Rubani  mwanamke wa Afrika Kusini anaonesha wanawake namna ya kujithibiti Rubani mwanamke wa Afrika Kusini anaonesha wanawake namna ya kujithibiti  

UNICEF:Zaidi ya wasichana milioni 10 wako hatari ya ndoa za utotoni sababu ya COVID-19

Ripoti mpya: “COVID-19:Tishio kwa maendeleo dhidi ya ndoa za utotoni”,imezinduliwa katika Siku ya Wanawake kimataifa.Ripoti hiyo inakumbusha kuwa kufungwa kwa shule,shida za uchumi,kuvurugika kwa huduma,ujauzito na vifo vya wazazi kwa sababu ya janga la Covid-19 zinachochea hatari zaidi ya wasichana kuolewa mapenda wakiwa wadogo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ulimwenguni leo hii kuna wanawake na wasichana milioni 650 ambao wamelazimishwa kuolewa katika ndoa utoto. Kwa kipindi cha miaka 10 milioni 25 ya ndoa za utotoni zimeepukwa. Ni katika Ripoti iliyotolea na Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto UNICEF katika kilele cha Siku ya wanawale dunia tarehe 8 Machi 2021, ambapo katika muktadha huowamezindua  tafiti mpya ambapo wanathibitisha kuwa ikiwa hakuna jitihada zaidi inawezekana kuona zinaongezeka ndoa za utotoni milioni 10 tena zaidi  ifikapo mwaka 2030, na kutishia miaka ya maendeleo endelevu. Ripoti COVID-19: A threat to progress against child marriage”, yaani "COVID-19: Tishio kwa maendeleo dhidi ya ndoa za utotoni", kwa hakika imetolewa katika siku hii ya Wawake duniani na ambayo inakumbusha kwamba kufungwa kwa shule, shida za uchumi, kuvurugika kwa huduma, ujauzito na vifo vya wazazi kwa sababu ya janga la virusi vya corona zinawaweka kuchochea hatazi zaidi ya wasichana kuolewa mapenda wakiwa wadogo.

Hata kabla ya janga la COVID-19, wasichana milioni 100 walikuwa katika hatari ya kuolewa mapema ifikapo mwaka 2030, licha ya kupunguzwa kwa kiwango kikubwa katika nchi kadhaa katika miaka ya hivi karibuni. Katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, asilimia ya wanawake vijana ulimwenguni ambao wameolewa wakiwa wadogo wamepungua kwa 15%, kutoka 1 kati ya 4 hadi 1 kati ya 5, sawa na ndoa karibu milioni 25 zilizoepukwa, hatua ambayo sasa iko hatarini. Kwa mujibu wa Bi Henrietta Fore, Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF amesema kuwa “janga la COVID-19 kwa mamilioni ya wasichana imefanya kuwa hali mbaya zaidi. Shule zilizofungwa, kutengwa na marafiki na mitandao ya msaada, na kuongezeka kwa umaskini kulichochea moto katika ulimwengu ambao ulikuwa ukijaribu kuzimwa jambo hili. Lakini hatuwezi  na lazima tuchanganue ndoa za utotoni. Siku ya Wanawake Duniani ni wakati muhimu kujikumbusha kile ambacho wasichana hawa wanaweza kupoteza ikiwa hatutachukua hatua sasa ya  elimu, afya na wakati endelevu”.

Wasichana wanaoolewa wakiwa watoto wanakabiliwa na athari za haraka na za maisha. Wana uwezekano mkubwa wa kupata unyanyasaji wa nyumbani na uwezekano mdogo wa kuendelea na masomo yao. Ndoa za mapema huongeza hatari ya ujauzito wa mapema na bila mpango pamoja na shida na vifo vya akina mama. Mazoezi haya yanaweza pia kuwatenga wasichana kutoka kwa familia na marafiki na kuwatenga kutoka kushiriki katika maisha ya jamii zao, mzigo mzito kwa afya yao ya akili na ustawi.  Janga la virusi vya Corona au  COVID-19 inaendelea kuathiri sana maisha ya wasichana. Vizuizi vya kusafiri na umbali wa kijamii kwa sababu ya janga hilo hufanya iwe ngumu kwao kupata huduma za afya, huduma za kijamii na msaada wa jamii, ambayo inawalinda kutokana na ndoa za utotoni, mimba zisizohitajika na unyanyasaji wa kijinsia. Wakati shule zimefungwa, wasichana wana uwezekano mkubwa wa kuacha shule na wasirudi shuleni. Kupoteza kazi na kuongezeka kwa usalama wa kiuchumi pia kunaweza kushinikiza familia kuoza binti zao ili kupunguza shinikizo la kiuchumi.

Ulimwenguni kote leo hii kuna wanawake na wasichana milioni 650 ambao wameozwa  wakiwa Watoto na  karibu nusu ya ndoa hizi zilifanyika nchini Bangladesh, Brazil, Ethiopia, India na Nigeria. Ili kukomesha athari za COVID-19 na kukomesha mazoea haya ifikapo mwaka 2030, ambao ndiyo mwisho wa Malengo ya Maendeleo Endelevu inahitaji kuharakishwa sana mkakati. Mwaka mmoja baada ya janga la Corona , hatua za haraka zinahitajika kupunguza mzigo kwa wasichana na familia zao amesisitiza Bi Fore. “Kwa kufungua shule, kutekeleza sheria na sera madhubuti, kuhakikisha upatikanaji wa huduma za afya na kijamii, pamoja na huduma za afya za uzazi na kutoa hatua kamili za ulinzi wa jamii kwa familia, tunaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari za kuibiwa utoto wao na ndoa za utotoni

SIKU YA WANAWAKE KIMATAIFA 8 MACHI
08 March 2021, 13:20