Balozi wa Italia na Afisa wake pamoja na Dreva wao wameuawa huko Drc katika mashambulizi na wamgambo Balozi wa Italia na Afisa wake pamoja na Dreva wao wameuawa huko Drc katika mashambulizi na wamgambo 

Masikitiko ya WFP kuhusu shambulio na vifo vya ujumbe wa ubalozi wa Italia huko DRC!

Kufuatia na shambulio dhidi ya ujumbe wa Ubalzio wa Italia uliokuwa ukizuru ndani ya Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC,Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP,limeelezea kusikitishwa kwake na kutuma salamu za rambirambi kwa familia,wafanyakazi na marafiki wa watu watatu waliouawa tarehe 22 Februari 2021.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican.

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP, limeelezea kusikitishwa kwake na kutuma salamu za rambirambi kwa familia, wafanyakazi na marafiki wa watu watatu waliouawa tarehe 22 Februari 2021 katika shambulio dhidi ya ujumbe wa ubalozi wa Italia uliokuwa ukizuru ndani ya Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.  Kwa mujibu wa WFP abiria wengine waliokuwa wakisafiri na ujumbe huo wamejeruhiwa wakati wa shambulio hilo. Watu watatu waliopoteza maisha ni balozi wa Italia nchini DRC Luca Attanasio, afisa wa ubalozi wa Italia na dereva wa WFP.  Ujumbe huo ulikuwa unasafiri kutoka Goma kuzuru programu ya WFP ya mlo shuleni katika eneo la Rutshuru wakati shambulio hilo lilipotokea.

Shirika la Mpango na chakula (WFP ) limesema litashirikiana na mamlaka ya DRC kubaini taarifa zaidi za waliohusika na shambulio hilo lililotokea katika barabara ambayo iliruhusiwa watu kusafiri bila kusindikizwa na vikosi vya  usalama.   Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani vikali shambulio hilo  dhidi ya msafara wa pamoja wa shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani, WFP na ubalozi wa Italia huko Kibumba karibu na Goma mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Shambulio hilo lililofanywa na watu wasiojulikana limesababisha vito ya watu watatu.

“Katibu Mkuu ametuma salamu za rambirambi kwa familia za wafiwa na serikali ya Italia na DRC huku akielezea mshikamano wake na wafanyakazi wa WFP na timu nzima ya Umoja wa Mataifa nchini humo,” imesema taarifa ya msemaji wa Guterres iliyotolewa  tarehe 22 Februari 2021 jijini New  York, Marekani. Katibu Mkuu ametoa wito kwa serikali ya DRC kuchunguza haraka tukio hilo na washukiwa wafikishwe mbele ya sheria huku akisema kuwa Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia serikali na watu wake katika kusaka amani ya kudumu mashariki mwa nchi hiyo.

23 February 2021, 13:18