ITALY PANDEMIC CORONAVIRUS COVID-19 ITALY PANDEMIC CORONAVIRUS COVID-19 

Who:Asilimia 90 ya nchi 105 zimevurugwa na changamoto ya corona!

Katika utafiti uliofanywa na Shirika la Afya duniani (WHO)unaonesha takwimu zilizokusanywa katika nchi 105 duniani tangu mwezi Machi hadi Juni mwaka huu,kuwa takriban asilimia 90 ya nchi hizo huduma zake za afya zimekabiliwa na changamoto huku nchi za kipato cha chini na cha wastani zikionesha matatizo makubwa zaidi.

Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO, tarehe 31 Agosti 2020  limechapisha utafiti wake wa kwanza wa athari za janga la corona au COVID-19 katika  mifumo ya afya ulimwenguni. Katika utafiti huo uliofanyika na takwimu kukusanywa katika nchi 105 duniani tangu mwezi Machi hadi Juni mwaka huu, unaonyesha kuwa takriban asilimia 90 ya nchi hizo huduma zake za afya zimekabiliwa na changamoto huku nchi za kipato cha chini na cha wastani zikionesha matatizo makubwa zaidi.

Katika Utafiti wa Shirika la Afya duniani WHO unasema nchi nyingi zimesema utaratibu na huduma maalum zimesitishwa huku huduma za muhimu kama za upimaji wa saratani na matibabu ya  Virusi vya Ukimwi (VVU) yamekuwa katika hatari kubwa ya kuingiliwa katika nchi masikini. Akizungumzia utafiti huo mkurugenzi mkuu wa WHO Dr. Tedros Adhanom Ghebreyesua amesema “Utafiti huu unaweka wazi nyufa zilizopo katika mifumo yetu ya afya, lakini pia unatumika kutujuza mikakati mipya ya kuboresha utoaji wa huduma za afya wakati wa majanga na zaidi. COVID-19.  inapaswa kuwa somo la kujifunza kwa nchi zote ambazo afya sio suala la msingi, ni lazima tujiandae vyema kwa majanga ya ghafla lakini pia kuendelea kuwekeza katika mifumo ya afya ambayo itaweza kutimiza mahitaji ya watu wakati wote wa maisha yao.”

Kwa mujibu wa utafiti huo miongoni mwa huduma  zilizoathirika zaidi ni 25 ikiwemo za chanjo za kawaida, huduma za nje za kuwatembelea wagonjwa, huduma za kwenye vituo, huduma za magonjwa yasiyo ya kuambukiza, za uzazi wa mpango, za matibabu ya afya ya akili, za saratani, matibabu ya malaria, kifua kikuu au TB, dawa za kupunguza makali ya Ukimwi (VVU), huduma za meno  na nyinginezo.

31 August 2020, 16:43