UN umezindiua hatua ya kuzuia usambazaji wa taarifa za uongo mitandaoni,tarehe 21 Oktoba 2020 na kutoa  wito kwa watu kutoa ahadi ya kutulia kabla ya kusambaza taarifa mitandaoni. UN umezindiua hatua ya kuzuia usambazaji wa taarifa za uongo mitandaoni,tarehe 21 Oktoba 2020 na kutoa wito kwa watu kutoa ahadi ya kutulia kabla ya kusambaza taarifa mitandaoni. 

Umoja wa Mataifa wasihi watu wote duniani kuahidi kutulia kwanza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres akizindiua hatua ya kuzuia usambazaji wa taarifa za uongo mitandaoni, tarehe 21 Oktoba 2020 ametoa wito kwa watu ulimwenguni kote kutoa ahadi ya kutulia kwanza kabla ya kusambaza taarifa mitandaoni.

Kupitia kampeni ya kutulia kwanza kabla ya kusambaza taarifa mitandaoni, iliyopewa kitambulish cha mada au hashtag #PledgetoPause, yaani ahadi ya kutulia kwanza kabla ya kusambaza taarifa ambazo bado hazijathibitishwa, ni sehemu ya kampeni pana ya mabadiliko ya tabia ambayo inakusudia kuunda kanuni mpya za mitandao ya kijamii kusaidia kupambana na athari zinazoongezeka za habari potofu zinazosambaa.  Kupitia katika video fupi ambayo Katibu Mkuu Guterres ameiweka katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter na Instagram, kiongozi huyo wa Umoja wa Mataifa ameanza kwa kutulia kwa takribani sekunde 5 ili kuonesha angalau kwa mfano kwamba watumiaji wa mitandao wanatakiwa kutulia kidogo kabla ya kuanza kusambaza video ambazo hawajawa na uhakika na kilichomo katika video hizo na ikiwa ni cha kweli au la na kisha akasema, “wakati wa janga la COVID-19, taarifa potofu inaweza kuwa hatari. Ahidi kutulia kwanza na usaidie kuzuia kusambaa kwa habari potofu.” Mtindo wake huo alioutumia kutulia kwa sekunde chache na kisha kutoa ujumbe, unategemewa kuigwa na kurudiwa na viongozi wengi wa ulimwengu, watu wenye ushawishi na pia wananchi kote ulimwenguni. 

Kampeni ya Pause au Tulia ni sehemu ya kampeni kubwa ya #Ziliyothibitishwa, mpango wa Umoja wa Mataifa uliozinduliwa mnamo Mei 2020 ili kuwasilisha habari za kiafya zinazoweza kuthibitika kisayansi hususani wakati wa mshikamano wa ulimwengu wakati wa COVID-19.  Kampeni hii imetumia ushahidi wa utafiti kwamba mtumiaji wa mitandao anapochukua muda kiasi kutulia na kuitafakari taarifa kabla ya kuisambaza, inapunguza uwezekano wa kusambaza taarifa za kushitusha na za uongo. Dai hilo limesindikizwa na video moja kuhusu mnyama Paka ambayo inaonekana mtu akiisambaza pasipo kujiridhisha kilichomo ndani na kina lengo gani na hivyo kusababisha taharuki kwa jamii dhidi ya  aka jambo ambalo halikuwa sahihi. 

Kampeni hii ya Tulia kwanza kabla ya kusambaza taarifa mitandaoni inalenga kuwafikia watu bilioni 1 duniani kote kupitia mitandaoni na wadau kufikia mwezi DesembaAsasi za kiraia zinazounga mkono kampeni hii ni pamoja na mashirika yanayojitolea kupambana na habari potofu kutoka kote duniani ikiwemo Chequeado, Newschecker.in na First Draft wakati barani Afrika mashirika au makampuni ya habari kama MultiChoice, na Yuvaa wanasaidia kusambaza ujumbe wa kampeni hiyo.

Kwa upande wake Bi  Melissa Fleming, ambaye ni Mkuu wa Idara ya mawasiliano ya umma wa Umoja wa Mataifa akihusisha hatari ya habari potofu na ugonjwa wa COVID-19 unaosababishwa na virusi vya corona amesema, “COVID-19 sio tu janga la kiafya, lakini dharura ya mawasiliano pia. Wakati habari potofu inaenea, umma hupoteza uaminifu na mara nyingi hufanya maamuzi ambayo yanakwamisha hatua ya umma na hata maisha yao wenyewe. Inazidi kuwa wazi kuwa hatuwezi kufanikiwa kukabiliana na janga hilo bila pia kushughulikia habari potofu mtandaoni. Kila mmoja wetu anaweza kusaidia kuvunja mlolongo wa habari potofu kwa kutulia kabla hatujasambaza.” 

22 October 2020, 15:37