Rais John Pombe Magufuli akiwa Uwanja wa  Jamhuri Dodoma akitoa kiapo tarehe 5 Novemba 2020 Rais John Pombe Magufuli akiwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma akitoa kiapo tarehe 5 Novemba 2020 

Tanzania:Rais John Pombe Magufuli aapishwa!

Tarehe 5 Novemba 2020 Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania ameapishwa kuendelea na wadhifa wa urais kwa muhula wa pili madarakani,kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Oktoba 2020.Tukio limefanyika jijini Dodoma mji mkuu wa Tanzania kwa mara ya kwanza katika tukio kama hilo katika historia ya Tanzania.

 Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican.

Tarehe 5 Novemba 2020, Rais wJohn Pombe Magufuli  wa Tanzania ameapishwa  kuendelea na wadhifa wa urais kwa  muhula wa pili kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe  28 2020,  pia hata kiapo cha makamu wake Bi Samia Suluhu. Afla ya chereko chereko na usalama uliimarishwa kabla ya kuanza tukio hilo la  kuapishwa Rais Magufuli katika uwanja wa Jamhuri huko Dodoma Mji Mkuu wa Tanzania. Mwaka 2015 Rais Magufuli aliapishwa kwenye uwanja wa uhuru Dar Es  Salaam, lakini kwa muhula wa pili amekuwa Rais wa Kwanza kuapishwa Dodoma jambo ambalo wakati wa hotuba yake ya kwanza ameshukuru.

Rais Magufuli ameahidi wananchi wote kuendeleza yale yote ambayo tayari amekwisha anza na kukuza ushirikiano na nchi rafiki pamoja na taasisi mbali mbali kama ambavyo imekuwa kwa miaka mitano iliyopita. Katika hotuba yake kwa kusistiza zaidi, Rais Magufuli amesema kuwa atashirikiana na watu wote ili kuhakikisha kwamba yote aliyoahidi wakati wa kampeni zake yanatekelezwa. Hakusita kuweleza kwamba uchaguzi sasa umekwishwa na ndiyo ilikuwa kauli yake na kwamba jukumu kubwa linalobaki na ambalo ni muhimu mbele yao ni kuelendeza jitihada zaidi za kulijenga na kuleta maendeleo kwa nchi yao.

Tukio hilo limedhuriwa na marais, wawawakilishi,viongozi wa serikali na dini  wa ndani na nje Afrika, na wakati wa  kupewa fursa ya neno naye Rais jirani Bwana Yoweri Kaguta Museveni kati ya mambo mengi aliyosema muhimu ni suala la kuwaiga waasisi wa Afrika, kwa watanzania wote  hasa vijana amewashauri mambo a manne ambayo amesema yamekuwa yakiwaongoza viongozi mashuhuri wa Afrika na zaidi kushuhudia ushirikiano na baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, na kwa maana hiyo “udugu, ukombozi, matarajio na mikakati msingi wa kitaifa”. Guaride la kijeshi, nyimbo, ngoma kutoka Zanzibar vilitangulia na hatimaye kwa kuhitimishwa afla hiyo na nyimbo mchanganyiko kutoka kwa wasanii.

05 November 2020, 16:55