Tafuta

Yemen:Watu wakiwa kwenye mstari kupokea vocha katika kituo cha usambazaji wa chakula kinachoungwa mkono na Mpango wa Chakula Ulimwenguni huko Sanaa Yemen:Watu wakiwa kwenye mstari kupokea vocha katika kituo cha usambazaji wa chakula kinachoungwa mkono na Mpango wa Chakula Ulimwenguni huko Sanaa 

Yemen:Umoja wa mataifa bado kufikia lengo la mchango wa dola bilioni 2.4!

Umoja wa Mataifa umekusanya nusu tu ya dola bilioni 2.4 zinazohitajika kujaribu kumaliza mzozo mkali wa kibinadamu katika nchi ya Yemen iliyokumbwa na vita na janga baada ya mkutano wa wafadhili.Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa janga la virusi vya corona ni janga juu ya majanga mengine kama la wakimbizi na wahamiaji.

Na Sr. Angela Rwezaula - Vatican

Saudi Arabia imejaribu kuchangisha dola bilioni 2.3, kama msaada kwa Yemen ambayo inakumbwa na janga la virusi vya corona, ikiwa tayari imesambaratishwa na vita vya miaka sita.  Mchango huu wa  Saudi Arabia umekusanywa katika mkutano kwa njia ya video ulioandaliwa kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa, wakati mashirika ya wahisani yakionya kuhusu  athari za virusi hivyo vinavyosambaa kwa haraka. Hata hivyo Umoja wa Mataifa umeweza kusanya nusu tu ya dola bilioni 2.4 zinazohitajika kujaribu kumaliza mzozo mkali wa kibinadamu katika nchi ya Yemen iliyokumbwa na vita na janga baada ya mkutano wa wafadhili

Uingereza imeahidi kuchangia dola milioni 200. Mkutano huo unawashirikisha Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, waziri wa mambo ya nje wa Saudi Arabia Faisal bin Farhan, na naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na misaada ya kibinadamu Mark Lowcock.  Shirika la msaada la Save the Children limeonya juu ya uwezekano wa watu milioni 5.5 kukosa chakula na maji nchini Yemen mwaka huu, wakati virusi vya corona vikiendelea kusambaa na kama vile Shirika la kusaidia watoto ulimwenguni WHO na  UNICEF.

Janga la virusi au COVID-19 ni janga juu ya majanga  mengine kama la wakimbizi na wahamiaji. Janga la virusi vya Corona, COVID-19  wakati likendelea kutetemesha maeneo mbalimbali duniani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bwana Antonio Guterres ametoa tamko lake likitaka hatua zaidi kusaidia wakimbizi, wakimbizi wa ndani na wahamiaji ambao amesema kwa makundi hayo janga hilo ni sawa na mwiba wa tatu katika majanga ambayo wanakumbana nayo. “Hivi sasa watu hao wanakumbwa na majanga matatu kwa wakati mmoja, mosi, janga la kiafya, kwani wanapoambukizwa virusi, mara nyingi kwenye maeneo walimolundika kupindukia na ambako kutochangamana hakuwezekani, huduma ya afya, maji na huduma za usafi, lishe ni sawa na anasa. Na hali ni mbaya zaidi kwa nchi zinazoendelea na zaidi ya yote theluthi moja ya wakimbizi wa ndani wamo kwenye mataifa yaliyo hatarini zaidi kupata COVID-19.”

Katibu Mkuu ametaja janga la pili kuwa ni watu hao wanakumbwa na janga la kiuchumi na kijamii, hasa wale wanaofanya kazi kwenye sekta isiyo rasmi bila kuwa na fursa ya kunufaika na mfumo wa hifadhi ya jamii.  “Ukosefu wa kipato kutokana na COVID-19, kunaweza kusababisha anguko la utumaji wa fedha kwa thamani ya dola bilioni 109, hii in sawa na robo tatu ya misaada rasmi ya maendeleo, ikimaanisha watu milioni 800 wanaotegemea fedha hizo huko nyumbani hawatozipata,” amesema Katibu Mkuu.

Katika umktadha huo Katibu Mkuu anataka katika janga hili la Corona kufirikia kwa upya mienendo au hamahama ya kibinadamu kwa kuzingatia misingi mikuu minne. Misingi hiyo ni mosi, kutambua kuwa kuengua mtu ni gharama kubwa kuliko kumjumuisha na kwamba , “mfumo jumuishi wa afya, kijamii na kiuchumi utasaidia kukabili virusi na kuanzisha upya uchumi na kuendeleza mbele malengo ya maendeleo endelevu. Pili lazima tuzingatie utu tunapokabiliana na janga hili na tujifunze kutoka katika nchi chache ambazo zimeonesha jinsi ya kudhibiti mipaka huku zikiheshimu haki za binadamu, na kanuni za kimataifa za kulinda wakimbizi.”

Msingi wa tatu ni kutambua kuwa hakuna mtu aliye salama hadi pale kila mtu yuko salama hivyo uchunguzi, tiba na chanjo lazima ziwafikie watu wote.Na msingi wa nne  ni kuhakikisha kuwa wakimbizi na wahamiaji ni sehemu ya suluhisho.  Kwa njia hiyo “Hebu na tuondoe vikwazo visivyo na maana, tutafute mbinu mpya za kuhalalisha njia kwa wahamiaji na kupunguza gharama za utumaji wa fedha,”amesema Katibu Mkuu.  Kwa kukumbusha kauli ambay amekuwa akirudia mara kwa mara amesema “hakuna taifa ambalo linaweza kukabili janga la Corona peke yake au hata suala la uhamiaji, lakini kwa pamoja, tunaweza kudhibiti kusambaa kwa virusi, tukahimili athari zake hasa kwa wale walio hatarini zaidi na tukaibuka bora kwa maslahi ya wote,” amehitimisha Katibu Mkuu.

03 June 2020, 15:56