Tafuta

   Harakati za Rais Biden za ushirikiano kikanda kwa masuala ya kuomba hifadhi,kuimarisha mfumo wa kuwapatia wakimbizi makazi mapya, kushughulikia mizizi ya machafuko na ukosefu wa usalama Harakati za Rais Biden za ushirikiano kikanda kwa masuala ya kuomba hifadhi,kuimarisha mfumo wa kuwapatia wakimbizi makazi mapya, kushughulikia mizizi ya machafuko na ukosefu wa usalama 

UNHCR:pongezi kwa Marekani kubadili mfumo wa kuomba hifadhi

Serikali ya Marekani,tarehe 2 Februari 2021 imetia saini maagizo yanayolenga kutoa usalama na suluhisho kwa wale wanaotafuta hifadhi kwa misingi kwamba wanahitaji ulinzi kutokana na machafuko na mateso katika nchi zao. Katika hatua hiyo Shirika la wakimbizi UNHCR limekaribisha mpango wa Rais Biden wa kuunda kikosi kazi cha kuwatafuta na kuwaunganisha familia zilizotengananishwa kwenye mpaka wa Kusini mwa nchi hiyo.

Shirika la Umoja la kuhudumia wakimbizi UNHCR limesema limefarijika na hatua ya serikali ya Marekani, Jumanne tarehe 2 Februari 2021 kutia saini maagizo yanayolenga kutoa usalama na suluhu kwa wale wanaotafuta hifadhi kwa misingi kwamba wanahitaji ulinzi kutokana na machafuko na mateso katika nchi zao.  Shirika hilo limekaribisha mpango wa Rais Joe Biden wa kuunda kikosi kazi cha kuwatafuta na kuwaunganisha familia zilizotengananishwa kwenye mpaka wa Kusini mwa nchi hiyo akisema kwamba “inaonesha maadili halisi ya kibinadamu.”

Kwa mujibu wa mwakilishi wa UNHCR, Bwana Matthew Reynolds kwa ajili ya Marekani na kwa maeneo ya caribbean amesema , “hatua hizi zinathibitisha utamaduni wa Marekani wa huruma na utu kwa walio hatarini na ni ishara muhimu kwa nchi zote duniani kuchukua hatua ambazo ni salama na za kibinadamu.”  UNHCR pia imesema kwamba hatua hiyo inathibitisha “uongozi wa Matekani wakati dunia ikishuhudia idadi kubwa ya watu kulazimika kutawanywa kuwahi kushuhudiwa tangu vita vya pili vya dunia.”  Aidha  “Hakuna anayetaka kulazimishwa kukimbia katika nchi yake, lakini ni bayana kwamba watu waliokata tamaa wanaokimbia machafuko Kaskazini mwa Amerika ya Kati hawakatishwi tamaa na sera kali utekelezaji kwa sababu maisha nyumbani hayafai kabisa.” Ameongeza Bwana Reynolds.

Rais Biden pia amearifiwa kuahidi kushirikiana na serikali nyingine na mashirika mengine kujenga uwezo wa kikanda wa masuala ya kuomba hifadhi, kuimarisha mfumo wa kuwapatia wakimbizi makazi mapya na kushughulikia mizizi ya machafuko na ukosefu wa usalama unaoendelea kulazimisha watu kukimbia kutoka sehemu za Amerika ya Kati.  Kwa mujibu wa Bwana Reynolds amesema, “Hatua zilizotangazwa na Marekani zinathibitisha umuhiumu wa mifumo bora ya kibinadamu ya ukimbizi na hatua zinazoratibiwa na serikali zote kuunda mazingira ambayo yatazuia familia kuchukua hatua za kukimbia makwao.”

Rais huyo mpya wa Marekani amechukua hatua ya haraka kubadili msimamo wa mtangulizi wake kuhusu uhamiaji. Kwa mujibu wa duru za Habari kuacha ujenzi wa ukuta wa mpaka uliopangwa kati ya Matrekani na Mexico, kuondoa marufuku ya kusafiri kwa mataifa mengi ya Kiislamu na kupunguzwa kwa idadi ya wakimbizi wanaopewa makazi mapya. Rais Biden pia ameanzisha muongozo wa mkakati wa kupata uraia kwa wafanyakazi wasio na hati wanaoishi Marekani.  UNHCR ambayo inafanyakazi katika nchi 130 duniani ina uzoegfu wa miaka 70 ya utendaji na imesema iko tayari “Kuunga mkono serikali ya Marekani kuhakikisha kwamba watu wanaohitaji ulinzi wa kimataifa, wakimbizi wanaosaka hifadhi pamoja na watu wasio na utaifa wanaweza kupata haraka hadhi hizo na bila vizuizi.”

Naye mkuu wa ofisi ya shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM mjini Washington DC, Bwana  Luca Dall’Oglio amesema “watu wanaoishi katika mazingira ya machafuko na kutawanywa kwa muda mrefu na mazingira mengine hatarishi wako katika hali mbaya na wanauhitaji mkubwa wa ulinzi hivyo hawapaswi kusahaulika. IOM imefurahishwa kuona kwamba suluhu za kibinadamu na kiutu kwa watu wanaokimbia ni kipaumbele muhimu kwa uongozi wa Biden.” Ameongeza kuwa kama mwanachama mwanzilishi wa IOM, Marekani imesaidia kazi za shirika hilo kwa muda mrefu katika historia na inaslia kuwa mshirika mkubwa katika kushughulikia changamoto na fursa za kibinadamu na uhamiaji kote duniani.

03 February 2021, 10:27