili kumaliza mwenendo wa machungu wanayokumbana nayo wahamiaji. Wakati huo huo, IOM imesema makumi ya maelfu ya wahamiaji kutoka pembe ya Afrika wamekwama Yemen na wanaishi katika mazingira magumu, wakiwa hawana maji, chakula, huduma za tib ana usalama. Kwa wale ambao wanataka kurejea nyumbani, wanalazimika kuwalipa wasafirishaji haramu kiwango kikubwa cha fedha. IOM inachofanya ni kuwapatia chakula, maji safi, huduma za matibabu na ushauri nasaha hususan wale waliopitia machungu wakati wa safari. Tayari wahamiaji zaidi ya 6,000 nchini Yemen wamejisajili ili kurejea nyumbani kwa hiari na IOM inatoa wito kwa serikali kwenye ukanda huo kuchukua hatua zadi kufanikisha mpango huo wa kurejea nyumbani kwa hiari, VHR. Ili kufanikisha, mwezi uliopita, IOM ilizindua ombi la dola milioni 98 ili kusaidia wahamiaji walioko Pembe ya Afrika na Yemen.

13 April 2021, 15:33