Tafuta

Vatican News
Mabara ulimwenguni Mabara ulimwenguni 

Ulimwenguni:Ebu tutazame ya masuala ya kijamii na kisiasa!

Rusesabagina ashtakiwa na kufikishwa kizimbani akikabiliwa na mashitaka ya ugaidi.Rais Vladimir Putin wa Urusi amemuunga mkono rais wa Belarus Alexander Lukashenko na ameahidi kumpa mkopo wa dola bilioni 1.5.Hatua mpya ya majadiliano Ulayana na China kuhusu uwekezaji wa biashara.Korti ya Katiba Ivory Coast imemruhusu Rais Ouattara kugombea muhula wa tatu.

Na Sr.Angela Rwezaula – Vatican

Kwa mara ya kwanza tangu kukamatwa kwake mmoja wa wapinzani wakuu wa serikali ya Rwanda Paul Rusesabagina amefikishwa kizimbani mjini Kigali nchini Rwanda akikabiliwa na mashitaka ya ugaidi. Paul Rusesabagina alipata umaarufu mkubwa kupitia filamu maarufu kama Hotel Rwanda. Anashutumiwa kuendesha mauaji ya raia wasio na hatia kupitia mashambulizi ya kundi la wapiganaji wa FLN kusini magharibi mwa Rwanda miaka miwili iliyopita. Paul Rusesabagina amefikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya mwanzo ya wilaya ya Kicukiro mjini Kigali kujitetea dhidi ya kusikilizwa kesi yake akiwa nje au akiwa rumande. Hata hivyo Mawakili wake alionyesha vipingamizi vya aina tatu huku wakishikilia kwamba mahakama hii haina mamlaka ya kuendesha kesi yake. Mawakili wake pia wamesema kwamba kesi yake ilipaswa kusikilizwa katika  wilaya jirani ya Gasabo kwa sababu ndipo mtuhumiwa ana makazi. Jambo jingine mawakili wamesema kwamba mashtaka yanayomkabili aliyatenda akiwa nchini Ubelgiji na kwamba kwa kiasi kikubwa ilikuwa ni mikutano ya hadhara ambayo haikuhusu uraia wa mshukiwa upande wa mashtaka umesema kwamba, Paul Rusesabagina hakuwahi kupoteza uraia wa Rwanda kwa mujibu wa sheria na kwamba kisheria anachukuliwa kama raia wa Rwanda licha ya kuwa na uraia wa nchi nyingine. Mshukiwa huyu ni maarufu kwa sababu alijulikana sana kupitia filamu aliyoicheza mwaka 2004 kuhusu kuwaokoa watu zaidi ya 1200 katika mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi mwaka 94, filamu ambayo licha ya kutambuliwa na Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush kumpa tuzo ya ushujaa, manusura wa mauaji hayo waliadai filamu hiyo likuwa ni uzushi mtupu. Paul Rusesabagina ni raia wa Rwanda aliyekuwa na uraia wa Ubelgiji huku pia akiwa na hati rasmi inayompa haki ya kuishi nchini Marekani. Alionyeshwa mbele ya vyombo vya habari mnamo tarehe 31 mwezi uliopita mjini Kigali baada ya kukamatwa katika nchi ambayo mpaka leo haijajulikana na kwamba alikuwa na uhuru na haki ya kuifanya mikutano hiyo.

Urusi na Belarus: Putin amemuunga mkono Lukashenko akitaka ushirikiano zaidi na Urusi

Rais Vladimir Putin wa Urusi amemuunga mkono mwenzake wa Belarus Alexander Lukashenko aliyezungukwa na maandamano makali ya upinzani, na ameahidi kuipa Belarus mkopo wa dola bilioni 1.5. Katika mazungumzo baina ya viongozi hao yaliyofanyika  katika mji wa utalii wa Sochi, Lukashenko ameahidi kuimarisha ushirikiano na Urusi, ambayo ameitaja kama kaka mkubwa.  Hata hivyo Putin amesifu mpango wa kiongozi huyo wa kuandaa mabadiliko ya katiba katika juhudi za kuridhia matakwa ya upinzani. Rais Putin amesema mabadiliko hayo yataruhusu hatua mpya ya maendeleo ya kisiasa na kiuchumi nchini Belarus. Lukashenko amelaani teke teka za kijeshi zinazofanywa na jumuiya ya kujihami ya NATO karibu na mpaka wa Belarus, na amesema Urusi na nchi yake wako tayari kupambana na kitisho chochote.

Pwani ya Pembe:Mahakama ya Katiba ya Pwani ya Pembe imemruhusu Rais Ouattara kugombea muhula wa tatu

Mahakama ya katiba ya Pwani ya Pembe imemsafishia njia rais wa nchi hiyo Alassane Ouattara kugombea muhula wa tatu. Uamuzi huo umefuatiwa na maandamano yenye ghasia, yanayotishia kuitumbukiza nchi hiyo ya Afrika magharibi katika machafuko kwa mfano wa yale ya muongo mmoja uliopita, ambayo yaliangamiza maisha ya watu zaidi ya 3000. Aidha, mahakama hiyo hiyo imemzuia rais wa zamani Laurent Gbagbo, na kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro kugombea urais katika uchaguzi ujao. Majaji wa mahakama hiyo wameridhia wagombea wanne tu kati ya 44 waliotia nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 31. Miongoni mwa walioruhusiwa kusimama dhidi ya Ouattara no Konan Bedie, rais wa zamani wa Pwani ya Pembe ambaye sasa anao umri wa miaka 86. Waandamanaji wenye hasira walichoma magari katika miji ya Yopougon na Bangolo, kufuatia makabiliano baina ya wafuasi wa upinzani na maafisa wa usalama.

Ulaya na China:Hatua mpya ya majadiliano ya Ulana na China kuhusu biashara na uwekezaji

Hatua mpya jana katika mazungumzo ya Ulaya juu ya biashara, lakini bado kuna njia ndefu ya kuelekea. Baraza la UE hko Brussels inaomba Beijing kufungua kampuni za Ulaya, hali iliyowekwa na EU kwa makubaliano ya uwekezaji wa nchi mbili kufikia mwishoni mwa mwaka huu. Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na maafisa waandamizi wa Umoja wa Ulaya wamefanya mazungumzo na rais wa China Xi Jinping, wakijadili masuala ya biashara, uwekezaji na kujenga imani juu ya masuala magumu ya kisiasa. Mazungumzo kati ya pande hizo mbili zilizo na nguvu kubwa kiuchumi duniani na wafanyabiashara, ilikuwa ni fursa kwa Brussels na Beijing kuchukua usukani wa mahusiano yao huku Umoja wa Ulaya ukitaka kujikita zaidi katika masuala ya kiuchumi, mageuzi ya shirika la kimataifa la biashara WTO, mabadiliko ya tabia nchi na janga la virusi vya corona. Kabla ya kufanyika mazungumzo ya kibiashara, pande mbili zilitia saini mkataba wa kulinda vyakula na viywaji vinavyosafirishwa kwa kila mmoja. China ilikuwa ni soko la tatu kwa bidhaa za chakula za Umoja wa Ulaya mwaka 2019, zilizokuwa na thamani ya euro bilioni 14.5.

15 September 2020, 15:11