2020.05.27 BARA LA AFRIKA & MADAGASCAR NA BENEDERA ZAKE 2020.05.27 BARA LA AFRIKA & MADAGASCAR NA BENEDERA ZAKE  

Tanzania ina imani na UN ambao ujitathimini na wanachama wake pia!

Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa,Balozi Kennedy Gastorn wakati wa mahojiano na Idhaa ya Umoja wa Mataifa amesema Tanzania ina imani na Umoja wa Mataifa(UN),lakini akasema kuwa lazima umoja huo ujitathmini na wanachama wake pia wajitathmini.Amesema hayo siku moja kabla ya kutoa hotuba yake katika mjadala Mkuu wa mkutano wa 75 wa Baraza Kuu la UN.

Mjadala Mkuu wa mkutano wa 75 wa Baraza Kuu  la Umoja wa Mataifa, (UNGA75) unafunga pazia  Jumanne  tarehe 29 Septemba 2020 ambapo miongoni mwa nchi za Afrika ambazo zimeutubia ni pamoja na Tanzania, ambayo kwamba ujumbe wake mkuu kwenye jukwaa hilo ni kueleza kuwa bado Tanzania ina imani kubwa na chombo hicho chenye wanachama 193 japokuwa hata Umoja ujitathimini na wanachama wenyewe wajitathimini.

Akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa, Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Profesa Kennedy Gastorn, ambaye ni mwakilishi wa kusoma  hotuba hiyo kwa niaba ya Rais John Magufuli amesema,“ujumbe mkubwa kwanza ni huu, sisi tuna imani kubwa sana na Umoja wa Mataifa kama chombo ambacho kinaweza kuratibu shughuli za nchi zote duniani, kama chombo muhimu ambacho kwa kweli ni kama Bunge la dunia tunapokwenda kwenye Baraza Kuu. Hilo ni moja!”

Pamoja na hayo lakini amesema ni muhimu pia kusititiza, “Umoja wa Mataifa ujitathmini, na sisi pia kama wanachama wa Umoja wa Mataifa lazima tujitathmini katika ngazi ya nchi na katika ngazi ya umoja wetu. Tukishajitathmini basi tuweze kuwa na uhalisia katika kusaidia ili kuweza kusaidia kutekeleza majukumu yake kama ilivyoanishwa kwenye chata yake.”

Akazugumzia muktadha wa hoja ya Afrika kuhusu Umoja wa Mataifa amesema, “tunakwenda na ujumbe kwamba kama Afrika tuna mapendekezo ya maboresho ambayo tungependa sana Umoja wa Mataifa tuweze kuipa nafasi Afrika katika kuboresha mifumo ya utawala ndani ya Umoja wa Mataifa. Lakini pia ni wakati mwingine ambapo sisi kama nchi ni muhimu pia kutoa mchango katika baadhi ya mambo makubwa sana ya kimataifa yanayoendelea hapa duniani ambayo tuna michango mingi katika na maslahi yetu, na kama nilivyosema ni chombo ambacho kila nchi kinapaswa kulinda maslahi yake.”

Katika mjadala huu mkuu ulioanza tarehe 22 mwezi huu Septemba, wakuu wa nchi na serikali pamoja na mawaziri wametoa hotuba zao kwa njia ya mtandao kutokana na vikwazo vya janga la Corona au COVID-19 ambavyo vimelazimu mkutano kufanyika kwa mtandao na kutoka ukumbini. Hata hivyo ukumbini waliopo ni wawakilishi wa kudumu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa na kwamba hata Balozi Gastorn atahutubia kutoka ndani ya ukumbi wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

29 September 2020, 14:25