Tafuta

Wakati harakati za kupambana na janga la virusi vya corona,serikali ya Congo Drc imetangaza kuzukwa tena kwa Ebola. Wakati harakati za kupambana na janga la virusi vya corona,serikali ya Congo Drc imetangaza kuzukwa tena kwa Ebola. 

WHO#coronavirus:Lazima kuwa makini maana virusi vya corona bado vinaua watu!

Shirika la Afya ulimwenguni linabainisha kuwa mgogoro wa virusi vya Corona umeathiri kwa kiasi kikubwa matibabu na huduma kwa watu wanaougua magonjwa mengine yasiyo ambukizwa.Wengi hawapati huduma muhimu za dawa japokuwa virusi vya corona bado vipo na vinaua.Wakati huo huo nchini Congo DRC imetangaza rasmi mlipuko tena wa Ebola.

Na Sr. Angela Rwezaula – Vatican

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la afya ulimwenguni WHO linabainisha kuwa mgogoro wa virusi vya Corona umeathiri kwa kiasi kikubwa matibabu na huduma kwa watu wanaougua magonjwa mengine ulimwenguni kote. Katika uchunguzi kwa mataifa 155 mwezi uliopita, Shirika hilo Afya la Umoja wa mataifa (WHO) liligundua kuwa watu wanaougua magonjwa ambayo si ya kuambukiza, wengi wao wakiwa katika hatari kubwa ya kupata matatizo kutokana na ugonjwa wa COVID-19 hawapati huduma muhimu ya afya na madawa wakati huu wa janga la virusi vya corona.

Uchunguzi huo unaonesha kwamba asilimia 31% ya nchi hizo zimeweka utaratibu mgumu wa huduma ama kusitisha kabisa huduma kwa matatizo makubwa ya wagonjwa wenye matatizo ya moyo au kifua kikuu, asilimia 42% kwa wagonjwa wa saratani, asilimia 49% kwa wagonjwa wa kisukari na zaidi ya nusu ya mataifa hayo yalishindwa kutoa huduma kwa watu wenye ugonjwa wa shinikizo la damu. Uchunguzi huo pia umegundua kuwa asilimia 31% ya nchi zimevuruga huduma kwa wagonjwa wa dharura wa moyo.

Congo (Drc) imetangaza rasmi janga jipya la Ebola: Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo (DRC) imetangaza rasmi janga jipya la ugonjwa wa Ebola tarehe Mosi Juni 2020  katika mji wa Kaskazini  magharibi mwa nchi hiyo huko Mbandaka. Janga hili linaongezea na lile linaloendelea katika eneo la mashariki mwa nchi  kwa  za virusi vya corona au Covid-19Waziri wa afya Eteni Longondo amesema watu wanne ambao wamefariki wamethibitika kuwa wameambukizwa virusi vya Ebola kufuatia upimaji. Mkuu wa shirika la afya ulimwenguni (WHO) Bwana Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema mlipuko wa ugonjwa huo ni kukumbusha  kuwa COVID - 19 sio kitisho pekee yake  cha kiafya ambacho watu wanakabiliana nacho.

Nchi ya Congo DRC imekuwa ikihangaika katika harakati za kumaliza janga la mlipuko wa Ebola kwa miaka miwili karibu na mipaka yake na Rwanda na Uganda, ambapo watu 2,200 walifariki dunia. Janga la hivi sasa limekuwa mlipuko wa pili uliosababisha maafa katika historia tangu kuanza kwa ugonjwa huo.  Wakiwa katika harakati za kutangaza mwisho wa mlipuko huo, kutokana na maambukizi kupungua kasi yake tangu Aprili, maafisa wamejikuta bado wanakabiliwa tena na ebola kwa upande wa mashariki ambako  kumesababisha kutotangaza hatua hiyo. Huu ni mlipuko wa 11 katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC tangu mwaka 1976.

02 June 2020, 14:09