Siku ya kimataifa ya kuzuia unyonyaji wa mazingira katika hali za vita kivita na migogoro Siku ya kimataifa ya kuzuia unyonyaji wa mazingira katika hali za vita kivita na migogoro 

Siku ya kimataifa ya kuzuia unyonyaji wa mazingira katika hali ya vita na migogoro

Siku hii uadhimishwa kila ifikapo tarehe 6 Novemba kila mwaka ambayo ilitangaza tangu 2001.Papa Francisko anasema ikiwa tunataka maendeleo fungamani ya kibinadamu kwa wote,ni lazima kufuata jitihada bila kuchoka za kuzuia vita.Na Padre Kureethadam:sisi ni familia moja ya wanadamu inayoishi katika nyumba ya pamoja.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican.

Na katika ujumbe wa Papa Francisko kwa njia ya mitandao ya kijamii, katika fursa ya Siku ya Kimataifa ya Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuzuia unyonyaji wa mazingira katika hali za  vita na migogoro ya kisilaha anasema, Vita ni kukataa haki za wote ni janga la kusonga mazingira. Ikiwa tunataka kwa dhati  maendeleo fungamani ya kibinadamu kwa wote, ni lazima kufuata bila kuchoka jitihada za kuzuia vita. Lengo la Siku hii inayohamasishwana UN ni kukuza uelewa kati ya jamumuiya ya kimataifa juu ya athari mbaya zinazozalishwa kwenye mazingira na mizozo ambayo leo hii bado inaendelea leo, kwa sababu vita sio tu vinaua askari na raia kwa silaha, lakini pia zinaua au kuhatarisha maisha kupitia uharibifu wa maliasili, kupungua kwa ardhi na kutoweza kulima ardhi ya kilimo, ukataji miti hovyo, jangwa, kuambukizwa kwa watu, sumu na vitu vingine vya sumu zitokanazo na nikeli na tindikali.

Ujumbe ambao Umoja wa Mataifa  UN unakusidia kuhamasisha Siku hii ni kuhakikisha kuwa ulinzi wa mazingira ni sehemu ya mikakati iliyo pana ya kuzuia migogoro na kulinda amani. “Haiwezekani kuwa na amani ya kudumu  ​​ikiwa maliasili na mifumo ya ekolojia ambayo maisha ya watu hutegemea imeharibiwa”. Tivuti ya Umoja wa Matiafa Italia (Onuitalia.it) imeandika. Sio hivyo tu, udhibiti wa maliasili ni moja ya sababu zinazosababisha mizozo. Uchunguzi wa Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa (UNEP) umeonyesha kuwa katika miaka 60 iliyopita angalau 40% ya mizozo yote ya ndani ilihusiana na unyonyaji wa maliasili.

Siku ya leo  inaonekana, kwa maana hiyo kuwa na fursa zaidi kwa mujibu wa maoni ya Padre Joshtrom Kureethadam, mwenye asili ya India, na mratibu wa Sekta ya Ekolojia  ya Baraza la Kipapa la Huduma ya Maendeleo Fungamani ya watu ambaye ameeleza akihojiwa na Vatican Nes kufafanua juu ya mpango mzuri kama huo. “Ni mada ya zamani  amekumbuka  kwa sababu tayari katika Biblia, katika Kumbukumbu la Torati, juu ya kuzingirwa kwa mji, kwa muda mrefu, inashauriwa kutokata miti yake na sio kutia sumu katika visima, kwa sababu maumbile yamekuwa yakiteseka katika vita pamoja na ubinadamu.

Lakini pia ni suala la mada kubwa ya sasa . Hivi karibuni, tulikuwa kwa mfano, na vita vya Ghuba: mabomu yalikuwepo na tukaona kwamba theluji ambayo wakati huo ilianguka katika mlima wa Himalaya, maelfu ya kilomita, ilikuwa ni nyeusi, kwa sababu ya athari za mazingira ilikuwa imefikia hata huko juu ya mlima.  Kwa ujumla, Padre  Kureethadam,amesema vita vinaleta madahra makubwa hasa kwa wanadamu lakini pia jamii zinazoteseka, na hasa kaka na dada walio katika mazingira magumu, maumbile pia yanateseka kwa maana hiyo ni suala linaloangukia watu wote na tunahitaji kuzmuza zaidi juu ya suala hili.

06 November 2020, 16:55