Tafuta

HARAKATI ZA UNICEF ZA KUANDAA MICHEZO NA KUWASAIDIA WATOTO KISAIKOLOJIA MARA  BAADA YA MLIPUKO JIJINI BEIRUT NCHINI LEBANON. HARAKATI ZA UNICEF ZA KUANDAA MICHEZO NA KUWASAIDIA WATOTO KISAIKOLOJIA MARA BAADA YA MLIPUKO JIJINI BEIRUT NCHINI LEBANON. 

UNICEF/LEBANO:Nusu ya familia na watoto ni waathirika wa viwewe na wasiwasi baada ya mlipuko!

Kwa mujibu wa tathimini za haraka kuhusu mahitaji ya watoto na familia zao jijini Beirut,uliofanywa na UNICEF na wadau washiriki kati ya tarehe 10/17 Agosti,kuwa nusu ya taarifa zilizobainika ni kwamba watoto na familia zao baada ya mlipuko,wanaonesha mabadiliko ya tabia au ishara za wasiwasi, kiwewe na mishtuko ya hali ya juu.

Na Sr. Angela Rwezaula -Vatican.

UNICEF ina wasiwasi kuwa watoto wengi wamepata kiwewe na wamesalia katika mshituko. Kwa mujibu wa taarifa za hivi karibuni, kuna ripoti kadhaa za watoto ambao baada ya mlipuko uliotokewa eneo la Gemmayze, huko Beirut, Lebanon. Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya kutoka kwa Marixie Mercado, msemaji wa UNICEF jijini Geneva Uswiss.

Watoto na familia zao wanaonesha wasiwasi,kiwewe na mshituko

Kwa mujibu wa tathimini za haraka kuhusu mahitaji ya watoto na familia zao jijini Beirut, uliofanywa na UNICEF na wadau washiriki kati ya tarehe 10/17 Agosti, kuwa nusu ya taarifa zilizobainika ni kwamba watoto na familia zao baada ya mlipuko, wanaonesha mabadiliko ya tabia au ishara za wasiwasi au kiwewe na mishtuko ya hali ya juu.

Aina za dalili hizi  na tabia

Tabia hizi na dalili zinaweza kujumuisha wasiwasi mkubwa; ukimya au kujitenga na wazazi na familia; ndoto mbaya za usiku na ugumu wa kulala na tabia ya fujo. Theluthi moja ya familia pia iliripoti dalili mbaya kati ya watu wazima. Ni wazi kuwa mahitaji ni makubwa amesisitza msemaji wa UNICEF. Watoto wengi watahitaji usaidizi wa kisaikolojia wa haraka na wa kudumu kukabiliana na hali iliyosababaishwa na mlipuko.

Sehemu za kutoa msaada kwa njia ya Unicef

Msaada wa kisaikolojia wa UNICEF unawakilishwa kwa njia ya vifaa vya kisaikolojia kwa watoto na wazazi; kuweka nafasi za kupendeza zinazolingana na watoto katika maeneo yaliyoathirika; aidha utoaji wa msaada maalum zaidi wa kina  na wa muda mrefu kwa wale wanaouhitaji.

22 August 2020, 11:38