Tafuta

Vatican News
Wakazi wa Ziwa Albert nchini Uganda,wameomba serikali ichukue hatua kuwanusuru na janga la kufurika kwa maji ya ziwa ambalo sasa linazidi kuongezeka kimo chake. Wakazi wa Ziwa Albert nchini Uganda,wameomba serikali ichukue hatua kuwanusuru na janga la kufurika kwa maji ya ziwa ambalo sasa linazidi kuongezeka kimo chake.  (AFP or licensors)

Uganda:Kuishi ndani ya maji kutokana na kuongezeka kwa Ziwa Albert!

Ziwa Albert nchini Uganda,wameomba serikali ichukue hatua kuwanusuru na janga la kufurika kwa maji ya ziwa ambalo sasa linazidi kuongezeka kimo chake na kusababisha nyumba zao kutuama kwenye maji,huku huduma muhimu za kijamii na kiuchumi zimesima kwenye maji.

Na Sr. Angela Rwezaula- Vatican

Katika muktadha wa hali ya hewa hata wakazi wa maeneo yanayozunguka Ziwa Albert nchini Uganda, wameomba serikali ichukue hatua kuwanusuru na janga la kufurika kwa maji ya ziwa ambalo sasa limesababisha nyumba zao kutuwama kwenye maji, huku huduma muhimu za kijamii na kiuchumi zikizamishwa kwenye maji. Katika ufukwe wa Butiaba ulio mkubwa zaidi kwenye Ziwa Albert ambao ni makazi ya kituo cha polisi wanamaji wa ziwa hilo na kile cha uhamiaji, kinachoshuhudiwa ni kiwango kikubwa cha maji, na watu waliokosa makazi, wakiwa hawana la kufanya, miundombinu ya umma vikiwemo vituo vya afya, hoteli na makazi vimeharibika. Wakati huo huo hamna dalili kwamba mafuriko yatarudi nyuma kutokana na kukaribia kwa msimu wa mvua wa mwezi Septemba na Oktoba mwaka huu.

Watu wanazidi kupungua katika eneo 

Hata hivyo kwa kutambua kuwa hali siyo, shwari naye diwani wa eneo hilo la wa  Mulimba Bwana Kalolo Bugoigo amesema kuwa, “tumekwisha aandika barua nyingi kwa ofisi ya majanga na wanatuma watu lakini bado hatujaona chochote. Hapo walikuwa na watu 1,500 lakini sasa wamepungua. Hali ya hospitali ni mbayá kwa sababu maji yamefika, barabara imesombwa lakini sasa inabidi wachukue mtumbwi uende hospitali na watu hawana fedha. Wajawazito ni shida zaidi, huko, shida ni kubwa sana kuliko wanavyofikiria walio juu.

Ombi kwa serikali ili watu wafunguliwe kutoka karantini

Na kiongozi mwingine mmoja wa viongozi wa serikali ya mitaa, Wanseko,  yeye amesema kuwa tangu azaliwe hajawahi kuona shida kama hiyo na wito wake wakati huu ambao eneo lao linakumbwa na janga baada ya janga kuanzia nzige, baadaye  homa ya manjano, sasa Corona na  mafuriko ni kwamba “tunaomba serikali kama inaweza kufungua hii karantini ya COVID-19 hapa Buliisa kama wilaya nyingine. Hiyo ndiyo shida kubwa sana. Tunaomba wafungue pia Buliisa ili watu watembee, ile ya kuokoa watu ziwani imetwama, ofisi ya uhamiaji, soko letu kubwa pia la samaki nalo sasa liko majini”.

Kando na haya kivuko kilichokuwa kinasaidia kusafirisha bidhaa kutoka eneo la Bunyoro hadi mto Nile magharibi, nacho kimesitisha safari zake kutokana na bandari yake kufunikwa na mafuriko. Shule zilizofungwa kwa sababu ya COVID-19 zimegeuzwa kuwa makazi kwa waliokosa malazi, na hawajui watakuwepo hadi lini  kwa kuwa maji yanawasogelea kila uchao.

Serikali kutathimini athari za janga

Naye Naibu Waziri wa huduma za umma, Bwana David Karubanga, amesema wanatathmini athari za janga hili kabla ya kutoa msaada hivi karibuni. Bwana Karubanga akiongea kwa njia ya simu amesema kuwa, “shida iliyopo ni kwamba, wakati tulipata shida hiyo, tulikuwa tunakaribia mwisho wa mwaka wa fedha wa serikali. Kwa hiyo wakifungua hazina tutawanunulia vifaa, wasife moyo, rais alitoa amri wanunuliwe vifaa, lakini haiwezekani sasa hivi kwa sababu tulikuwa tunafunga mwaka wa fedha.”

17 July 2020, 13:47