Dunia#coronavirus:Kasi ya kesi za corona Marekani,wakati Ulaya yafungua ukurasa mpya!
Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican
Licha ya kuendelea kwa virusi, nafsi mpya za kazi kwa watu milioni 4.8 zimeundwa nchini Marekani kunako mwezi Juni, kwa maana hiyo hata hii ni rekodi. Nchini Brazili, hali nyingine ya kutisha sana, iko kwa watu asilia ambao wanaishtaki serikali kwa kukosa kusimamia vema changamoto za huo. Katika Bara la Amerika ya Kusini, uzito wa shida ya kiuchumi unaonekana wazi kupitia takwimu fulani: makambpuni ya biashara yamepotea milioni 2.7 zimepotea na watu milioni 8.5 wamepoteza ajira zao (kwa mujibu wa hesabu iliyofanywa na ofisi za UN).
Maambukizi mapya zaidi ya 53,000 Marekani
Marekani imerekodi maambukizi mapya zaidi ya 53,000 ya virusi vya corona katika muda wa masaa 24 yaliyopita tarehe 2 Julai, idadi iliyowekwa pamoja na chuo kikuu cha Johns Hopkins imeonesha, ikiwa ni rekodi mpya ya siku moja wakati maambukizi yakiongezeka nchini Marekani, serikali ya Uingereza imesema inaondoa sheria ya kuwaweka watu karantini kwa siku 14 kwa watu wanaowasili nchini humo kutoka nchi kadhaa ambazo zinaonekana kuwa hazina hatari ya maabukizi ya virusi vya corona, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Ujerumani na Italia. Mabadiliko hayo yanaanza rasmi Julai 10, kiasi cha mwezi mmoja baada ya Uingereza kuanza kuhitaji watu wanaowasili nchini humo kujitenga kwa wiki mbili.
WHO bado inasisitiza kuwa na taadhari ya virusi kwani bado ni hatari
Shirika la afya ulimwenguni WHO hata hivyo limeonya siku ya Jumatano hii kuwa janga hilo linaongezeka, kwa zaidi ya nusu ya maambukizi ya dunia katika muda wa nusu ya mwaka katika mwezi Juni pekee. Na wiki iliyopita imeshuhudia viwango vya juu, wakati kesi zimefikia 160,000 katika kila siku moja ," Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema. Idadi ya maambukizi nchini Ujerumani imeongezeka kwa watu 446 na kufikia watu 195,674, na Korea kusini imeripoti maambukizi mapya 63 na , wengi wao ni kutoka ndani ya nchi hiyo nje ya mji mkuu Seoul, na kusababisha kurejea kwa vizuwizi vikali vya kuzuwia kusogeleana wakati uwezekano wa wimbi la pili la ugonjwa huo likiwatia wasi wasi maafisa.
Uganda yafungua mipaka yake kati ya Congo japokuwa na maambukizi ya virusi
Na Uganda imefungua mipaka yake ya nje na pia imepitisha hatua za kuepusha kuchangamana ndani ya taifa hilo ambalo hadi sasa limeripoti kuwa na wagonjwa 889 na hakuna hata mmoja aliyefariki dunia. Ripoti za maelfu ya raia wa DRC kukwama katika mpaka wa nchi mbili hizo, zilifikia wabunge wa Uganda ambao waliridhia kufunguliwa kwa muda mpaka kati ya Uganda na DRC kwa misingi ya kibinadamu kwenye vituo vya mpakani vya Zombo ili wakimbizi waweze kuingia na kupata huduma muhimu za kuokoa maisha. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linasema kuwa kitendo cha Uganda kufungua mpaka wake wakati huu wa janga la COVID-19, ni ishara ya mshikamano na kinaonesha jinsi ya udhibiti wa mipaka huku ikifungua maeneo ya hifadhi. Hilary Obaloker Onek, ambaye ni Waziri wa masuala ya misaada, majanga na wakimbizi amesema kuwa “hatujachoka, na hatuna ardhi ya kutosha, nchi yetu ni ndogo lakini bado tunawaruhusu kwa sababu ya huruma. Natamani jamii ya kimataifa nayo ingalikuwa na huruma na kusaidia watu hawa. Haya si matatizo yetu, haya ni matatizo ya dunia, matatizo ya kimataifa.”