Tafuta

Vatican News
2019.02.011 kulinda watoto,manyanyaso dhidi ya watoto na biashara mbaya ya watu. 2019.02.011 kulinda watoto,manyanyaso dhidi ya watoto na biashara mbaya ya watu.  

Mtoto 1 kati ya 4 ulimwenguni ni mwathirika wa biashara haramu ya binadamu!

Katika mkesha wa Siku ya Kimataifa ya kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu,Shirika la Saidia Watoto linatoa taarifa kuhusu biashara na unyonyaji wa watoto wadogo,ambapo katika muktadha huo mwathirika 1 kati ya 4 ni mtoto mdogo.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Katika mkesha wa Siku ya Kimataifa ya kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu, ambayo uadhimishwa kila tarehe 30 Julai kila mwaka, shirika la Saidia watoto ( Save the Children) limetangaza toleo la X la Ripoti ya “watoto wadogo watumwa wasioonekana” tarehe 29 Julai 2020. Shirika hili katika mpango wake  uitwao “ njia za kuondokana”, linapambana kwa miaka mingi na tukio hili na zaidi kuonesha ni kwa jinsi gani dharura ya kiafya ya Covid-19 imeweka hatari kubwa na ugumu wa michakato  kusaidiwa waathirika kuweza kujitegemea kwa sababu ya mgogoro wa kutopata ajira katika sekta msingi ambazo huajiri watu waathirika wa biashara hii.

Covid-19 na madhara yake hata kwa waathiriwa wa unyanyasaji

Kufuatia na mgogoro wa Covid-19 pia umesukuma unyanyasaji wa kingono kwa watoto wadogo  barabani, ndani ya majumba yao, na kuongezeka kwa manyanyaso ndani ya mitandao ya kijamii. Barani ulaya imefunga rekodi katika udhalilishaji watoto kingono, pamoja na kujihusisha na shughuli za kingono na watoto, kuwaonyesha mambo yasiyo na heshima, kujenga urafiki na kuanzisha mahusiano na kihisia na watoto, au kuwatumia watoto kutengeneza picha za ngono.

Watoto wa kike ni waathirika zaidi

Kwa mujibu wa takwimu inakadiriwa idadi ya waathiriwa 40 milioni ya watu ambao ni waathirika wa biashara haramu au utumwa, unyanyasaji,  kulazimishwa utumwa na zaidi ni asilimia 70 ni wanawake na wakati huo karibia asilimia 20 ni watoto, ndiyo ni idadi, lakini kwa bahati mbaya ni zaidi. Na mtoto 1 kati ya 4 na ambao hawajafikia umri wa miaka 18. Janga hili limezidi kuongezeka zaidi hasa katika sehemu zenye migogoro ya kivita, uhamishashwaji wa kulazimishwa na ambao unaona ongezeka kwa watoto wengi wa kike na kiume.

Ukosefu wa msaada kwa waathiriwa wakati wa covid-19

Ukweli ambao, ikilinganishwa na idadi kubwa ya watoto wanaohusika, unathibitishwa katika takwimu chache zilizopatikana za kesi zilizoripotiwa mwaka wa 2019 na nchi 164 ulimwenguni, zaidi ya 108,000, ambayo ni 23% inahusiana na watoto na katika kesi 1 kati ya 20, hata watoto chini ya miaka 8. Hawa ni watoto na vijana mara nyingi hunyimwa haki ya kupata elimu, kwani 10% hawajuhi kusoma na kuandika na karibu robo hawakufika shule ya sekondari. Huko Ulaya, takwimu ya Tume zimasimama kwenye  kesi takriban 20,000 za uchunguzi wa mwaka 2015-2016, ambazo zinathibitisha idadi ya robo kwa watoto na zinaonyesha kiwango cha waathirika ni wanawake (68%). Hata nchini Italia usafirishaji na unyonyaji unahusisha watoto wadogo sana hata katika dharura ya Covid-19 imewafanya waathiriwa kutengwa zaidi na kuwa na ugumu wa kuwafikia.

Mitindo tofauti ya biashara ya wanadamu

Kwa hakika biashara haramu ya usafirishaji wa wanadamu hufanyika wakati watu wanapolazimishwa kuwa katika hali za kutumiwa vibaya kwa faida ya mtu mwingine na inafanyika  iwe kwa wanaume, wanawake na watoto. Biashara haramu ya usafirishaji wa wanadamu na utumwa inaweza kujumuishwa kwa mitindo mingi kama ifuatavyo: Utumwa, kufanyishwa kazi kwa lazima katika viwanda kama vile vya ukarimu, ujenzi, misitu,uchimbaji madini, au kilimo hata pia mahusiano ya kimapenzi; Utumwa wa madeni; kutumiwa vibaya kimapenzi; ndoa ya lazima; au biashara haramu kwa lengo la kuondolewa kiungo.

Hofu ya kuomba msaada

Biashara haramu ya usafirishaji wa wanadamu na utumwa ni uhalifu uliofichwa wakati mwingine, na wengi katika jamii kufumbia macho kama vile hawaoni. Biashara haramu ya usafirishaji wa wanadamu na utumwa unaweza kuwa mgumu kugunduliwa. Huenda watu wasitafute msaada kwa sababu wanaogopa adhabu kutoka kwa wanaowanyanyasa au kupoteza yao ya uhamiaji. Ishara ambazo zinaweza kuonyesha mtu anasafirishwa kiharamu zinaweza kujumuisha mahali mtu: anashurutishwa, kutishwa au kulazimishwa kufanya kazi; amepewa hali duni za kufanya kazi; halipwi au anaonekana analipia deni kubwa kwa mwajiri wake au mtu mwingine; au pasipoti yake au hati zingine za kibinafsi zimechukuliwa na mtu mwingine, na hawezi kupata hati hizi akizitaka.

 

29 July 2020, 15:29