2020.08.01 kushirikishana chakula na maskini katika kipindi cha janga la corona nchini India. 2020.08.01 kushirikishana chakula na maskini katika kipindi cha janga la corona nchini India. 

UN Women/UNDP:COVID-19 yadumbukiza wanawake milioni 47 zaidi katika ufukara!

UN Women amesema kuwa ongezeko la wanawake kutumbukia katika ufukara ni ishara dhahiri ya mapungufu makubwa ya njia zilizoweka za ujenzi wa jamii zetu na uchumi wetu.Na UNDP inasema wanawake na wasichana zaidi ya milioni 100 wanaweza kuinuliwa kutoka umasikini endapo serikali zitatekeleza mkakati kwa lengo la kuboresha fursa za elimu na uzazi wa mpango,haki na usawa katika ujira na kupanua wigo wa masuala ya kijamii.

Takwimu zilizoainishwa katika Ripoti ya UNDP na UN Women inasema athari za COVID-19 zitabadili mtazamo wa umasikini uliokithiri katika kila kanda. Ripoti iliyopewa jina “Kutoka kwenye wazo kuingia kwenye hatua:Usawa wa kijinsia wakati wa COVID-9” zinaonyesha kwamba janga la COVID-19 litawatumbukiza watu milioni 96 kwenye ufukara ifikapo 2021, na milioni 47 kati yao ni wanawake na wasichana.

Kwa mujibu wa takwimu za pamoja za mashirika ya Umoja wa Mtaifa zinasema kiwango cha umasikini kilitarajiwa kushuka kwa asilimia 2.7 kati ya mwaka 2019 na 2021 lakini makadirio sasa yanaonyesha kutakuwa hivyo na kuna ongezeko la umaskini la asilimia 9.1 kutokana na athari za janga la corona au COVID-19.  Makadirio hayo yanaonyesha kuwa janga la COVID-19 litaasababisha umasikini duniani kote, na wanawake ndiyo wataathirika zaidi hususani walio katika umri wa kuzaa.  Kutokana na hivyo mashirika hayo yamesema ifikapo mwaka 2021 kwa kila wanaume 100 wa umri wa kati ya miaka 25 na 34 wanaoishi katika umasikini uliokithiri au ufukara wa chini ya dola 2 kwa siku kutakuwa na wanawake 118, na pengo hilo linatarajiwa kuongezeka hadi wanawake 121 kwa kila wanaumee 100 ifikapo mwaka 2030.

Mkurugenzi mtendaji wa wanawake wa Umoja wa Mataifa (UN Women) Bi Phumzile Mlambo Ngcuka akizungumzia juu ya  pengo hilo amesema “Ongezeko la wanawake kutumbukia katika ufukara hususan katika hatua hizo mbili za maisha yao ni ishara iliyo dhahiri ya mapungufu makubwa ya njia tulizoziweka za ujenzi wa jamii zetu na uchumi wetu. Tunajua kwamba wanawake ndiyo wanaobeba mzigo mkubwa wa kuhudumia familia, wanalipwa ujira kidogo, wanaweka akiba ndogo na wanafanya kazi zisizo na uhakika, ukweli ni kwamba kwa ujumla ajira ya wanawake iko hatarini kwa asilimia 19 zaidi ya wanaume.”  Kwa kusisitiza zaidi Bi. Ngcuka amesema  kwamba Ushahidi uliopo wa mapengo ya usawa ni muhimu zikachukuliwe hatua  na sera ambazo zitawaweka wanawake katika kitovu cha kujikwamua na janga hili.

Katika takwimu hizo zitaongeza idadi ya wanawake na wasichana wanaoshi katika umasikini wa kupindukia hadi kufikia milioni 432, huku matarajio yakionyesha kwamba ifikapo mwaka 2030 idadi hiyo haitashuka na kufika kiwango kama  ilivyokuwa kabla  ya mlipuko wa janga la COVID-19.  Kwa maana hiyo Takwimu hizo mpya pia zinasema janga hilo ni tishio kubwa katika matarajio ya kutokomeza umasikini ifikapo mwisho wa muongo huu. Na inawezekana ukweli halisi ukawa mbaya zaidi hasa ukizingatia kwamba haijajumuisha sababu nyingine kama vile wanawake kuacha kazi ili waangalie watoto wao wakati huu wa COVID-19 hali ambayo itaathiri mgawanyiko wa umasikini.

Kwa upande wake mkuu wa Shirika la Mipango na maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) Achim Steiner amesema “Wanawake na wasichana zaidi ya milioni 100 wanaweza kuinuliwa kutoka kwenye umasikini endapo serikali zitatekeleza mkakati wenye lengo la kuboresha fursa za elimu na uzazi wa mpango, haki na usawa katika ujira na kupanua wigo wa masuala ya kijamii. Wanawake wanabeba gharama za COVID-19 kwani wako hatarini zaidi kupoteza vyanzo vyao vya mapato na si rahisi kulindwa na hifadhi ya jamii hivyo kuwekeza katika kupunguza pengo la usawa wa kijinsia,na   sio tu kwamba ni busara bali pia ni chaguo la haraka linaloweza kufanywa na serikali kubadili athari za janga la corona katika kupunguza umasikini.”

Ripoti hiyo ya UNDP na UN Women inasema athari za COVID-19 zitabadili mtazamo wa umasikini uliokithiri katika kila kanda.  Wakati asilimia 59 ya wanawake masikini kabisa duniani hivi sasa wanaishi Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara, ukanda huo utaendelea kuwa mwenyeji wa idadi kubwa zaidi ya mafukara duniani. Na baada ya kupiga hatua kubwa katika kupunguza umasikini katika miaka michache iliyopita Asia Kusini inatarajiwa kukabiliana na kuibuka tena kwa umasikini uliokithiri. Ifikapo mwaka 2030 kwa kila wanaume 100 wa umri wa miaka 25 hadi 34 wanaoishi katika umasikini Asia Kusini kutakuwa na wanawake 129 masikini zaidi na hii itakuwa ni ongezeko kubwa kutoka makadirio ya 118 ifikapo mwaka 2021. Wakati takwimu hizi zinaogopesha utafiti unakadiria kwamba itahitaji asilimia 0.14 pekee ya pato la dunia sawa na dola trilioni 2 kuuinua ulimwengu kutoka katika umasikini uliokithiri ifikapo mwaka 2030, na dola bilioni 48 ndio zinazohitajika kuziba pengo la kijinsia la umasikini. Hata hivyo idadi kamili huenda ikawa ni ya juu zaidi endapo serikali zitashindwa kuchukua hatua au zitachelewa kuchukua hatua zinazohitajika.

03 September 2020, 14:02