2019.03.14 Jangwa,mawe,ukame 2019.03.14 Jangwa,mawe,ukame 

Maelfu ya wahamiaji na wakimbizi wanakufa kwa kukosa haki msingi kama binadamu!

Kwa mujibu wa ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi iliyotolewa tarehe 29 Julai 2020 imesema maelfu ya wakimbizi na wahamiaji wanakufa wakati wengine wakionja ukatili mkubwa na ukiukwaji wa hali za binadamu wakati wako njiani kukatisha Afrika Magharibi na Mashariki hadi Pwani ya baharí ya Mediterranea.

Ripoti mpya iliyotolewa 29 Julai 2020   na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, kituo cha wahamiaji mchanganyiko katika baraza la wakimbizi la Denmark MMC, na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Condo DRC, imesema maelfu ya wakimbizi na wahamiaji wanakufa huku wengine wakipitia ukatili mkubwa na ukiukwaji wa haki za binadamu wakiwa katika safari baina ya Afrika Magharibi na Afrika Mashariki na mwambao wa Afrika wa bahari ya Mediterranea.  Ripoti hiyo iliyopatiwa jina “katika safari hii, hakuna anayejali kama utakufa au utaishi” imeeleza kwa kina jinsi gani watu wengi wanavyofanya safari hizi wanateseka au kushuhudia ukatili wa hali ya juu wakiwa mikononi mwa wasafirishaji haramu wa binadamu, wanamgambo na katika matukio mengine hata mikononi mwa maafisa wa serikali.

Naye Filippo Grandi kamishina mkuu wa wakimbizi amesema “kwa muda mrefu ukatili wa hali ya juu wanaoupitia wakimbizi na wahamiaji katika safari hizo za hatari umekuwa hauonekani. Ripoti hii inaorodhesha mauaji, kusambaa kwa ghasia za kikatili zinazofanywa dhidi ya watu wanaokimbia vita, machafuko na mteso. Uongozi imara na hatua za Pamoja zinahitajika kwa nchi husika katika ukanda huo kwa msaada kutoka jumuiya ya kimataifa , ili kukomesha unyama huu, kuwalinda waathirika na kuwawajibisha wahusika wa ukatili huo.”  Ameongeza kuwa kukusanywa takwimu za vifo kwa minajili ya watu hao mchanganyiko wanaodhibitiwa na wasafirishaji haramu wa binadamu na maharamia ni vigumu sana kwani matukio mengi yanatokea kizani na mbali ya macho ya mamlaka na mifumo iliyopo kwa ajili ya kudhibiti takwimu.   Hata hivyo matokeo ya ripoti hiyo ambayo yametokana na takwimu zilizokusanywa na mpango wa ukusanyaji takwimu wa 4Mi wa MMC na takwimu kutoka katika vyanzo vingine yanaonyesha kwamba idadi ya chini ya watu waliokufa katika safari hizi za hatari mwaka 2018 na 2019 ni 1,750.

Idadi hiyo ni saw ana vifo 72 kwa mwezi na hivyo kuzifanya safari hizo kuwa miongoni mwa za hatari na kukatili maisha ya wakimbizi na wahamiaji zaidi duniani.  Kwa mujibu wa UNHCR vifo hivyo ni nyongeza ya maelfu ya watu waliokufa au kutoweka katika miaka ya karibuni wakijaribu kufanya safari za hatari kuvuka bahari ya Mediterranea kuingia Ulaya baada ya kuwasili pwani ya Afrika Kaskazini. Ripoti hiyo aidha inasema takribani asilimia 28 ya vifo vilivyoripotiwa mwaka 2018 na 2019 vilitokea wakati watu wakijaribu kuvuka jangwa la sahara. Maeneo mengine ambayo yalichangia vifo vingi ni Pamoja na Sabha, Kufra na Qatrun Kusini mwa Libya, kwengineko ni kitovu cha kuwasafirisha watu kinyemela cha Bani Walid Kusini Mashariki mwa mji wa Tripoli na maeneo mengine ya safari Afrika Magharibi ikiwemo Bamako na Agadez.  Wakati taarifa na takwimu zikiendelea kuja kwa mwaka 2020, takriban wakimbizi na wahamiaji 70 wameyhibitishwa kufa tayari mwaka huu wakiwemo wtu 30 ambao waliuawa mikoni mwa wasafirishaji haramu huko Mizdah mwishoni mwa mwezi Mei.

