Utafiti wa  UNICEF wakati wa kipindi cha karantini ya Covid-19 ni kwamba watoto wengi wamepata manyanyaso kutokana na  ukosefu wa huduma ya ulinzi katika  zaidi ya nchi 100. Utafiti wa UNICEF wakati wa kipindi cha karantini ya Covid-19 ni kwamba watoto wengi wamepata manyanyaso kutokana na ukosefu wa huduma ya ulinzi katika zaidi ya nchi 100. 

UNICEF:Zaidi ya nchi 100 zimekatiza huduma ya ulinzi wa watoto

Kwa mujibu wa utafiti wa UNICEF kutokana na sababu za COVID -19 nchi zaidi ya 100 zimepunguza huduma za ulinzi wa watoto zaidi.Ni Utafiti mpya uliofanywa kuhusu Ulinzi wa watoto kutoka katika vurugu kwenye kipindi cha COVID-19.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Kwamujibu wa uchunguzi wa kimataifa wa UNICEF, huduma za kuzuia unyanyasaji na majibu yake vimekatizwa sana wakati wa janga la COVID-19, na kuwaacha Watoto njiapanda  wakiwa kwenye hatari kubwa ya dhuluma, unyonyaji na unyanyasaji. Kati ya nchi 136 ambazo zilijibu uchunguzi wa UNICEF kuhusu COVID-19  wa athari za kiuchumi wa kijamii, nchi 104 ziliripoti kukatisha huduma zinazohusiana na ukatili dhidi ya watoto.  Karibu theluthi mbili ya nchi zilizoripotiwa angalau huduma moja iliathiriwa sana, mojawapo ni Afrika Kusini, Malaysia, Nigeria na Pakistan. Asia Kusini, Ulaya Mashariki na Asia ya Kati wana asilimia kubwa ya nchi ambazo zimeripoti kukatisha uwezekano wao wa  upatikanaji wa huduma, kwa mujibu wa msemaji Francesco Samengo, Rais wa UNICEF nchini Italia. Hata kabla ya janga hilo, udhihirisho wa watoto ulikuwa umeenea na karibu nusu ya watoto ulimwengu wanapata adhabu ya viboko nyumbani; karibu watoto 3 kati ya 4 wenye umri kati ya miaka 2 na 4 wanakabiliwa na aina za nidhamu za ukatili; na wasichana 1 kati ya 3  wenye  umri wa miaka 15 na 19 wameteswa na wenzi wao wakati fulani maishani mwao.

Uharibifu mkubwa kwa watoto wakati wa karantini

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa UNICEF, Bi Henrietta Fore  amesema : “Tunaanza kuelewa kabisa uharibifu uliofanyiwa watoto katika kuongezeka kwa vurugu wakati wa karantini kutokana na janga. Kuendelea kufungwa kwa shule na harakati za vizuizi vimewaacha watoto wengine wengi wakiwa nyumbani, na wanyanyasaji kuzidi kiasi kikubwa. Matokeo ya huduma za ulinizi na wafanyakazi wa kijamii inamaanisha kuwa watoto hawana mahali pa kupeleka maombi yao ya  msaada”. Kwa kujibu, UNICEF inaunga mkono serikali na mashirika mbali mbali katika kudumisha na kurekebisha huduma za kukabiliana na dharura kwa watoto walioathiriwa na ukatili wakati wa COVID-19.

Mifumo ya ulinzi wa watoto ilikuwa tayari yenye shida kabla ya janga

Kwa upande wa Bi Fore ameongeza kusema: “Mifumo ya ulinzi wa watoto tayari ilikuwa katika shida ya kuzuia na kujibu unyanyasaji dhidi ya watoto, na sasa janga la ulimwengu limezidisha shida hiyo na kufunga mikono ya wale ambao walipaswa kulinda wale walioko hatarini,” Aidha Bi Fore ameongeza kusema: “Watoto wengi sana hutegemea mifumo ya ulinzi wa watoto kukaa salama. Wakati wa shida, serikali zinahitaji kuchukua hatua za haraka na za muda mrefu ili kulinda watoto dhidi ya vurugu, pamoja na: kubuni na kuwekeza katika wafanyakazi wa huduma za kijamii huku wakiongeza  safu za msaada kwa watoto na kuwezesha upatikanaji wa  rasilimali nzuri ili kusaidia ujana”

Hata Sudan asilimia 60 ya watoto wanakosa huduma

Kwa mujibu wa UNICEF, nchini  Sudan Kusini asilimia 60 ya watu wanakosa huduma ya maji safi, watoto milioni 1.3 wataugua utapiamlo na kiwango cha chanjo hivi sasa ni asilimia 40 tu.  Shirika hilo limeonya kwamba watoto wengi wako hatarini na kushughulikia mahitaji yao ya msingi ni muhimu sana ili kuwawezesha kuishi wakati huu wa janga la COVID-19, kwani hatua za kupambana na gonjwa hilo zimepunguza fursa za huduma ya kusaidia  uhai wao na kubaki njiapanda.  Shirika hilo linasema watoto wengi wanakosa chanjo za msingi,  shule zimefungwa na wengi wako katika hatari ya ukatili na unyanyasaji. Licha ya changamoto hizo UNICEF na wadau wake wanajitahidi kuendelea kutoa huduma za kuokoa maisha na hadi kufikia sasa mwaka huu pekee watoto 292,000 wamepatiwa chanjo ya surau na milioni 1.6 wamepewa matone ya vitamin A.

Jitihada za Unicef wakati wa covid-19

Mbali ya chanjo, UNICEF imetoa msaada wa kisaikolojia kwa wavulana na wasichana 13,000 nchini humo na watoto wengine zaidi ya laki moja wamepata matibabu dhidi ya utapiamlo. Katika kupambana na malaria shirika hilo limeshagawa wajawazito na watoto vyandarua 148,000 vya ya kujikinga na mbu. Na kupambana na maambukizi ya COVID-19 UNICEF imehakikisha watu wengine 260,000 wamepata huduma ya maji safi na salama.   Shirika hilo limeahidi kuendelea kufanya kila juhududi kuhakikisha maisha ya mamilioni ya watoto wa Sudan Kusini yanaokolewa.

18 August 2020, 12:07