Tafuta

Vatican News
Makundi ya kutumia silaha nchini DRC yamesababisha madhara makubwa ya kubaka wanawake na watoto. Makundi ya kutumia silaha nchini DRC yamesababisha madhara makubwa ya kubaka wanawake na watoto.  (AFP or licensors)

Congo DRC:Harakati za SOFEPAD kusaidia wahanga wa ukatili wa kingono

Shirika la kiraia la SOFEPAD linalohusika na usaidizi kwa wanawake na watoto waliobakwa,limechukua hatua kusaidia manusura nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Haya ni matukio ya ukatili mbaya ya kingono na ubakaji na vikundi vya upiganaji nchini humo.

Matukio ya ukatili wa kingono ikiwemo ubakaji yanaendelea kutekelezwa kimfumo na vikundi vinavyopigana na kuhuhudiwa magano hayo mara kwa mara  kwenye nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Matukio hayo yamekuwa yakiripotiwa mara kwa mara kupitia ripoti za Umoja wa Mataifa huku yakitajwa kuwa ni uhalifu sna iyo tu kwa mujibu wa sheria za DRC bali pia sheria za kimataifa.  Hata hivyo baadhi ya manusura wa vitendo hivyo wamekuwa wakiangaikia kupata haki ambapo shirika la kiraia la SOFEPAD linalohusika na usaidizi kwa wanawake na watoto waliobakwa, limechukua hatua kusaidia manusura hao.

Naye Élisabeth Furaha,daktari kwenye kliniki ya shirika hili la SOFEPAD anasema kuwa, “sisi ndiyo tunaokutana na waathiriwa wa ukatili wa kingono   mara ya kwanza baada ya tukio. Kwa mwezi Januari  mwaka huu pekee, tumepokea waathirika 46 wa ukatili wa kingono, tumewapatia dawa za virusi vya UKIMWI, vidonge vya kuzuia mimba zisizotakiwa. Wanapata pia kipimo cha kujua iwapo wamepata ujauzito au la na pia vipimo vya UKIMWI.”  Kwa mujibu wa shuhuda mwingine  ambaye ni mmoja wa waasisi wa SOFEPADI anathibitisha kuwa hali wanayoiona inakuwa si nzuri kwa kuwa, “watu wanaofika hapa wamebakwa, wameteswa, wamejeruhiwa. Na kile ambacho ni kigumu kwetu ni kwamba hivi karibuni tumeona watoto ambao wameuawa.”

Manusura wanawake na watoto, kutokana na machungu waliyopitia inakuwa vigumu sana kusimulia yaliyowakumba na hata kutaja jina, hivyo SOFEPAD imeajiri mwanasaikolojia Espérance Karungi, kwa ajili ya kuwasaidia. Bi. Karungi anasema kuwa,“Tupo hapa kusaidia wagonjwa, tunapowapokea, kwanza tunasikiliza shida zao. Tunatafuta majibu, hasa  tunatafuta mzizi wa tatizo, tunafanya yote haya kwa pamoja na mgonjwa ili wao wenyewe waweze kuamua kile cha kufanya, sisi hatupo hapa kuwaeleza cha kufanya.”

Kwa mujibu wa Shirika hili wamesema waathirika hao wanapatiwa pia msaada wa matibabu na kisheria ambapo kwa ushirikiano na wafanyakazi na ofisi ya pamoja ya Umoja wa Mataifa na DRC ya haki za binadamu yenye mamlaka ya kusaka haki na fidia kwa waathirika wa ubakaji na wanafanya kazi kwa ushirikiano na kliniki ya SOFEPADI.

Kwa njia hiyo mganyakazi wa ofisi hiyo  ya umoja wa mataifa amesema: “Tunaweka kumbukumbu ya kesi hizi ili tuweze kuziwasilisha kwenye mfumo wa sheria, hasa ule wa kijeshi, kwa kuwa wao wana uwezo wa kuamua kuhusu makosa yaliyofanywa na vikundi vilivyojihami au jeshi la serikali. Baada ya hapo wanawajibika, kama mamlaka, kuweka kumbukumbu na kuchunguza ukiukwaji huu wa haki za binadamu,”

01 August 2020, 11:31