Katika Ripoti imeongeza kuwa wanaume, wanawake na Watoto wengi wanaonusurika katika safari hizo mara nyingi huachwa na kovu lisilofutika la athari za kiakili kutokana na madhila waliyopitia.  Kwa wengi kuwasili Libya ni kituo cha mwisho katika safari zinazoelezewa kuwa ni za hatari kubwa zilizojaa ukatili ikiwemo mauaji, mateso, ajira za shuruti na kupigwa.  Wengine wameendelea kutripoti kufanyika unyama na machafuko makubwa ikiwemo kuchomwa na Mafuta ya moto, na plastiki zilizoyeyushwa ay vyuma vilivyowekwa kwenye moto, kushtuliwa na umeme na kufungwa kama katika mazingira magumu sana.  Ripoti imeendelea kusema kwamba wanawake na wasichana lakini pia wanaume na wavulana wako katika hatari kubwa ya kubakwa na kufanyiwa ukatili wa kingono na kijinsia hususan kwenye vituo vya upekuzi mpakani na wakati wanapovuka jangwa. Kwa mujibu wa ripoti hiyo inathibitisha kuwa  asilimia 31waliohojiwa na MMC walioshuhudiwa au kufanyiwa ukatili wa kingono na kijinsia mwaka 2018 na 2019 wamesema wasafiririshaji wa watu kinyemela ndio waliokuwa wakatili wa kwanza hasa kuwafanyia ukatili wa kingono Kaskazini na Mashariki mwa Afrika wakitekeleza asilimia 60 na 90 ya ukatili katika maeneo hayo.

Hata hivyo kwa upande wa Afrika Magharibi watekelezaji wakuu wa uhalifu huo walikuwa ni vikosi vya usalama, wanajeshi, maafisa wa poli ambao ukatili wao ulikuwa robo ya ukatili wote. Wakimbizi na wahamiaji wengi pia wameripoti kushinikizwa na wasafirishaji wao haramu kuingia katika ukahaba au mifumo mingine ya unyanyasaji wa kingono.  Kati ya Januari 2017 na Disemba 2019, UNHCR iliorodhesha zaidi ya visa 630 ya usafirishaji haramu wa wakimbizi Mashariki mwa Sudan, huku karibu 200 kati yao ni wanawake na wasichana wakiarifiwa kuwa ni manusura wa ukatili wa kingono na kijinsia.  Wakiwa ndani ya Libya wakimbizi na wahamiaji wako katika hatari ya kufanyiwa ukatili zaidi kwani vita vinavyoendelea nchini humo na udhaifu wa utawala wa sharia vinamaanisha kwamba wasafirishaji wa watu kinyemela, wasafirishaji haramu wa binadamu na wanamgambo mara nyingi wanaweza kutekeleza uhalifu na kukwepa sheria.  Hadi kufikia sasa mwaka huu wa 2020 pekee wakimbizi na wahamiaji 6,200 wamewasili Libya na kuna uwezekano mkubwa idadi ikapita ile ya waliorudishwa mwaka jana ya 9,035.

Mara nyingi wanachukuliwa na kuzuiliwa kwenye vituo ambako wanakabiliwa na ukatili kila uchao na kuishi katika mazingira magumu san ana wengine huishia mikoni mwa wasafirishaji haramu ambao kuwaweka kwenye majumba maalum na kuwafanyia ukatili wa kimwili ili kupata fedha kutoka kwao. Mkuu wa MMC Bram Frouws amesema “Vitendo vibaya tunavyoshuhudiwa wakitendewa wahamiaji na wakimbizi katika safatri hizi havikubaliki. Takwimu tunazotoa kwa mara nyingine zinadhihirisha kwamba Libya sio mahali salama kuwarejesha watu. Kwa bahati mbaya hii huenda ikawa sio ripoti ya mwisho kuainisha ukiukaji huo mkubwa wa haki lakini inaongeza Ushahidi ambao hauwezi tena kupuuzwa.”

Kwa ujumla juhudi kubwa zinahitajika imesema ripoti ili kuimarisha ulinzi kwa watu hao wanaosafiri na kuwapa suluhu mbadala ya kisheria. Ushirikiano mkubwa unahitajika miongoni mwa mataifa ili kuwabaini na kuwawajibisha watekelezaji wa ukatili katika vituo mbalimbali vya safari hizo, kushirikiana taarifa muhimu na mashirika na vyombo vya sheria, kusambaratisha mitandao ya wasafirishaji haramu na kuzuia rasilimali fedha zao. Mamkala za serikali pia zinapaswa kuchukua hatua kubwa kuchunguza ripoti za ukatili unaofanywa na maafisa wa serikali. Ripoti imesisitiza kwamba hatua hizo lazima ziende sambamba na kushughulikia mizizi inayofanya watu kuchukua safari hizo na ahadi ya kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeokolewa baharini anarejeshwa hatarini Libya.

30 July 2020, 12:47