Tafuta

Tume ta Tafifa ya Uchaguzi Nchini Tanzania imetangaza kwamba, uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba na Kampeni zitaanza tarehe 26 Agosti 2020. Tume ta Tafifa ya Uchaguzi Nchini Tanzania imetangaza kwamba, uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utafanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba na Kampeni zitaanza tarehe 26 Agosti 2020. 

Uchaguzi Mkuu Tanzania ni Tarehe 28 Oktoba 2020! Kumekucha!

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC, watanzania, Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 watafanya uchaguzi mkuu kwa kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge pamoja na Madiwani. Kampeni za uchaguzi mkuu zitaanza rasmi tarehe 26 Agosti hadi 27 Oktoba 2020, huku tarehe ya uchaguzi ikianguakia siku ya jumatano ambayo ni tarehe 28 Oktoba 2020.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Semistokles Kaijage, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC amesema kwa kuzingatia Ibara ya 41 kifungu cha nne cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 pamoja na marekebisho yake, ikiambatana na vifungu kadhaa katika sheria ya uchaguzi pamoja na sheria ya uchaguzi wa serikali za mitaa sura ya 292, inatoa kibali kwa tume hiyo kutangaza ratiba ya uchaguzi. Ni katika muktadha huu, watanzania, Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 watafanya uchaguzi mkuu kwa kumchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wabunge pamoja na Madiwani.

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC amesema, mbali na mambo mengine, kampeni za uchaguzi mkuu zitaanza rasmi tarehe 26 Agosti hadi tarehe 27 Oktoba 2020, huku tarehe ya uchaguzi ikianguakia siku ya jumatano ambayo ni tarehe 28 Oktoba 2020. Kwa mara ya kwanza, Tanzania imeondokana na mazoea ya kufanya uchaguzi mkuu Jumapili ya mwisho wa Mwezi Oktoba. Hatua hii imepongezwa na watanzania wengi, kwa sababu itatoa fursa kwa watu wengi kushiriki pamoja na kuendelea kuheshimu uhuru wa kuabudu nchini Tanzania.

22 July 2020, 14:27