KIVU KASKAZINI HUKO DRC SI YA USALAMA N KIVU KASKAZINI HUKO DRC SI YA USALAMA N 

Congo DRC:kwa juma moja raia 32 wameuawa Kivu Kaskazini!

Kituo cha Mafunzo kwa ajili ya Amani,Demokrasia na haki za binadamu(CEPADHO)kinatoa mwaliko na kuwatia moyo jitihada za Rais wa Jamhuri ya Congo DRC na Rais wa Umoja wa Afrika katika kuandaa mkutano kwa ajili ya amani Afrika ili kupambana dhidi ya ugaidi kwa ngazi ya kibara.Hii ni kutokana na kuendelea mauaji ya kinyama huko Kaskazini mashariki mwa DRC na makundi yenye silaha.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Ni raia 32 walioawa wiki iliyopita Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC), kati ya Ituri na Kivu Kaskazini. Taarifa imetolewa na Kituo cha Mafunzo kwa ajili ya Amani, Demokrasia na haki za binadamu (CEPADHO). Kufuatia na mashambulizi hayo ambayo yanahusishwa na magaidi wenye silaha wenye asili kutoka Uganda (Nguvu za pamoja za kidemokrasia na ADF na Madinat Tawhid wa-l-Muwahidin(MTM,). Zaidi ya waathiriwa wanahesabau hata watu wengi waliotekwa nyara na wengine kupotea.

Mashambulizi ya mwisho ni yale ya  siku ya Jumamosi  27 na Dominika 28 Februari 2021, huko Kainama Kaskazi ni masharikimwa  eneo la Beni katika Wilaya ya Kivu Kaskazini ambapo magaidi wa ADF/MTM wamemuua mwanamme mmoja mzee na watoto na kuchoma nyumba sita wakati huko Bwakardi, eneo la Ituri, majihadi wameua raia 7 na kuchoma nyumba 2 na kuharibu vitu mbalimbali wakati wakitafuta chakula na vitu vyenye thamani. Kivu kaskazini ni wilaya ya mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo(DRC), mahali ambapo tarehe 22 februari 2021, wamuawa Balozi wa Italia nchini DRC,  Bwana Luca Attanasio, Afisa wake mlinzi, Vittorio Iacovacci, na dreva wa Congo,  Mustafa Milambo.

Katika eneo hilo kwa miaka kadhaa, inaendelea kuwa na hali ya ukosefu wa usalama kutokana na uwepo wa mamia ya makundi ya wanamgambo yenye silaha. Kwa maana hiyo kituo cha CEPADOH katika taaarifa yao iliyotumwa kwenye vyombo vya habari za kimisionari (Fides,) wanatia moyo jitihada za Rais wa Jamhuri ya Congo DRC na Rais wa Umoja wa Afrika (UA) katika kuandaa mkutano kwa ajili ya amani Afrika ili kupambana dhidi ya ugaidi kwa ngazi ya kibara. “Shirika letu linaomba kwamba wakati wa mkutano mkuu, ukabiliane na masuala ya kigaidi ya Beni na Ituri, kwa kuwatia moyo Mataifa rafiki wa DRC kuzingatia ulazima wa kuwasaidia wanajeshi katika kupambana dhidi ya  tishio la pamoja la  ADF / MTM mbao wanaungana na serikali ya kiislamu ya Daesh”.

01 March 2021, 17:45