Tafuta

Chanjo aina ya AstraZeneca/Oxford AZD1222 imeorodheshwa kwa matumizi ya dharura na WHO sasa linatathmini chanjo hiyo na matokeo yatatangazwa. Chanjo aina ya AstraZeneca/Oxford AZD1222 imeorodheshwa kwa matumizi ya dharura na WHO sasa linatathmini chanjo hiyo na matokeo yatatangazwa. 

Chanjo dhidi ya COVID-19 inaanza kusambazwa Afrika mwezi huu

Kwa mujibu wa mfumo wa usambazaji wa chanjo umebainisha kuwa mwezi huu kampeni ya chanjo karibu milioni 90 za COVID-19 zitaanza kusambazwa barani Afrika.

Kwa mujibu wa mfumo wa kusambaza chanjo za COVID-19, COVAX ulioundwa na Umoja wa Mataifa na wadau wake umebainisha kuwa mwezi huu kampeni ya chanjo karibu milioni 90 za COVID-19 zitaanza kusambazwa barani Afrika.  Chanjo hiyo aina ya AstraZeneca/Oxford AZD1222 imeorodheshwa kwa matumizi ya dharura na WHO ambapo sasa linatathmini chanjo hiyo na matokeo yatatangazwa. Maeneo mengine yameshuhudia yakianza utoaji wa chanjo ya COVID-19, lakini Afrika yenyewe ikiwa kando. Mpango huu wa kupeleka chanjo ni hatua ya kwanza muhimu katika kuhakikisha kuwa bara hilo linapata fursa sawa ya chanjo kama maeneo mengine. Amesema  hayo Dk.  Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika akizungumza katika mkutano na wanahabari kwa njia ya mtandao huku akisema  kwamba wanatambua  kuwa hakuna aliye salama hadi pale kila mtu atakuwa salama.

COVAX kupitia barua yake ya tarehe 30 Januari 2021, imejulisha nchi za Afrika kuhusu mpango huo wa upelekaji chanjo. Kutokana na kiwango kikubwa cha mahitaji ya chanjo ya COVID-19, shehena za mwisho zitategemea kiwango cha uzalishaji kutoka kwa kampuni husika na utayari wa nchi kupokea chanjo hizo. Nchi zinazopokea chanjo hizo zinatakiwa kuwasilisha mipango yao ya mwisho ya usambazi na utoaji wa chanjo hiyo kutoka COVAX.

Chanjo ya Pfizer yahitaji kuhifadhiwa ubaridi wa -70°C

Kandoni mwa chanjo hiyo ya sasa, dozi 320 000 za chanjo aina ya Pfizer-BioNTech zimepangwa kwa mataifa manne ya Afrika ambayo ni Cabo Verde, Rwanda, Afrika Kusini na Tunisia. Chanjo hii imepokelewa na WHO na kuorodheshwa kwa mahitaji ya dharura lakini inahitaji nchi kuwa na uwezo wa kuhifadhi na kusambaza katika kiwango cha nyuzi joto 70 chini ya sifuri katika kipimo cha selsiyasi. Katika kuwasilisha ombi za chanjo hiyo ya Pfizer, nchi zilitakiwa kuwasilisha maombi ambapo nchi 13 ziliwasilisha na maombi yao kufanyiwa tathmini ikiwemo kiwango cha sasa cha vifo kutokana na COVID-19 na uwezo wa kuhifadhi chanjo chanjo hizo katika joto la -70°C.

Dk. Moeti amesema kwa tangazo hili, nchi zinapata fursa ya  kujiandaa na kukamilisha mipango yao ya utoaji wa chanjo hiyo ikiwemo kuwa na mifumo sahihi ya majokofu ya kuhifadhi chanjo. “Hatuwezi kukubali kuharibika hata kwa dozi moja ya chanjo.” Awamu ya kwanza ya dozi milioni 90 itasaidia nchi hizo katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, kutoa chanjo kwa asilimia 3 ya wale walio hatarini zaidi wakiwemo wahudumu wa afya na makundi mengine yaliyo hatarini. Katika kuunga mkono juhudi za COVAX, Muungano wa Afrika, AU, umepata dozi milioni 670 za chanjo ya COVID-19 ambazo zitasambazwa mwaka huu wa 2021 na 2022 kwa kuwa nchi zimepata fedha. Benki ya African Export-Import itawezesha malipo kwa kupatia watengenezaji malipo ya awali ya dola bilioni 2 kwa niaba ya nchi husika.

06 February 2021, 17:12