Nchini Kazakhstani wamekomesha adhabu ya kifo tangu tarehe 2 Januari 2021 Nchini Kazakhstani wamekomesha adhabu ya kifo tangu tarehe 2 Januari 2021 

Jumuiya ya Mt.Egidio yapongeza nchi ya Kazakhstan kukomesha adhabu ya kifo!

Kutoka ofisi ya Urais wa Jamhuri ya Kazakhstan,tarehe 2 Januari 2021 imetangaza kukomesha adhabu ya kifo nchini humo.Kufuatia na suala hilo Jumuiya ya Mtakatifu Egidio inapongeza hatua hiyo muhimu katika utetezi wa haki za binadamu.Tangu 2006 Jumuiya hii imekuwa nao bega kwa bega katika mchakato wa safari hii ya utetezi wa haki ya mwanadamu.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Jumuiya ya Mtakatifu 'Egidio imepokea na kuridhika sana kuhusu kukomeshwa kwa adhabu ya kifo nchini Kazakhstan. Nchi ya Asia ya Kati kiukweli imeridhia Itifaki ya pili ya Hiari katika Mkataba wa Kimataifa wa Haki za Kiraia na Kisiasa, kama ilivyotangazwa tarehe 2 Januari, 2021 kutoka ofisi ua Urais wa Jamhuri hiyo, mara baada ya kujiunga na mkataba huo mwezi Septemba iliyopita. Hatua ya uamuzi wa kuheshimu maisha  kwa mujibu wa Jumuiya ya Mtakatifu Egidio,ilizinduliwa mnamo 2003, lakini ambayo kwa hali yoyote haikuzuia kutolewa hukumu mpya za kifo kwa uhalifu wa kipekee, ambao utabadilishwa kuwa kifungo cha maisha.

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio imekuwa bega kwa bega nao tangu 2006

Tangu 2006, Jumuiya ya Mtakatifu Egidio imekuwa ikisindikiza nchi ya  Kazakhstan bega kwa bega kwenye mchakati wa  njia hii kuelekea kuondoa kabisa adhabu ya kifo kupitia mikutano ya kimataifa juu ya masuala yanayohusiana na haki na amani, ambayo Rais wa sasa wa Jamhuri, Bwana Kassym-Jomart Tokayev, alishiriki. Hasa, kwa namna ya pekee wanakumbuka kujitoa kwa karibu miaka ishirini ya Tamara Chikunova na chama chake kiitwacho “Mama dhidi ya adhabu ya kifo na mateso”, kwa ajili ya kukomesha adhabu ya kifo katika eneo lote la zamani la ya kisovieti ya Asia ya Kati, kuanzia na nchi yake, Uzbekistan, ambapo alichangia kukomeshwa kwa adhabu ya kifo mnamo 2008, na imeongezeka sasa  kufutilia mbali katika nchi jirani ambayo imepata mafanikio katika eneo lote linalozungumziwa, hadi Mongolia.

Harakati za Jumuiya ya Mtakatifu Egidio kushimana na wenye shida wakati wa Noeli

Hata hivyo Jumuiya ya Mtakatifu Egio katika harakati zake za kutoa  mshikamano kwa walio wa mwisho, wakati wa siku kuu ya Noeli mwaka 2020, bado umeoneshwa kwa dhati kwani imeweza kutoa zawadi kwa watu 1,000 wasio na makazi, 1200 wazee maskini na 1,500 familia zilizo kwenye shida kubwa huko Napoli nchini Italia. Kwa mujibu wa Jumuiya hii, wamesema ilikuwa ni Noeli tofauti mwaka jana  lakini kwa kuendelea kuwa na marafiki, kuwapa joto na fuaha ya daima bila kusita. Kwa sababu, ikiwa umaskini na kuchanganyikiwa kumeongezeka karibu nao, mshikamano pia umezidi kukua.

Meza za chakula cha mchana kama utamaduni hazikuwepo, lakini zawadi ndiyo

Jumuiya ya Mtakatifu Egidio haikuweza kuandaa meza za kiutamaduni na kuungana kula pamoja na maaskini kama miaka mingine, lakini jitihada zao zimeongezeka za ubunifu ili kufanya siku kuu ya Noeli ifanikiwe hata katika kufuata kanunizilizo wekwa kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya virusi vya corona. Noeli imemfikia kila mtu: wale walio na shida sana, wale ambao ni masikini na wapweke, wale ambao hawana makazi, wale ambao ni wazee na wanahisi uzito wa kutengwa, wengi ambao, labda kwa mara ya kwanza maishani mwao, walijikuta wakilazimika kuomba msaada kwa sababu masikini na shida.

Watoto wa shule ya Amani na wafungwa vile vile zawadi zilitolewa

Hata watoto 200 wa “Shule za Amani “walipokea vitabu kama zawadi na kuandaa kadi za salamu ambazo zilitolewa pamoja na zawadi kwa wazee katika taasisi hiyo, kati ya walioathirika zaidi na janga hili. Wakati wa siku za Krismasi, mipango mingine ilipangwa huko Aversa, Salerno, Benevento na katika maeneo muhimu ya Napoli. Wafungwa wote wa magereza ya Poggioreale, Secondigliano na Pozzuoli walipokea zawadi ya kifurushi kidogo na vitu vya kutia moyo.

JUMUIYA YA MTAKATIFU EGIDIO
04 January 2021, 13:32