Tafuta

COVID-19:Maambukizi mapya nchini Marekani yashika kasi wakati Ulaya imeanza ukurasa mpya japokuwa umakini ni muhimu COVID-19:Maambukizi mapya nchini Marekani yashika kasi wakati Ulaya imeanza ukurasa mpya japokuwa umakini ni muhimu  

Dunia#coronavirus:Kasi ya kesi za corona Marekani,wakati Ulaya yafungua ukurasa mpya!

Katika matazamio ya kilele cha shererhe za Siku ya uhuru nchini Marekani,lakini bado wanajikuta wanaendelea kuathirika zaidi na virusi vya corona kwa kasi ya kesi 53,000.Na wakati huo huo Uingereza na Ulaya wanaanza kufungua ukurasa mpya japokuwa umakini zaidi unahitajika.Nchini Brazili watu asilia bado hatarini.Uganda imefungulia mipaka yake watu wa Congo DRC.

Na Sr. Angela Rwezaula-Vatican

Licha ya kuendelea kwa virusi, nafsi mpya za kazi kwa watu milioni 4.8 zimeundwa nchini Marekani kunako mwezi Juni, kwa maana hiyo hata hii ni rekodi. Nchini Brazili, hali nyingine ya kutisha sana, iko kwa watu asilia ambao wanaishtaki serikali kwa kukosa kusimamia vema changamoto za huo. Katika Bara la Amerika ya Kusini, uzito wa shida ya kiuchumi unaonekana wazi kupitia takwimu fulani: makambpuni ya biashara yamepotea milioni 2.7 zimepotea na watu milioni 8.5 wamepoteza ajira zao (kwa mujibu wa hesabu iliyofanywa na ofisi za UN).

Maambukizi mapya zaidi ya 53,000 Marekani 

Marekani imerekodi maambukizi mapya zaidi ya 53,000 ya virusi vya corona katika muda wa masaa 24 yaliyopita tarehe 2 Julai, idadi iliyowekwa pamoja na chuo kikuu cha Johns Hopkins imeonesha, ikiwa ni rekodi mpya ya siku moja wakati maambukizi yakiongezeka nchini Marekani, serikali ya Uingereza imesema inaondoa sheria ya kuwaweka watu karantini kwa siku 14 kwa watu wanaowasili nchini humo kutoka nchi kadhaa ambazo zinaonekana kuwa hazina hatari ya maabukizi ya virusi vya corona, ikiwa ni pamoja na Ufaransa, Ujerumani na Italia. Mabadiliko hayo yanaanza rasmi Julai 10, kiasi cha  mwezi mmoja baada ya Uingereza kuanza kuhitaji watu wanaowasili nchini humo kujitenga kwa wiki mbili.

WHO bado inasisitiza kuwa na taadhari ya virusi kwani bado ni hatari

Shirika  la  afya  ulimwenguni WHO hata hivyo  limeonya siku  ya  Jumatano hii  kuwa  janga  hilo linaongezeka, kwa  zaidi  ya  nusu  ya  maambukizi ya  dunia katika  muda  wa  nusu  ya  mwaka  katika  mwezi  Juni pekee. Na  wiki  iliyopita  imeshuhudia  viwango  vya  juu, wakati kesi zimefikia  160,000  katika  kila  siku  moja ," Mkuu  wa  WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus  alisema. Idadi  ya  maambukizi nchini  Ujerumani  imeongezeka  kwa  watu 446  na  kufikia  watu 195,674, na Korea  kusini imeripoti maambukizi  mapya  63 na , wengi  wao ni kutoka  ndani  ya  nchi  hiyo nje ya mji  mkuu  Seoul, na  kusababisha kurejea  kwa  vizuwizi vikali vya kuzuwia  kusogeleana  wakati uwezekano  wa  wimbi  la  pili la  ugonjwa  huo likiwatia  wasi  wasi maafisa.

Uganda yafungua mipaka yake kati ya Congo japokuwa na maambukizi ya virusi

Na Uganda imefungua mipaka yake ya nje na pia imepitisha hatua za kuepusha kuchangamana ndani ya taifa hilo ambalo hadi sasa limeripoti kuwa na wagonjwa 889 na hakuna hata mmoja aliyefariki dunia. Ripoti za maelfu ya raia wa DRC kukwama katika mpaka wa nchi mbili hizo, zilifikia wabunge wa Uganda ambao waliridhia kufunguliwa kwa muda mpaka kati ya Uganda na DRC kwa misingi ya kibinadamu kwenye vituo vya mpakani vya Zombo ili wakimbizi waweze kuingia na kupata huduma muhimu za kuokoa maisha. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR, linasema kuwa kitendo cha Uganda kufungua mpaka wake wakati huu wa janga la COVID-19, ni ishara ya mshikamano na kinaonesha jinsi ya udhibiti wa mipaka huku ikifungua maeneo ya hifadhi. Hilary Obaloker Onek, ambaye ni Waziri wa masuala ya misaada, majanga na wakimbizi amesema kuwa “hatujachoka, na hatuna ardhi ya kutosha, nchi yetu ni ndogo lakini bado tunawaruhusu kwa sababu ya huruma. Natamani jamii ya kimataifa nayo ingalikuwa na huruma na kusaidia watu hawa. Haya si matatizo yetu, haya ni matatizo ya dunia, matatizo ya kimataifa.”

03 July 2020, 11:26